Saturday, August 25, 2012

MWENYEKITI CCM UYUI AKANUSHA KUTUMIA FEDHA ZA MABALOZI


Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM anayemaliza muda wake wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Abdalah Kazwika amekanusha vikali kuhusika na ubadhilifu wa fedha za mabalozi kama inavyoenezwa na baadhi ya wagombea wenzake.

Hivi karibuni kumekuwepo na uvumi kwamba Mwenyekiti huyo alitafuna fedha ya mabalozi kila mmoja shilingi 5,000 ambavyo hulipwa kila mwezi kama posho ya kujikimu.

Kazwika alitoa kauli hiyo katika ofisi ya chama hicho wilaya ya Uyui,  muda mfupi mara baada ya  kurejesha fomu ya kuomba kutetea wadhifa wake tena kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.


Alisema kuwa kumekuwepo na maneno mengi na hasa kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi ndani ya chama, kwamba anahusika upotevu wa shilingi milioni 12 ambazo zilitolewa na CCM makao makuu kwa ajili ya kuwalipa viongozi wa CCM kata, matawi na mabalozi.

“Nashangaa sana kuhusishwa na hizo pesa mimi sio mtendaji na pesa hizo zilikuja kwa katibu wangu, anapo simama mtu na kunituhumu mimi eti nimekula hizo pesa ananione.

“Hapo niwe mkweli hizo pesa nilizisikia na pia zilisomwa katika kikao cha kamati ya Siasa lakini mimi mwenyewe kuziona sijaziona hata kidogo, na kiutaratibu wa CCM mimi kama Mwenyekiti siruhusiwi kugawa pesa, mwenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Katibu na si vinginevyo” alisisiza Kawika.

Aidha alisema kuwa kila anapoenda katika ziara zake amekuwa akikumbana na maswali kama hayo na hasa la fedha za mabalozi.

Alieleza kwamba kuna baadhi ya watu wamekuwa wakipita kwa wana-chama wa CCM sehemu mbalimbali na kumpaka matope kuwa yeye ndiye amechakachua fedha za mabalozi hao pamoja na viongozi ngazi ya kata na matawi, kitu ambacho ni uzushi utupu ambao unalenga kumchafulia jina ili asichaguliwe tena kushika wadhifa huo.

Kuhusu uhai wa chama, Kazwika alijinasibu kwamba wakati anashika madaraka yake kwa mara ya kwanza mwaka 2002 ya kuwa Mwenyekiti wa wilaya hiyo, alikuta kunawanachama 17000 elfu tu, lakini kwa sasa ameweza kukusanya jumla ya wanachama hai 38000 elfu.

Alibainisha kuwa iwapo atachaguliwa tena kukiongoza chama katika wilaya hiyo atahakikisha anaua makundi yote ndani ya chama na kuleta umoja, amani, upendo na mshikamano baina ya wana CCM.

Mwisho

IGALULA KUJENGEWA UJASILI WA KUHOJI KUHUSU KATIIBA MPYA


Na. Mwandishi wetu

SHIRIKA la Mtandao wa Maendelea wilaya ya Uyui mkoani Tabora (UCODEN) linatarajia kutumia shilingi milioni 30 kwa ajili ya kufanya midahalo mbalimbali kwa wananchi ili kuwajengea ujasili wa kutoa maoni yao bila woga, kuhusu madiliko ya katiba mpya.

Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Shirika hilo, Ally Magoha wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, kuhusiana na kazi hiyo watakavyoifanya katika kipindi cha mwaka mmoja.

Magoha alisema kwamba lengo kuu la midahalo hiyo ni kuwajengea ujasili na uwezo wananchi ili wakati ukifika wakutoa maoni kwenye tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya watoe maoni yao bila ya woga wowote jinsi ambavyo wanataka katiba iwe na muundo upi.

Alieleza kwamba iwapo wananchi watajengewa uwezo huo bila shaka katiba itayoundwa itakuwa na tija zaidi kwa wananchi kuliko ilivyo sasa katiba hiyo haiwapi uhuru wa kufanya mambo yao ya msingi.

“Midahalo hiyo itawajengea ujasili wananchi juu ya kuwahoji  wajumbe wa tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya pia nao kutoa maoni wanahitaji katiba hiyo iwe na muundo wa namna gani”alisema Magoha.

Kwa upande wake Mratibu wa Shirika hilo ,Christopher Nyamwanji alisema kuwa lengo lingine la kufanya midahalo hiyo pia ni kukuza mahusiano kati ya wananchi na viongozi wa Serikali.

Nyamwanji pia alisema midahalo  hiyo pia italenga kutoa elimu kwa wananchi hao, kuhusu tabia nchi na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanapelekea kwa sasa katika baadhi ya mikoa hapa nchini mvua kutonyesha kwa wakati.

Alisema kama uhusiano utakuwawepo baina ya wananchi na viongozi kazi za miradi mablimbali ya maendeleo zitasonga mbele na kwamba midahalo inatarajiwa kufanyika katika vijiji vya Igalula na Goweko wilayani Uyui.

Mwisho.



MADEREVA WATAKIWA KUWA NA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI


MADEREVA

Madereva  nchini wametakiwa kuwa wangalifu na kufuata  sheria za barabarani  kikamilifu ili waweze kuokoa maisha  ya wasafiri na kupunguza ongezeko la ajali za barabarani hapa nchini

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Saveli Maketta, alipokuwa akikabidhi vyeti kwa madereva wa magari na pikipiki waliopatiwa na mafunzo na chuo cha udereva cha Dodoma, ambacho kinatambuliwa na serikali. 

Alisema iwapo kama madereva watafuata sheria na taratibu za usalama barabarani hakuna shaka kwamba ajali zinazoikabili taifa hivi sasa zitapungua na hivyo kusaidia kuokoa maisha ya watu  wanaokuwa safarini. 

Alisema udereva usiozingatia nidhamu na sheria umekuwa chanzo kikubwa cha ajali za barabarani hapa nchini ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaasa vijana walioingia katika fani hiyo kuwa makini na kuepukana na tabia ya kuleta mzaha wawapo barabarani. 

Mkuu huyo wa wilaya ya Kaliua, alikabidhi vyeti vya udereva kwa  vijana 154 katika wilaya hiyo, ambao walifundishwa na mkufunzi wa udereva anayetambuliwa na chuo cha usafirishaji cha Taifa  (NIT) Marijani Majani. 

Mwenyekiti wa chama cha madereva nchini (TDA) mkoa wa Tabora, Ali Kitenge, aliishukuru serikali kutokana na kuweka program za mafunzo kwa madereva hali ambayo alisema itasaidia uwepo wa umakini kwa madereva wenye sifa zinazotakiwa kuendesha magari na hivyo kupunguza ajali za barabarani.

Mwisho.

Friday, August 24, 2012

RAIS MSTAAFU AKIWA NA KAFUMU

Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin W. Mkapa akiwa na mgombea wa Ubunge Jimbo la Igunga kupitia Chama Cha Mapinduzi Peter Dalali Kafumu, aliyefanikikwa kushinda kiti hicho kwa kura 26000, lakini Mahakama kuu imetengua Ubunge wake.

DR. PETER DALALI KAFUMU WAKATI WA KAMPENI

Dr. Peter Dalali Kafumu akiwa na mkewe wakati wa harakati za kampeni za kuwania Ubunge Jimbo la Igunga,

SIKU YA HUKUMU YA DR. DALALI PETER KAFUMU

Wananchi wa Wilaya ya Nzega wakiwa nje ya mahamaka ya Kuu wakisikiliza hukumu ya kesi ya kupinga  matokeo ya uchaguzi Jimbo la Igunga

Wananchi wakisubiri kuanza kwa kesi ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi Dr. Kafumu Dalali

Wapenzi na mashabiki wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Wakishangilia baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kutengua matokeo ya uchaguzi Jimbo la Igunga.


Mashabiki wa chadema wakiondoka katika eneo la Mahakamani

SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA 2012

IFIKAPO TAREHE 26 AUGUST, 2012 NI SIKU YA KUHESABU WATU NA MAKAZI KWA TAIFA ZIMA, HII NI KWAAJILI YA MAENDELEO YA WANANCHI NA TAIFA KWA UJUMLA. TAFADHALI TOA USHIRIKIANO KWA MAENDELEO YA TAIFA LAKO.

Thursday, August 23, 2012

WAJITOKEZA KUWANIA NAFASI YA MWENYEKITI MKOA NA WILAYAN TABORA

Na Lucas Raphael,Tabora
CCM

Kinyanganyiro cha kuwania nafasi ya wenyeviti wa mkoa na wilaya kimepamba moto baada ya wananchma wa chama cha mapinduzi kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho.

Waliojitokeza kuchukua fomu hizo ni wale waliokuwa wakishikilia nafasi zao za uongozi na wengine kujitokeza kwa mara ya kwanza kuwania uongozi wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu msaidizi wa mkoa wa Tabora ,Elia Kimaro alisema kwamba hadi kufikia jana ni mwenyekiti anayemaliza muda wake Hassani Wakasuvi ndiye alikuwa amechukua fomu kwa ajili ya kutetea kiti chake hicho.

Alisema kwamba muda bado hupo hadi angasti 28 mwaka huu ambayo itakuwa ndio siku ya mwisho kuchukua na kurudisha fomu hizo kwa nafasi ya mwenyekiti na wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (nec)

Katika wilaya za Uyui waliojitokeza kuchukua fomu kuwani nafasi ya mwenyekiti wa wilaya hiyo ni Mussa Ntimizi ,Hamisi Bundala na Abdallla Kazwika ambaye natetea nafasi yake ya kiti.

Katika wilaya Igunga katibu wa wilaya hiyo Mary Maziku aliwataja waliochukua fomu hizo kwa nasafi ya wenyekiti wa wilaya hiyo ni Costa Olomi na Felix Mkunde.

Nzega aliyekuchukua fomui hizo ni Patric Bulubuza pekee hadi leo hiyo sikonge aliyechukua nafasi hiyo fomu za kuwania nafasi ya wenyekiti Abed Malifedha  ambapo kwa Tabora mjini aliyechukua fomu hiyo ni Simon Madolu .

Mwisho
Na Lucas Raphael,Tabora

Mwenyekiti.

Baraza la madiwani la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora, limemchagua diwani wa kata ya Ilolangulu katika wilaya hiyo, Said Shaaban Ntahondi,  kuwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mwaka 2015 utakapofanyika uchaguzi mkuu nchini.

Katika kikao chake kilichofanyika makao makuu ya wilaya hiyo mji mdogo wa Isikizya na kuhudhuriwa na madiwani wote 29 wa halmashauri hiyo,  madiwani hao walimchagua diwani Said Shaaban Ntahondi, kuiongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu
.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Uyui, Doroth Rwiza, alisema Ntahondi amepata kura 29 kati ya kura 29 zilizopigwa na hivyo kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Diwani Ntahondi, amechaguliwa kushika nafasi hiyo kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mashaka Kalyuwa, aliyeuwawa kwa kupigwa risasi na majambazi nyumbani kwake Ipuli mjini Tabora, Mwanzoni mwa Mwaka huu.

Aidha Kikao hicho kwa kauli moja kilimchagua diwani wa Igalula, Seleman Kapalu kuwa makamo mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, kapalu alipata kura 29 kati ya kura 29 zilizopigwa na madiwani wa halmashauri hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Said Ntahondi, alisema kuwa atajitahidi kuiongoza halmashauri hiyo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na kwamba anachohitaji ni ushirikiano kutoka kwa madiwani na watumishi.
Alisema kwamba bila ushirikiano kati ya wataalam na madiwani kazi kwake itakuiwa ni ngumu kwanio umajo na mashikamano utakuwa ni ndogo ,hivyo rai yake kubwa ni kupata ushirikiano kutoka sehemu zote mbili na tatu kwa viongozi kuwatumikia wananchi kwa nguvu na kasi.
Ntahodi kabla ya kupata nafasi hiyo alikuwa ni makamo mwenyekiti wa halmashauri hiyo na mara baada ya kufariki mwenyekiti wake aliongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha miezi 4.

Mwisho.
NA LUCAS RAPHAELTABORA
 
MAKALA YA MICHEZO.
 
“ili kiwango cha michezo mkoani Tabora kiweze kukua wanatakiwa wapatikane viongozi watakaojitoa kwa hali na mali kwa ajili ya kuendeleza soka la mkoa wa huo.
 
Kusimamia michezo kwa vitendo ,kukuza vipaji na kuwa na mbinu mbadala kwa ajili ya kukuza viwango vya michezo mbalimbali ya mpira wa miguu wa wananwake ,watoto na watu wazima wenye umri wa miaka 20 hadi 25.
 
Bila ya kuchaguliwa kwa na viongozi bora wenye nia ya dhati ya kuendeleza soka la mkoa  huu,  tena wenye uwezo wa kujitolea na kuendeleza michezo mkoani hapa,katu kiwango cha mpira hakitafanikiwa kukua kama ilivyokuwa miaka 20 iliyopita”
 
Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF kutoka mkoani Tabora, Yussuf Kitumbo katika mahojiano maalum na gazeti hili,amesema kwamba wakati umefika mkoa wa Tabora kuchangua viongozi watakaokuwa tayari kujitolea kwa ajili ya soka la mkoa huu.
 
Amesema kwamba katika kipindi cha kupata viongozi wa wilaya hakikishe wanapata viongozi wanaopenda michezo ili kujenga timu bora ya uongozi katika kukuza kiwango cha soka mkoani Tabora kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
 
Amesema kuwa umefika wakati  sasa wa kuhakikisha soka la mkoa linakua ili kuweza kurejea rekodi ya miaka iliyopita ambayo soka linakuwa bora na kuweza kuwatoa wachezaji bora kwenye timu ya mkoa na timu ya Taifa .
 
Kitumbo amesema kwamba kwa kipindi hicho cha kuelekea kwa uchaguzi huo wa TAREFA basi hakuna budi kuhakikisha viongozi wanachaguliwa kuongoza vyama vya michezo wilayani wawe wakereketwa wa michezo kwa maana ya kujitolea kwa hali na mali katika maswala ya michezo .
 
Amesema kwamba bila kuwa na uongozi mzuri katika vyama vya michezo ndio chanzo kikubwa cha kushuka kwa kiwango cha soko mkoani hapa .
 
Amesema kuwa wakipatikana viongozi wazuri katika vyama hivyo na kufanya kazi kama timu ya ushindi, ushindi utapatina kwa ushirikiano bila kuwepo kwa makundi ,soka la Tabora litakuwa na mafanikio yatakayonekana.
 
Amesema kwamba viongozi hao wakipatika na kuongoza vizuri vyama vya soka na chama cha soka mkoa wanaweza kufanya vizuri katika kukuza soka la mkoa wa Tabora.
 
Mjumbe huyo wa mkutano mkuu wa Tff amendelea kusema kwamba dawa ya kukuza soka la mkoa ni kupata viongozi wenye nia ya dhati ya kukuza kiwango cha mpira wa miguu na kukuza vipaji kwa vijana chini nya miaka 13,15 na 17.
 
“Viongozi watakao changuliwa warejeshe imani kwa wadau wasoka ili waweze kujitokeza kuzichangia timu za mkoa zinazoshiriki katika michezo mbalimbali ya ndani na nje ya mkoa huo”amesma kitumbo.
 
Amesema kwamba wadau wa michezo hawaoni nini wachangia kwani uongozi  wa chama cha soka mkoa wa Tabora ,TAREFA umeshindwa kufanya kazi kama timu ili kuweza kuwavuta wadau wa soka ambao wapo tayari kuchangia maendeleo ya soka .

Amesema kwamba lazima viongozi wanaopata nafasi ya kukiendesha chama cha soka mkoa wa Tabora wahakikishe  wanarudiasha imani kwa wadau kwenye mchezo wa mpira wa miguu”
 
Amesema kwamba hilo likifanyika tutakuwa tumeishirikisha jamii nzima kwenye soka ambapo mwisho wa siku watakuwa na uwezo wa kuchangia soka mkoani hapa.
 
Amesema hali hiyo inatokana na viongozi wa mkoa wa cha soka umedhamirie kukuza kiwango cha mpira mkaoni Tabora kuwa timu zake zote zinafanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
 
Kitumbo amesema kwamba chama chochote cha  soka kama akina mipango madhubuti ya kuendeleza soka ni lazimakitakuwa akina dira wale mwelekeo wa badaye , chama kiwe na fedha kwa ajili ya kuzisaidia timu ambazo zinashiriki katika mashindano mbalimbali.
 
Akizungumzia swala la vyama kukosa mipango na ukosefu wa fedha na kushindwa  kuzisaidia timu zinashirikia katika michezo mbalimbali amesema tatizo hilo linasababishwa na viongozi kutojitoa katika kukuza soka la sehemu husika na kushindwa kupandisha hata daraja, hawana mipango endelevu ya michezo.
 
Amesema kuwa iwapo cha cha soka cha sehemu husika kikiwa na mikakati madhubuti ya kupata fedha na kiaminika akiwezi kushindwa kukosa fedha kwa ajili ya kuisaidia timu ambayo inashiriki katika mashindano ndani na nje ya mkoa wa Tabora.
 
Amesema kwamba mkoa wowote upate timu zinashirikia katika ligi daraja la kwanza kama ilivyotokea kwa mkoa wa Tabora huko morogoro,iwapo chama kingikuwa na fedha za kutosha timu hizo zingeweza kufanya vizuri.
 
Amesema ni lazima tuvisaidie vilabu kimkakati kwa maana ya kujipanga lengo likiwa ni kupata timu itakayoshiriki ligi ya voda com na wilaya nazo ziwe na mikakati ya kuhakikisha kupandisha timu daraja Fulani hayo yote ni mikakati ya chama cha soka cha mkoa .
 
“Lakini chama cha soka wilaya na  mkoa hawana mipango endelevu yenye lengo la kukuza kiwango cha soka ”amesema kitumbo .
 
Hata hivyo amesema kwamba mipango mingine ya chama cha soka kwa viongozi wanaotaka nafasi ya kuongoza vyama vya soka kuhakikisha wanasimamia soka la watoto wadogo ili kesho na keshokutwa TAREFA wawe na wachezaji katika vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ikiwemo AZAM,YANGA na SIMBA.
 
AIDHA amesema kuwa Tabora kuwepo na kituo cha michezo kwa ajili ya kukuza vipaji vya watoto hasa wanaoshirikia Copa coca cola.kichosimamiwa na chama cha soka mkoa wa Tabora .
 
Haya yote yanaweza kufanikiwa kukuza kiwango cha soka mkoani hapa iwapo wanamichezo wataondokana  na malumbano mbayo yanachangia kwa kiwango kikubwa kudidimiza soka .
 
Licha ya hivyo viongozi kushindwa kuonesha mshikamano wakuendeleza soka la mkoa wa Tabora na kusababaisha hata wadau wa michezo kushindwa kushirikiana na chama hicho kwa kukosa imani na viongozi waliopa madarakani.
 
Wadau mbali mbali wa soka mkoani hapa wamempongeza mjumbe huyo kwa kujitole kuendeleza soka la mkoa huu licha ya kuwepo kwa malumbanao kwa baadhi ya viongozi .
 
Wadau hao wamesema mdau huo wa soka  amekuwa akujitolea kuzichangia timu za Polisi  na Rhino Rangers za mjini hapa ambazo  zinashiriki ligi daraja la kwanza pamoja na timu ya Majimaji ambayo ni bingwa wa mkoa kwa msimu  uliopita.
 
Mwisho