Saturday, April 18, 2015

DOCTOR KAMBUZI ANATIBU MAGONJWA MBALIMBALI



DOCTAR KAMBUZI KUTOKA WILAYA YA SIKONGE MKOA WA TABORA ANAWEZA KUTIBU MARADHI MBALIMBALI .

MGANGA HUYO ANATIBU MGONJWA YAFUATAYO KUTIBU MIFUPA KWA MTU ALIYEVINJIKA MKONO NA MGUU,.

KUONDOA MIKOSI ,KURUDISHA WATU KAZINI .

KUTIBUKISUKARI,PUMU,KIFAFANGUVU ZA KIUME , WANAWAKE WANAOTAOKA DAMU MFULULIZO  NA KUWARUSHA KWENYE NDOA WALE WALIOTENGANA .

MAGANGA HUYO ANAPATIKANA KWENYE SIMU NAMBA 0785-829311 NA 0754-768437

IMETOSHA WATINGA MWANZA KWA AJILI YA KUTOA ELIMU KUHUSU MAUAJI YA ALBINO NCHINI

 

Katibu wa Imetosha Salome Gregory akifuatiwa na Balozi Mdimu na Issaya Mwakilasa(wakuvwang) wakiteremka toka ndegeni leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa Mwanza.







Toka kushoto Wakuvwanga, Zaytuni Biboze, Salome Gregory, Henry Mdimu na  msanii wa muziki wa reggae Jhikoman Manyika wakiwa nje ya uwanja wa ndege jijini Mwanza mara baada ya kuwasili leo asubuhi

 
Ujumbe wa taasisi ya Imetosha inayojishughulisha na utoaji elimu juu ya kumaliza unyanyapaa,  ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino nchini uliwasili jijini Mwanza leo hii saa 2 asubuhi kwa ziara ya siku 3 ambapo kati siku hizo tatu ujumbe huo utakutana na viongozi wa ki serikali na usalama wa baadhi ya mikoa na wilaya za kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza na Shinyanga. Lengo la mikutano hiyo ni kamati kujitambulisha kwa viongozi hao na kuwaeleza nini Imetosha inatarajia kufanya katika kanda hii mwezi ujao ambako pamekuwa na matukio mengi ya ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino nchini Tanzania. 

 Vile vile kamati itakuwa na siku moja ambapo itatembelea vyombo ya habari vya jijini hapa kabla ya kurejea Dar es Salaam.

Habari na picha na Mkala Fundikira wa Mkalamatukio/keronyingi blog

PSPF YAZINDUA HUDUMA YA WANACHAMA WAKE KUWASILISHA MICHANGO KUPITIA MAXMALIPO

 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Vvijana na Michezo, Juma Nkamia, (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (wapili kushoto), na Afisa Mtendaji Mkuu wa Maxcom Africa, Juma Rajabu, wakizindua huduma mpya ya wanachama wa Mfuko huo, kuwasilisha michango yao kupitia Maxmalipo. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ofisi za makao makuu wa PSPF, Golden Jubilee, katikati ya jiji leo Alhamisi Aprili 16, 2015. Kulia ni Mkurugenzi Mtendajiwa Glob al Publisher, Erick Shigongo, ambaye ndiye aliyebuni na kushawishi PSPF kutumia huduma hiyo kurahisishia wanachama wake 
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Constatina Martin, akizungumza wakati wa hafla hiyo

Naibu Waziri Nkamia

Mkurugenzi Mkuu, PSPF, Adam Mayingu

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publisher, ambaye ndiye mshawishi wa huduma hiyo, Erick Shigongo

Afisa Mtendaji Mkuu wa Maxcom Africa, Juma Rajabu

Wafanyakazi wa PSPF, wakifurahia hotuba na uzinduzi huo

Kutoka kushoto kwenda kulia, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa, Afisa Mtendaji Mkuu wa Maxcom Africa, Juma Rajabu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Myingu, Naibu Waziri Juma Nkamia, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publisher, Erick Shigongo, wakishikana mikono baada ya kuzinduz huduma hiyo

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Maxcom Africa, na wenzao wa PSPF, katika uzinduzi

Baadhi ya maafisa wa PSPF

Wafanyakazi wa PSPF

Mjomba band ikiongozwa na Mrisho Mpoto, ikitumbuiza

Baadhi ya wakurugenzi wa PSPF

Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu na mwenzake Erick Shigongo, (kushoto), wakiondoka baada ya shughuli hiyo ya uzinduzi

Naibu waziri Nkamia, akijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS)

Naibu waziri Nkamia, akisoma maelezo yaliyomo kwenye fomu hiyo, huku Meneja wa Mpango wa Uchagiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa PSPF, Mwanjaa Seme, (kulia), akisubiri kutoa msaada

Naibu Waziri Nkamia, (katikati), Mkurugenzi Mkuu Mayingu, na mwenzake wa Maxcom, Juma Rajabu, wakipiga makofi mwishoni mwa hafla hiyo

Shigongo(kulia), na mwenzake Juma Rajabu wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS wa Mfuko wa Penshni wa PSPF

Naibu waziri Nkamia, (kushoto), akijadiliana jambo na Erick Shigongo, huku Mkurugenzi Mkuu wa PSPF,Adam Mayingu, (watatu kulia), akijadiliana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Maxcom Africa, Juma Rajabu, (kulia) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, mwishoni mwa hafla hiyo

UNDP YAZITAKA REDIO JAMII KUONGEZA HAMASA WATU KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

 

DSC_0392
Mtaalamu wa mawasiliano Mradi wa uwezeshaji wa demokrasia (DEP) kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nicodemus Marcus akizungumza wakati wa kufunga warsha ya siku tatu ya kutathmini mradi wa uwezeshaji wa demokrasia na amani (DEP) kwa wanamtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) yenye lengo la kuimarisha ushiriki wa redio za jamii nchini kuelekea uchaguzi 2015 na kura ya maoni iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria Tanzania jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu,akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa mtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO FM, Bw.Joseph Sekiku na Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi.  

Na Mwandishi wetu
SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini limetoa wito kwa redio za jamii kujikita zaidi katika kutoa hamasa ya ushiriki wa wananchi katika mchakato wa uchaguzi ukiwamo kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Akizungumza matumaini ya Umoja huo katika tathmini ya mradi wa Uwezeshaji wa Demokrasia (DEP) kwa Redio za Kijamii nchini Tanzania zinazounda umoja wa COMNETA, chini ya ufadhili wa UNESCO, mtaalamu wa masuala ya mawasiliano wa UNDP Nicodemus Marcus alisema kwamba redio hizo zina kazi 5 muhimu kuelekea uchaguzi.

Alisema pamoja na kutekeleza makubaliano kati ya Umoja wa Mataifa na redio hizo kuhusu elimu kuelekea uchaguzi mkuu unaozingatia maadili ya uandishi na uwajibikaji katika mradi huo ni matumaini ya UNDP kwamba redio hizo zitatimiza wajibu wa kuhakikisha kwamba uchaguzi unafanyika kwa amani na makundi mbalimbali yanajitokeza kupitia vyama vyao vya kisiasa kuwania uongozi.

Akifafanua alisema kwamba hamasa ya watu kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura, kushiriki katika kura ya maoni,Kujitokeza kwa wingi katika upigaji kura, kuendeleza amani kuelekea katika uchaguzi mkuu na kuhamaisha makundi kuwania uongozi ni mambo matano ambayo Umoja wa Mataifa unategemea redio hizo zitafanya.

Aidha alisisitiza haja ya redio hizo kufuata makubaliano ya kuendesha elimu kwa uadilifu mkubwa ili wasijiingize katika matatizo yoyote yale yatakayokwamisha kazi ya kutoa elimu kwa umma kuelekea uchaguzi mkuu na mchakato wake.

Naye Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu ambaye taasisi yake ndiyo inayosimamia redio za jamii alisema kwamba Tathmini ya mradi wa uwezeshaji wa demokrasia (DEP) kwa radio za kijamii, umeonesha kuwapo kwa changamoto hasa katika utekelezaji wa makubaliano.
Alisema kati ya redio 28 zilizomo katika umoja wa Comneta ni redio kama 8 zilizofanya juu ya kiwango na kuonesha kwamba inawezekana kuhabarisha umma.

Ufanisi wa redio hizo umeoneshwa katika ripoti ya Umoja wa Vilabu vya waandishi wa UTPC uliopewa kazi ya kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya mwaka jana kuhusu uendeshaji wa vipindi mbalimbali vya uchaguzi katika mradi wa DEP.

Alisema redio zilizofanya vyema ni pamoja na Mpanda iliyopata alama 80 huku redio nyingine za Fadeco FM , Fadhila FM, Sibuka FM, Mazingira FM, Kwizera FM Kyela FM na Micheweni zikiwa na alama 60.

Pamoja na changamoto hiyo Bi. Rose Haji Mwalimu alisema wamejifunza kwamba kumekuwepo na kuboreka kwa vipindi kiasi ya kwamba watu wengi wanavutiwa kusikiliza redio hizo na wengine wakitaka kufanyanao kazi.

Aidha wametambua kwamba redio za jamii ndio mhimili mkubwa wa kupata taarifa mbalimbali za uchaguzi zilizofanyiwa kazi hasa uwapo wa watoa habari wa kuaminika katika jamii.

Pia alisema redio hizo zimeanza kuona umuhimu wa kufuata maadili, ushirikishaji kijinsia, utoaji wa nafasi kwa makundi mbalimbali wakiwemo walemavu na vijana katika kazi.
Hata hivyo alisema kwamba mapungufu yaliyojitokeza yalisababishwa na viongozi wa redio kupuuzia suala la uwajibikaji na pia kuwakoesha vitendea kazi watumishi husika na umbali wa maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi kutoka katika ofisi zilizopo redio husika.

Viongozi pia katika tathmini walishauriwa kuwapa motisha watendaji wao kwani walionekana kulalamikia suala la kukosa motisha katika kazi ambazo wanastahili kuzifanya ili kufuata maelekezo ya mradi wa DEP.

Wakati huo huo Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) moja ya taasisi inayotetea usalama wa waandishi wa habari maeneo ya kazi imewataka washiriki katika warsha wasipofuata maadili hawataweza kufanyakazi zao vyema ikiwa ni pamoja na kuingia katika migogoro na wadau wa habari.

Naye Balozi Christopher Liundi mshauri wa UNESCO amesisitiza pia haja ya kufuata maadili na pia kuhakikisha redio za jamii zinajijenga kupitia mtandao wao na kujiuza kwa umma.
Aidha alishauri kwamba ripoti ya UTPC igawiwe kwa wadau wote kwani imetengeneza msingi wa utendaji kazi katika radio za jamii ambazo kwa sasa zinakuja kasi katika kuhabarisha mambo mbalimbali kwa jamii hasa vijijini.

Katika tathmini hiyo ya mradi wa DEP walikuwepo wawakilishi kutoka Ofisi ya Msajili, Tume ya taifa ya uchaguzi (baba nay a Visiwani), Under the same Sun, Human Rights Defenders Coalition(THRDC) na taasisi nyingine zinazogusa masuala ya uchaguzi na amani.
DSC_0158
Mhariri wa Redio Kwizera FM ya Ngara mkoani Kagera, Seif Omary Upupu akichangia mada wakati wa warsha ya siku tatu ya kutathmini mradi wa uwezeshaji wa demokrasia na amani (DEP) kwa wanamtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA).
DSC_0166
Mhariri wa Sibuka FM, Anita Balingilaki akishiriki kuchangia mada kwenye warshi hiyo.
DSC_0289
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa washiriki wa warsha hiyo.
DSC_0020
Pichani juu na chini ni baadhi ya Wanamtandao wa redio jamii 28 nchini (COMNETA) waliohudhuria warsha hiyo ya siku tatu ya kutathmini mradi wa uwezeshaji wa demokrasia na amani (DEP) kwa wanamtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) yenye lengo la kuimarisha ushiriki wa redio za jamii nchini kuelekea uchaguzi 2015 na kura ya maoni iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
DSC_0018 DSC_0288
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza na wanamtandao wa redio jamii nchini (COMNETA) waliohuhduria warsha ya siku tatu ya kutathmini mradi wa uwezeshaji wa demokrasia na amani (DEP) iliyomalizika mwishoni mwa juma lililopita katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Sengerema FM, mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye pamoja na Mwenyekiti wa Gender and Media in Southern, Tanzania Chapter (GEMSAT) Dominica Haule.
DSC_0284
Mratibu wa Mradi wa uwezeshaji wa Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano akizungumzia ushiriki wao na majukumu kwenye mradi wa DEP kwa wana-COMNETA.
DSC_0028
Makamu mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Sengerema FM, mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye (kulia) akiwa na wadau kutoka Under the Same Sun walioshiriki kutoa mada kwenye warsha hiyo.

VIJANA WA CCM IRINGA WAMPA NGUVU KATIBU WA MKOA HASSAN MTENGA KUKOMBOA JIMBO, LA IRINGA MJINI


Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga katika kikao na baadhi ya vijana hao












KIU ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa kukomboa jimbo la Iringa Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu inazidi kuongezeka, baada ya umoja wake wa vijana (UVCCM Manispaa ya Iringa) kuahidi kuongeza nguvu ili kuufanikisha mkakati huo.



CCM ililipoteza jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa Mchungaji Msigwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayekaribia kumaliza muda wake.



Katika kikao kilichozikutanisha sekretarieti za umoja huo kutoka katika kata zote 18 za manispaa ya Iringa, Mwenyekiti wa UVCCM wa manispaa hiyo, Kaunda Mwaipyana alisema; “katika kukisaidia chama kushinda uchaguzi huo, kauli mbiu yetu ni chama kwanza mtu baadaye.”



“Tutapita katika matawi na kata zetu zote, tutafanya vikao, mikutano ya hadhara na kuwakumbusha vijana wajibu wa kukipigania chama chao ili mkakati wa kulikomboa jimbo ufanikiwe,” alisema.



Katibu wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliwaongezea hamasa vijana hao kwa kuwapa seti 60 za jezi na mipira watakazozitumia kuwahamasisha vijana hao kupitia mchezo wa soka.



“CCM ina vijana wengi sana katika jimbo hili, mnahitaji kukutana na kujipanga, tumieni mbinu zote za kukutana, iwe  vikao, mikutano na hata michezo na ndio maana nimewapa msaada huu,” alisema.



Aliwataka vijana wa chama hicho kujitokeza kwenye vikao visivyo rasmi vya maeneo yao wanayoishi na kuitetea CCM kwasababu majibu ya hoja nyingi za wapinzani wanayo.



Akiwakabidhi jezi hizo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM Mkoa wa Iringa, Ephraim Mhekwa alisema  CCM inayo nafasi ya kulikomboa jimbo hilo kama itajipanga vizuri.



“Pamoja na kwamba wapinzani walipata viti 65 katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana, wasisahau kwamba CCM ilipata viti 126; hesabu hiyo inadhihirisha chama chetu kinaungwa mkono mara mbili yao,” alisema.



Aliwataka vijana hao kuweka bendera za chama hicho kila panapostahili katika mitaa yote na akawasihi wasikubali kutumika na kukigawa chama kwa maslai ya wachache.



Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mahamudu Madenge alisema CCM itaendelea kuwepo hata kama watu wasiotaka kufuata utaratibu wataondoka.


“Wameondoka wengi, wengine hii leo ni viongozi wa vyama vikubwa vya siasa. Pamoja na kuondoka kwao CCM ipo pale pale na inaendelea kupata wanachama,” alisema

KIWANDA CHA TUMBAKU MOROGORO CHAFANYA SHERERE KUFUNGA MSIMU NA KUFUNGUA MSIMU MPYA

 

Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Tumbaku ya Tanzania Tobacco Procesing Limited (TTPL) na Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) David Crowhorst Akitoa hotuba yake wakati wa sherehe za kumaliza msimu uliopita na kukaribisha msimu mwingine pamoja na kutoa zawadi kwa wafanyakazi waliotumikia kampuni hizo kwa muda mrefu pamoja na wafanyakazi bora zilizofanyika Kiwandani hapo.Katika Hotuba yake Mkurugenzi Huyo alisema Makampuni hayoyamesaidia Mkoa wa Morogoro kuanza kuinuka kiuchumi kutokana na kutoa ajira za msimu takribani 3000 kila mwaka na kusaidia kupunguza matatizo ya uhalifu yaliyokuwa yakifanywa na vijana wasio kuwa na shughuli  za kujiingizia kipato. 
Mkurugenzi mkuu wa Makampuni ya Tumbaku ya Tanzania Tobacco Procesing Limited (TTPL) na Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) David Crowhorst Akikabidhi zawadi kwa wafanyakazi waliofanya kazi kwa muda mrefu Ambao wamefanya kazi kwa zaidi ya Miaka 15 Mfululizo.
Mkurugenzi mkuu wa Makampuni ya Tumbaku ya Tanzania Tobacco Procesing Limited (TTPL) na Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) David Crowhorst Akiwapakulia Chakula waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa tafrija hiyo
Mkurugenzi wa Ufundi wa Makampuni ya Tumbaku ya Tanzania Tobacco Procesing Limited (TTPL) na Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) Henry Lembert Akiwahudumia wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa Sherehe ya Kufunga Msimu.

Mkurugenzi mkuu w David Crowhorst akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda hicho
 Picha ya Pamoja ya waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha Tumbaku  cha Mkoani Morogoro

MABARAZA YA WAFANYAKAZI TAASISI ZA ELIMU YA JUU YATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) akiwa ameambatana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Prof. Isaya Jairo kabla ya kuzindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) lililojumuisha wawakilishi kutoka matawi 6 ya taasisi hiyo katika mikoa ya Kigoma, Singida, Mwanza , Mtwara, Dar es salaam na Mbeya.
Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akizindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) leo mjini Bagamoyo.
Wajumbe wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakiimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya kuanza kwa mkutano wao leo mjini Bagamoyo.

Wajumbe na viongozi wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) mara baada ya kuzinduliwa kwa baraza hilo leo mjini Bagamoyo. Picha na Aron Msigwa/MAELEZO.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

SERIKALI imeyata Mabaraza ya wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu kote nchini kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi, kanuni na sheria zinazosimamia  mabaraza hayo ili yawe chachu katika kuleta maendeleo ya Elimu  na mabadiliko ya kiuchumi ya taasisi hizo.

Kauli hiyo imetolewa  na Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akizindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) lililojumuisha wawakilishi kutoka matawi 6 ya taasisi hiyo  katika mikoa ya Kigoma, Singida, Mwanza , Mtwara, Dar es salaam na Mbeya.

Mhe. Mwigulu amesema kuwa iwapo mabaraza hayo yatazingatia weledi katika kusimamia masuala mbalimbali ya taasisi hizo nchini  yataleta mabadiliko ya kiutendaji katika usimamizi wa mapato na matumizi  na kutoa  ushauri utakaoisaidia Serikali kutekeleza mipango mbalimbali ya  maendeleo.

Mhe. Mwigulu ameeleza  kuwa endapo mabaraza hayo yataacha kufanya kazi kwa mazoea na kujikita katika kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa, taasisi hizo zitaongeza uzalishaji, zitakuza mapato na kutatua kero mbalimbali za wafanyakazi mahali pa kazi.

“ Napenda niweke wazi kuwa mabaraza haya  ni muhimu sana kwa wafanyakazi, hayana tofauti na bunge ,kazi yake  kubwa ni kusimamia mapato na matumizi, kushauri taasisi na Serikali juu ya utekelezaji wa  mipango mbalimbali ikiwemo ajira kwa watumishi wapya” Amesisitiza.

Akizungumzia changamato ya uhaba wa walimu na watumishi wa kada mbalimbali  katika taasisi hiyo na taasisi nyingine za Umma za Elimu ya juu amesema Serikali inaendelea  kutenga fedha katika bajeti ya kila mwaka ili kuondoa tatizo hilo.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kulishughulikia suala la usimamizi wa ziada ya mapato yanayozalishwa na taasisi za umma ili yaweze kupelekwa  katika maeneo mengine yenye uhitaji.

“Serikali tunaendelea kuangalia utaratibu wa kutumia ziada ya mapato inayozalishwa na taasisi mbalimbali za umma ili iweze kupelekwa katika maeneo mengine yenye uhitaji maana fedha hizi ni za umma,taasisi moja ya Serikali haiwezi kung’ania ziada ya mapato iliyozalisha, hizo ni fedha za umma lazima zikafanye kazi maeneo mengine yenye uhitaji hasa kwenye kugharamia mahitaji ya wodi za akina mama kote nchini”

Pia amesisitiza mkakati wa Serikali wa kuzifanya taasisi hizo za elimu ya juu kuwa na mamlaka yake katika kuajili watumishi wake na kjitegemea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ndiye Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda  akizungumza na wajumbe wa baraza hilo amesema kuwa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka 5 imepata mafanikio makubwa ya kuongeza  ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi Bilioni 6 za mwaka 2010 hadi kufikia shilingi Bilioni 18 mwaka 2014/2015.

Amesema Taasisi hiyo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uhaba wa miundombinu, ufinyu wa bajeti , uhaba wa walimu wenye shahada za uzamivu (PhD)  na watumishi kimeendelea kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaodahiliwa kutoka  7635 waliodahiliwa mwaka 2011/2012 hadi kufikia 14974 mwaka 2014/2015.

“Licha ya kuendelea kufanya vizuri taasisi yetu inakabiliwa na tatizo la waalimu katika matawi yetu yaliyo mikoani ,jambo hili hutufanya tutumie gharama kubwa kuwasafirisha kutoka makao makuu kwenda kufundisha wanafunzi wetu wanaochukua michepuo ya Biashara, Uhasibu, Rasilimali Watu, Ununuzi na Ugavi,Uhasibu katika Sekta ya Umma na Masoko na Mahusiano kwenye matawi yetu” Amesisitiza.  


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya wizara ya Fedha wa Taasisi hiyo Prof. Isaya Jairo akizungumza na wajumbe waliohudhuria mkutano huo amesema kuwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)katika kukuza na kuongeza mapato ya ndani na kupunguza utegemezi kutoka serikalini itaendelea kufanya shughuli kibiashara ,kufanya utafiti, kutoa ushauri katika Nyanja za uhasibu, ununuzi na ugavi kote nchini.

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI(MUWSA) YAKAMATA WEZI WA MAJI

Watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,wakiwa katika nyumba moja ambayo inadaiwa mmiliki wake alikuwa akiiba maji baada ya kujiunganishia kinyemera licha ya kukatiwa huduma hiyo kwa muda mrefu.
Wafanyakazi hao wakiongozwa na afisa uhusiano wa mamlaka hiyo ,Frolah Nguma na mkuu wa kanda ya Rau ,Selemani Zabron na fundi Aminiel Swai baada ya kufuatilia katika eneo hilo walibaini wapi wizi wa maji unafanyika.
Hivi ndivyo ilivyooonekana katika mauongio ya mteja wa mamlaka hiyo ambaye mtuhumiwa wa wizi wa maji alifanya usanii wa kujiungia maji bila ya kulipia huku mzigo wa kulipia ankala ya maji ikibaki kwa jirani yake aliyeunganisha bomba kwenye line yake.
Fundi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Aminiel Swai akiondoa bomba liliunganishwa kwa wizi .
Mkuu wa kanda ya Rau wa mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi Selemani Zabron akifukia eneo ambalo hujuma ya kujiunganishia maji ilikuwa imefanyika.
Mmiliki wa nyumba hii ndiye line ya kupeleka maji kwake imekutwa ikiwa imefanyiwa hujuma na kulazimika kulipa bili ya matumizi ya maji kwa nyumba mbili.
Watumishi wa MUWSA wakitizama kama maji yanatoka katika nyumba hiyo mara baada ya kuondoa bomba ambalo lilikuwa likitumika kupeleka maji katika nyumba nyingine kwa njia ya wizi.Hata hivyo katika operersheni hiyo Mtuhumiwa pamoja na mkewe walilazimika kuikimbia nyumba yao na kutelekeza watoto wao wawili wakiume wenye umri wa kati ya miaka miwili na minne.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.