Wednesday, September 26, 2012

Makamu Meya wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Waziri Mlenda akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufun guzi wa nyumba ya Mzee Laurent Mchele katika kijiji cha Uramba kilometa kumi kutoka mjini Tabora. 



SINGIDA WALALAMIKIA MAVAZI YA WANAFUNZI WA KIKE VYUO VYA UHAZILI NA UHASIBU










 Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akizungumza na wananchi wa kata ya Utemini manispaa ya Singida ahamasisha maadili mema kwa watoto.
(Picha  na Nathaniel Limu). 


Na Nathaniel Limu.

Baadhi ya ya wakazi wa manispaa ya Singida wamelalamikia mavazi yanayovaliwa na wanafunzi wa vyuo vya uhazili na uhasibu, kwa madai kwamba yanachangia kuharibu maadili ya watoto wao.

Malalamiko hayo yametolewa na wakazi  hao kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Utemini mjini Singida katika mkutano ulioitishwa kwa ajili ya mkuu wa wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi kuhamasisha ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za kata.

Wakifafanua, wamesema wanafunzi wa vyuo hivyo na hsasa wa kike, wanavaa nguo ambazo ni kinyume na maadili ya kitanzania na zinachochea vitendo vya ngono zembe.

“Mheshimiwa mkuu wa wilaya, nguo zinazovaliwa na hawa wanafunzi wa kike, zinaacha nusu ya mwili ubaki kama alivyozaliwa na mbaya zaidi zinawabana kupindukia, na Kwa upande wa wanafunzi wa kiume, wao suruali zao wanazivaa chini kabisa ya makalio” almeema Ntandu Jumbe.

Wamesema uvaaji wa nguo unaofanywa na wanafunzi wa vyuo hivyo, unachochea kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa vijana na atoto wao kuongezeka mara dufu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Queen Mlozi amesema tatizo hilo na yeye amelibaini lakini hata hivyo, akadai kuwa hayo ni matunda ya utandawazi.

Amesema tatizo la kuharibika kwa watoto kwa maana ya kutokuwa na maadili mema ni la karibu kila familia na hivi sasa ni kubwa mno.

Queen Mlozi amesema kwa kweli dawa pekee hivi sasa ya kupambana na janga hili la watoto kuharibika, ni sisi sote wazazi, walezi, viongozi wa serikali na wa madhehebu ya dini, kuunganisha nguvu zetu pamoja na kuimba wimbo mmoja, nao ni wa malezi bora kwa watoto wetu.

Aidha, mkuu huyo wa wilaya ameagiza kwamba kuanzia sasa kila vikao vya maamuzi vya ngazi mbalimbali, ajenda yao kuu iwe ni mkakati wa kudhibiti kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa watoto.


WILAYA 40 NCHINI ZA PATIWA MADAWA YA KUTIBU UGONJWA WA VIKOPE







Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akiangalia moja ya boksi la dawa za kutibu ugonjwa wa vikope aina ya Zithromax zilizotolewa na kampuni ya kimataifa inayofanya utafiti na utengenezaji wa Dawa ya PFIZER kutoka Marekani leo jijini Dar es salaam. Wengine ni Bi. Caroline Roan makamu wa Rais wa kampuni hiyo huduma za jamii (katikati) na Dkt. Peter Mbuji Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga(kushoto).



Na. Aron Msigwa –MAELEZO. , Dar es salaam. 

Wilaya 40 nchini zitarajia kunufaika na mkakati wa kutokomeza ugonjwa wa Vikope kufuatia kampuni ya kimataifa inayofanya utafiti na utengenezaji wa Dawa ya PFIZER kutoka Marekani kupitia mpango wa kimataifa wa kupambana na Ugonjwa wa vikope kuipatia Tanzania msaada wa dawa aina ya Zithromax kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya dawa hizo leo jijini Dar es salaam ,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekua ikifanya mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Vikope na kutoa elimu ya afya kwa jamii juu ya namna ya kupambana na ugonjwa huo. 

Amesema kuwa Wizara ya afya inaendelea kupambana na magonjwa yaliyosahauliwa ambayo yamekua yakiathiri watu kwa muda mrefu na kuongeza imekua ikisisitiza mbinu mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo zikiwemo matumizi ya dawa, uboreshaji wa mazingira ,matumizi ya maji safi na salama pamoja na utoaji wa elimu. 

 Ameongeza kuwa kampuni ya PFIZER kupitia mpango wa Kimataifa wa kupambana na Ugonjwa wa Vikope kwa mwaka 2012 imeipatia Tanzania msaada wa chupa 239,952 za dawa ya Zithromax zikiwa katika mfumo wa kimiminika na chupa za vidonge 17,520.

 “Ni matumaini yangu kuwa dawa hizi zitatoa msukumo wa kuondoa magonjwa haya kwa sababu tuna mkakati wa jumla wa kutokomeza na kuondoa kabisa ugonjwa huu na matokeo sasa ni mazuri” amesema. 

Kuhusu usalama na ubora wa dawa hizo Dkt. Mwinyi amesema kuwa dawa hizo zinakidhi viwango vya kimataifa na zina ubora na usalama kutokana na matumizi yake katika maeneo mbalimbali nchini toka mwaka 1999. 

“Nnachosema sasa tiba tunayo, ubora na usalama wake ni wa uhakika wananchi msiwe na hofu yoyote kwa sababu dawa hizi hazina madhara” alisisitiza. 

Kwa upande wake makamu wa Rais wa upande wa mahusiano na huduma za jamii wa kampuni hiyo Bi. Caroline Roan amefafanua kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwa jamii. 

Bi. Caroline amesema kuwa toka mwaka 1999 kampuni ya Pfizer imekuwa ikitoa msaada wa dawa za kukabiliana na ugonjwa wa Vikope/ Takoma kupitia mpango wa Kimataifa wa kupambana na ugonjwa huo (ITI). 

Kampuni ya Pfizer ambayo imekua ikitoa misaada ya dawa kwenye sekta ya afya nchini toka 1999 ina makao yake nchini Marekani ni miongoni mwa makampuni makubwa duniani yanayofanya kazi za utafiti, utengenezaji na usambazaji wa dawa katika nchi mbalimbali duniani ikiweka msukumo katika kuhakikisha kuwa binadamu mahali popote pale alipo anapata tiba sahihi na huduma bora za afya.

RADI YAUA WANAFUNZI DARASANI

Na Lucas Raphael,Tabora

MWANAFUNZI mmoja wa darasa la 3 katika shule ya msingi msiliembe amekufa hapohapo baada ya kupiga na RADI na wangine 23 wajeruhiwa na watano wamelezwa katika hospital ya mkoa kitete kwa matibabu zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana (leo)Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Edward Bukombe alisema kwamba tukio hilo septemba 25 mwaka huu ,katika kijiji cha msiliembe kata ya mabama , majira ya saa 8 alasiri katika shule ya msingi msiliembe wilaya ya Uyui mkoani hapa

Kaimu kamanda huyo alimtaja aliyefariki kuwa ni Husna Ramadhani (10) aliyekuwa akisoma darasa la tatu katika shule akiwa na wenzake daasani wakati mvua hiyo ilipoanza .

Bukombe alisema kwamba wakti mvua hiyo ilipoanza kunyesha ikiambatana na radi wanafunzi wa darasa la tatu na nne wote walikuwa wamekaa kwenye chumba kimoja cha darasa wakiwa wanaendelea kujisomea ndio radi hiyo ilipopinga na kusabisha kifo hicho.

Kaimu kamanda huyo wa jeshi la polisi mkoani Tabora alisendelea kusema kuwa watoto wengene 23 waliuokuwepo ndani ya darasa hilo nao walipata madhara ,lakini watoto 5 walipata madhara makubwa na kulazimika kulazwa katika hospital ya mkoa kitete kwa ajili ya matibabu .

Aliwataja waliozwa kuwa ni Bundala Juma (10) wa Darasa la nne ambaye ameumia kwenye macho hayaoni vizuri,Hamisi Mashaka(10) anayesoma darasa la tatu,Cresesia Simon (12) mwanafunzi wa darasa la nne,Kwangu Luone (12) anayesona darasa la nne na Zaituni Ally(10) mwanafunzi wa darasa tatu.

Alisema kwamba wanafunzi walijeruhiwa wanaendelea na matibabu katika hospia; hiyo na wanendelea vizuri kwa mujibu wa taarifa waliopata asubuhi hii kutoka kwa daktari wa mkoa .

Hata hivyo kaimu kamanda bukombe amewataka walimu  kuakikisha wanafunzi mara baada ya kuona mvua zinaaza kunyesha basi wanatakiwa kuingia madarasni kwa ajili ya kuepuka radi za aina hiyo.

mwisho

Tuesday, September 25, 2012































MWENGE WAZINDUA NYUMBA BORA ICHEMBA





















DIWANI WA KATA YA ICHEMBA JOHN KADUTU WAKIINGIA NDANI YA NYUMBA NA KIONGOZI WA MBIO YA MWENGE WA UHURU 

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE CAPT HONEST MWANOSSA  WAKIWA NA MKUU WA WILAYA YA KALIUA NA MBUNGE WA JIMBO LA URAMBO MAGHARIBI WAKIWA WAMEKAA KWENYE SOFA NDANI YA NYUMBA YA DIWANI WA KATA ICHEMBA 

MWENGE WA UHURU MARA BAADA YA KUWASILI KATIKA KUZINDUZI WA NYUMBA BORA KATIKA KATA YA ICHEMBA


MKUU WA WILAYA YA KALIUA SAVERI MAKETA AKIWA NA KIONGOZI WA MWENGE WA UHURU PAMOJA NA DIWANI WA KATA YA ICHEMBA JOHN KADUTU


KIONGOZI WA MWENGE WA UHURU CAPT HONEST MWANOSSA AKIKATA UTEPE WA NYUMBA BORA ILIYOPO KATIKA KATA YA ICHEMBA WILAYA KALIUA MKOA WA TABORA



KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU CAPT HONEST MWANOSAA AKIZUNGUA NYUMBA BORA KATIKA KATA YA ICHEMBA NA MBENI YAKE NI MWENYE NYUMBA HIYO NA DIWANI WA KATA HIYO JOHN KADUTU 

MWENGE WA UHURU WAZINDUA NYUMBA BORA ICHEMBA


 Na Lucas Raphael,Tabora
WANANCHI wilayani Kaliuwa mkoani Tabora wametakiwa kujenga nyumba bora zitakazo weza kudumu kwa muda mrefu tofauti na sasa baadhi yao hujenga nyumba zisizo bora kulingana na vipato vyao vya  kilimo cha tumbaku katika wilaya hiyo.
Hayo yalisemwa jana na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Capt Honest Mwanosa wakati akizundua nyumba bora ya diwani wa kata ya Ichemba John Kadutu yenye thamani ya million 40.
Alisema kuwa baadhi ya wakulima wa maeneo hayo hulima mazao ya biashara lakini kipato hicho hutumika kwa matumizi yasiyo ya msingi ikiwa na ulevi pamoja na kuoa wake wengi kuzidi uwezo wao.
Honest akiwahutubia wanan chi wa Kata ya Ichemba alisema kuwa ujen zi wa nyumba bora kwa mkulima ni mhimu zaidi kuliko kuendelea na ulevi pamoja na anasa mbalimbali.
Aliwataka wananchi hao wabalike na kuiga mfano wa Diwani huyo pamoja na wananchi wengine katika kata hiyo ili kubadili maisha pamoja na mazingira ya kata hiyo.
Akitoa maelekezo kwa wafanya kazi wa sekta mbalimbali kiongozi huyo wa mbio za mwenge aliwataka nawao kujenga nyumba bora kama hiyo ili kuwa mfano kwa wananchi wengine pamoja na kujijengea msingi bora wa maisha.
Daadhi ya wananchi wa kata hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti walimpongeza Diwani huyo kwa kuonesha mfano bora wa nyumba hiyo na kutoa ahadi ya kuiga mfano huo.
John Kitudu Diwani wa kata hiyo alisema kuwa nyumba hiyo imeghalimu kiasi cha shilingi milioni  40 kwa ujenzi wake na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kuiga mfano huo.
Alisema kuwa wananchi wa kata hiyo wanakipato kikubwa lakini baadhi yao hutumia kipato hicho kwa matumizi ya pombe pamoja na starehe na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kubadilika kutokana na hali hiyo.
Katika wilaya hiyo mwenge huo umezindua miradi yenye thamani ya shilingi milioni 300 ambapo bado upo mkoani hapa ukiendelea kuzindua miradi mingine kwa wilaya nne zilizo salia.

Mwisho.


WANAFUNZI 4000 WASHINDWA KUFANYA MTIHANI WA HABARI


Na Lucas Raphael,Tabora

Wanafunzi wapatao 4000 katika wilayani Igunga mkoani Tabora wameshindwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo na vifo na  utoro unaochangiwa na wazazi wa watoto kuwatka kuchanga mifugo .

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa wilaya ya Igunga Elibariki Kingu katika Mahafali ya pili ya Darasa la saba ya shule ya msingi ya sent Leo iliyopo wilayani Igunga.

Kingu alisema kuwa wanafunzi hao walianza wakiwa darasa la kwanza zaidi ya 12800 mpaka kuhitimu darasa la saba 8000 ambapo wanafunzi ambao hawakufanya mtihani wa kuhitimu darasa hilo walikuwa 4000.





Alisema kuwa wazazi wanatakiwa kuwafuatilia watoto wao pindi wanapo anza shule mpaka kuhitimu darasa husika ili kupambana na adui uchinga.

Alisema idadi hiyo ya wanafunzi 4000 kutofanya mtihani niidadi kubwa hivyo wazazi wanapaswa kubadili mara mmoja ili kuhakikisha kila mtoto anapata Elimu hiyo ya msingi.

Alisema kuwa mzazi atakaye bainika kuto mpeleka mtoto shule ama kuchangia mtoto kuto enda shule hatua kali zitachukuliwa ikiwa na kupelekwa mahakamani kwa mzazi husika atakaye bainika na tuhuma hizo.

’’wakazi wa Igunga badilikeni mjue uchungu wa Elimu kwa watoto wenu hivyo basi niabu kati ya watoto 12800 watoto 4000 hawajafanya mtihani hii haipendezi razima mzazi wajibishwe wazazi hawa ni wazembe,atakaye bainika hatua kari zitachukuliwa ikiwa na kufishwa mahakamani’’alisema Kingu.

Aliwaagiza viongozi wa vijiji,kata pamoja na viongozi wa dini kutoa hamasa kwa wananchi kuhakikisha watoto wanaandikishwa shule pamoja na kuwafuatilia watoto hao mpaka hatua ya mwisho ya mitihani yao.

Sababu mbalimbali zilizosababisha mpaka watoto hao kutofanya mtihani huo ni pamoja na utoro wa kupindukia,kuolewa kwa wan afunzi wa kike, shuguli za kiufugaji pamoja na shuguli za kilimo.

Meneja wa shule hiyo Coaster Olomi alisema kuwa wazazi wanapaswa kutambua umuhimu wa Elimu na kuwakazania watoto hao kupenda shule nakuongeza kuwa jamii za wafugaji zi Elimishwe zaidi ikiwa na kuachana na imani potofu ambazo bado mpaka sasa zinaendelea.

MWIsHO.



Monday, September 24, 2012

WATAKIWA KUACHA KAZI KAMA WANAONA MISHAHARA HAITOSHI


Na Lucas Raphael,Tabora


NAIBU waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Goodulack Ole Medeye amewataka watumishi wa wizara hiyo ambao wanaona mshahara wanaolipwa na serikali hautoshi waandike baarua ya kuacha kazi ,badala ya kuendelea kuomba na kuwashawishi wananchi kwa Rushwa kwa watu masikini.

Kauli hiyo wa wziri inafuatia kutolewa kwa malalamiko kutoka kwa wakazi wa mkoam wa tabora na wilaya zake juu ya watumishi wa Idara hiyo kukithiri kwa kuomba na kupokea Rushwa .

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Mandeleo ya makazi, alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Sekondari ya Uyui mjini Tabora, ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazohusiana na masuala ya ardhi na makazi.

Medeye aliwaambia wafanyakazi idara ya ardhi katika Manispaa ya Tabora kwamba kama kunamtumishi wa idara hiyo ambaye anaona mshahara anaolipwa hautoshi hana budi kuandika barua ya kuomba kuacha kazi badala ya kuwa wanaomba rushwa kwa wananchi wanaohitaji huduma ya kupatiwa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi.

“Mimi naona kama unaona mshahara wako unaolipwa na serikali haukutoshi, andika barua kwa mkuu wako ya kuacha kazi nasio kuwadhurumu wananchi masikini” alisema Medeye.

Alisema kuwa kwa muda mrefu sasa amekuwa akisikia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi dhidi ya watumishi wa idara ya ardhi katika Manispaa ya Tabora hivyo akamwagiza mkuu wa wilaya ya Tabora ,Suleiman Kumchaya, kuwachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwafirisi mali zao, watumishi wa idara hiyo watakaobainika kupora maeneo ya wananchi na kuwauzia matajili.

Kwa upande wake Naibu Waziri huyo alielezea jinsi ambavyo alitaka kupewa rushwa ya dola laki 8 ili atoe upendeleo wa kugawa eneo fulani na kampuni moja ambayo hata hivyo hakuitaja, lakini alikataa kuchukua.

“Mimi nilikataa rushwa ya dola laki 8 sasa ninyi hapa Tabora nawashangaa mnaendekeza vijirushwa hivi vidogo vitawasaidia nini, kwanza angalia huyu mtu unayechukua rushwa kwake anahali gani” alihoji Medeye.

Katika mkuatano huo mmoja wa wananchi ,Juma Rashid Nasssro alimtaka Naibu Waziri Medeye, kuondoka na Mwenyekiti wa baraza la ardhi wilaya ya Tabora, kwamadai kwamba amekuwa akitoa maamuzi katika kesi za ardhi kwa kuwapendelea watu wenye kipato cha juu nasio masikini.

Aliendelea kumshambulia Mwenyekiti huyo wa baraza la ardhi mbele ya Naibu waziri kwamba, amekuwa akiwapendelea matajili na kwanyanyasa wanyonge katika kesi za ardhi, na kusisitiza kwamba ahamishwe Tabora.

“Mheshimiwa Waziri tukuomba unapoondoka uondoke na huyu Mwenyekiti wa baraza la ardhi Tabora, huyu anatunyanyasa sana

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la ardhi wilaya ya Tabora Emmanuel Sululu, alipotakiwa kuthibitisha madai hayo alisema kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.

“Unajua mtu anapokwenda mahakamani huwa anatarajia kuwa atashinda, hakuna anayeenda mahakamani kwa matarajio ya kushindwa, sasa mimi ninapotoa maamuzi ya haki kwa mtu ambaye sio mwelewa ataona napendelea, kumbe hapana” alisema Sululu.

Mwisho  


Friday, September 21, 2012

BENKI YA KCB YATOA MSAADA KWA HOSPITALI ZA AMANA NA MWANANYAMALA

PICHA NA HABARI JUMA KAPIPI


Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB  Tanzania ,Christina Manyeye, akiwa amemshika mmoja wa watoto wenye umri wa siku moja waliozaliwa katika wodi ya wazazi ya Amana jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea waodi hiyo, baada ya kutoa msaada wa Mashuka 116 na Mashine ya joto ya kutunzia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wake  ( Baby Warmer Mashine) Vitanda Vitano vya kujifungulia akina mama wajawazito vvyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 15.640.000.Vilivyotolewa na Benki ya KCB Tanzania.

Mkuu wa Idaraya ya Uhazini wa beki ya KCB Tanzania Sam Kimath akimkabidhi msaada wa Mashuka 116  Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Asha Mahita, na Diwani wa kata ya Ilala Edson Fungo wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam, jumla ya vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 15,640,000. Vilitolewa msaada na benki hiyo kwa ajiri ya kusaidia hospitali hiyo ya Amana. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB Christina Manyeye.

Mkuu wa Idaraya ya Uhazini wa beki ya KCB Tanzania Sam Kimath akimkabidhi msaada wa Mashuka 116  Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Asha Mahita, na Diwani wa kata ya Ilala Edson Fungo wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam, jumla ya vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 15,640,000. Vilitolewa msaada na benki hiyo kwa ajiri ya kusaidia hospitali hiyo ya Amana. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB Christina Manyeye.

 Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB Christina Manyeye, akimkakabidhi  Mganga msaidizi wa Hospitali ya Mwananyamala DR.chrispian Kayola  Mashine ya Kutunzia joto ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda,(babyWarrmer Machine) yenye thamani ya shilingi Milioni 7.8.iliyotolewa na Benki ya KCB Kwa ajili ya kusaidia jamii inayopata huduma katika hospitali hiyo.wanao shuhudia ni Diwani wa kata ya Ilala Edson Fungo na Mganga msaidizi wa Hospitali ya Amana DR.Shaany Mwaruka. Hafla hiyo ilifanyika katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.



Na Mwandishi Wetu

 
Benki ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa vifaa  kwa wodi ya akina mama wajawazito


vyenye thamani ya shilingi milioni 15,640,000 kwa hospitali  ya  Amana katika uzinduzi wake wa   wiki ya jamii.
 

Akizungumza katika hafla fupi ya mabidhiano ya vifaa hivyo  yaliyofanyika hospitalini hapo,  Mkuu wa kitengo cha masoko na jamii wa benki ya KCB Christine Manyenye  alisema  Msaada huo unalenga kupunguza vifo vya akina mama na watoto. 

Manyenye  alisema, Benki ya KCB inatambua umuhimu wa  afya ya mama na mtoto na ndiyo maana iliona kuwa ni jambo zuri kuelekeza msaada huo muhimu kwa kundi hilo Kila mwaka. 

"Kwa kawaida tunaangalia sehemu yenye mahitaji sana msaada na kutoa mchango  sehemu hiyo, Kwa mfano tumegundua kuwa hospitali zetu haswa hizi zinazohudumia watu wenye kipato cha chini zina matatizo mengi na ndiyo maana leo tumekuja kutoa mchango hapa Amana,alisema Manyenye

"Ni matumaini yetu kuwa, vifaa hivi vilivyotolewa na Benki ya KCB vitachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha utoaji huduma kwa akina mama na watoto na hivyo kujenga taifa lenye jamii ya watu wenye afya bora," aliongeza.
 

Mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali hiyo  Dokta Shani Mwaruka aliishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema kuwa utasaidia  kuboresha huduma kutokana na kupatiwa vifaa hivyo.

"Hali za hospitali zetu hizi za serikali siyo nzuri sana kutokana na ukosefu wa vitendea kazi, hakika tunahitaji msaada ili tuweze kutoa huduma bora na ndiyo maana tunatoa shukrani za pekee kwa benki ya KCB, alisema Dk.Shani

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashine ya joto kwa watoto wachanga waliozaliwa bila kutimia, vitanga vya kujifungulia 5, vifaa vya kusaidia wakati wa akina mama wajawazito kujifungua 10, mashuka 116, drums 20 na Cord clamp 100.

MWANANYAMALA

Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, jana ilipokea msaada wa mashine ya joto kwa watoto waliozaliwa bila kutimia (baby warmer )  yenye thamani ya shilingi 7,850,000 kutoka katika Benki ya KCB Tanzania.


 Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo, mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo Christine Manyenye  alisema msaada huo umetolewa baada ya kubaini uwezo mdogo wa hospitali za umma kuhudumia watoto wanaozaliwa bila kutimia (pre mature) 

"Kabla ya kufukia uamuzi wa kutoa msaada huu tulichunguza na kugundua kuwa huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wao wa kuzaliwa bado si nzuri kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo tuliona ni jambo zuri kuelekeza msaada wetu kwa kundi hili" alisema Manyeye huku akibainisha  kuwa benki ya KCB imekuwa ikielekeza zaidi misaada yake kwenye makundi yenye mahitaji  makubwa na yenye uchache wa rasilimali za kutatua matatizo za aina mbalimbali.

Kwa upande wake Mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali hiyo  ya Mwananyamala Dokta Chrispian Kayolai aliishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao.


"Tunachangamoto nyingi ambazo tunakutana nazo wakati wa kutoa huduma na haswa kwa ajili ya vitendea kazi,Msaada huu tumeupokea leo utasaidia sana kuboresha huduma na tuna kila sababu ya kuishukuru sana benki ya KCB," alisema Dk Kayolai

Kwa mujibu wa Manyenye, katika kuadhimisha wiki ya jamii hospitali za KCMC Moshi, Mwembeladu Zanzibar, Morogoro na Mount Meru ya Arusha itanufaika na misaada itakayogharimu shilingi milioni 79,040,000/-