Sunday, September 29, 2013

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 LIKIENDELEA USIKU HUU NDANI YA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA.

Muigizaji wa filamu lakini pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya,aitwaye kwa jina la kisanii Shilole akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa ccm kirumba usiku huu.
Anaitwa Christian Bella ambaye alikuwa akifanya vyema sana kwenye bendi ya muziki wa dansi ya Acudo,akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013.
Anaitwa Neylee,msanii wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema sana kwenye anga ya muziki huo,akiimba kwa hisia mbele ya mashabiki wake usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea 2013.
Pichani kati ni Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu za mikononi ya Zantel akiwa na marafiki zake wakilifuatilia tamasha la serengeti fiesta 2013 usiku huu ndani ya uwanja wa ccm kirumba,ambapo wakazi wa jiji la Mwanza wamejitokeza kwa wingi.
Kila kona ni ileee full maraha tuu,huku wakiburudika na vunywaji mbalimbali kutoka kampuni ya bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la serengeti fiesta wakishirikiana na PSI kupitia bidhaa yao ya Salama kondom.
Vijana machachari kabisa kutoka kinondoni wakitambulika kwa jina la KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza ngoma za Michael Jackson mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza.
Mmoja wa sanii waliofanya vyema sana katika shindano la BSS,Walter Chilambo,akiimba usiku huu kwenye jukwaa la Serengeti fiesta.
Mashabiki wa fiesta kibao usiku huu ndani ya ccm kirumba.
PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA YAFUNGIWA



Serikali imeyafungia  kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia  27 Septemba,2013  kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari  na makala  za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi  wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano  ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa  kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu  hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la  tarehe 27 septemba,2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa  adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo  wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI
2013”  kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya
habari waraka huo ulikuwa wa Siri  haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari
yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI”  habari  hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa  mkali mwenye hasira.Habari na picha  hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika
maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la
 ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo  halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi  linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi  lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.

Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya
kiislam  mbwa ni najisi hapaswi kuingia  katika maeneo ya ibada.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia  tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti  hili limeonywa mara nyingi  lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa   kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za  fani ya
Habari.

Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia  maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20  Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA  DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo  “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.

Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18  Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha  Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo  ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia  kompyuta  kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika  .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la  Polisi linahusika  na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa  kumwagiwa tindikali na  waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.

Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.

Kwaujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya
  wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama  wavione kuwa
haviwasaidii.

Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali  imelifungia gazeti la Mtanzania  kutochapishwa kwa muda wa siku  tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332)  la tarehe 27 septemba,2013,. Serikali inawataka wamiliki,wahariri  na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili  yataaluma uandishi wa habari.

Serikali inawataka wamiliki na hasa  wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa  vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na  uzalendo wa hali ya juu.

Serikali inavionya vyombo vya habari  vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia  hatua kali ikiwemo ya kuvifungia .Serikali haitakubali kuona vyombo vya  habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani  nchini.
Imetolewa na

MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013

"KIWANDA CHA NYUZI TABORA KINAKABILIWA NA UCHAFU WA MAZINGIRA,NI HATARISHI KWA WATUMISHI"

 

Mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda cha nyuzi Tabora ambaye ni mjamzito amekutwa akifanya kazi huku akiwa amekaa chini  kulingana na mazingira mabaya ya kikazi ambapo pamoja na watumishi kudai maslahi bora lakini bado wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu.
Naibu Waziri wa viwanda na biashara Bw.Gregory Teu akimuhoji Meneja wa kiwanda cha nyuzi Tabora kuhusu uendeshaji wa kiwanda hicho ambacho kwasasa kimekuwa kikikabiliwa na mazingira yasiyostahili huku yakitishia usalama wa watumishi wa kiwanda hicho.
Mmoja kati ya watumishi wa kiwanda cha nyuzi



MUNDE AWATAKA WANAFUNZI WANAOHITIMU DARASA LA SABA KUEPUKA DAWA ZA KULEVYA NA NGONO!!!

Thursday, September 26, 2013

Mbunge wa vitimaalumu na mjumbe wa NEC CCM akizungumza katika mahafali ya darasa la Saba ya Shule ya msingi Isike Bi.Munde Tambwe ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kuepuka vitendo hatarishi vya kujihusisha na masuala ya ngono hatua ambayo pia itawasaidia kuepukana na janga la ukimwi huko mitaani.
Mbunge huyo Bi.Munde alipata fursa ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu ikiwa ni ishara kwa wanafunzi hao kukamilisha elimu ya msingi ambayo ndio chanzo cha kuianza safari ya elimu nchini.
Mh.Munde akikabidhi msaada wa shilingi laki tatu kwa mkuu wa Shule hiyo Bw.Charles Kidifu kama sehemu ya mchango wake katika shule hiyo ya Isike inayohitaji fedha kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya madarasa mawili.
Wahitimu wa darasa la Saba Shule ya msingi Isike wakati wa mahafali yaliyofanyika shuleni hapo.
Mh.Munde sambamba na kutoa msaada wa fedha hizo pia alikabidhi Ngoma zinazotumika wakati wa gwaride la Shule kwa wanafunzi,Munde alifanya hivyo ikiwa ni kumbukumbu yake muhimu ya kusomea katika shule hiyo elimu yake ya msingi.

CCM TABORA MJINI WAANZA KURUMBANA,KIGOGO AFANIKIWA KUWAZUIA WANAOKISAIDIA CHAMA HICHO

Kadri joto la kisiasa linavyozidi kupamba moto mjini Tabora Kigogo mmoja wa Chama cha Mapinduzi hatimaye amefanikiwa kutumia njia ya kuwazuia wanaokisaidia chama hicho kwa kufikisha malalamiko yake kwenye kamati ya maadili ya CCM ngazi ya Taifa eti kwa madai kwamba nia yao si kukisaidia chama hicho bali ni kujiandaa kuwania nafasi ya Ubunge.

Habari za ndani tulizozipata kutoka maeneo tofautitofauti zimeeleza kuwa kigogo mmoja ambaye jina tunalihifadhi amelazimika kumtumia mjumbe mmoja wa CCM ambaye kutokana na maradhi yanayomsumbua ametumia mwanya huo wa kumshurutisha aandike barua na kuipeleka kwa mkono wake kwenye kamati hiyo ya maadili akidai kuwa wapo jamaa Tabora mjini ambao wanatumia mikutano ya hadhara kwa maandalizi ya kuwania nafasi za udiwani na ubunge mwaka 2013 kwa kuitumia jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Tabora mjini jambo ambalo ni kinyume na taratibu na kanuni za katiba ya CCM.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hii ambavyo tunavihifadhi,Mjumbe huyo ambaye moja kati ya masharti aliyopewa kutokana na msaada wa matibabu aliopatiwa na Kigogo huyo ni kuhakikisha anaandika kwa makini malalamiko hayo ambayo hata kwenye fikra zake hakuwanayo huku akisahau kabisa  msaada wa kwanza aliopatiwa na hao alioshurutishwa kuwalalamikia  kwenye kamati ya maadili jambo ambalo pia limewachukiza wanaccm wa karibu yake ambao wamekuwa bega kwa bega katika kumsaidia adha ya magonjwa yanayomsumbua tangu awali.

Hata hivyo walalamikiwa wa sakata hilo waliofikishwa katika kamati ya maadili CCM taifa,ambao wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali kama wafanyavyo vyama vya Chadema na Cuf katika hatua ya kuviimarisha vyama vyao,wao kupitia Jumuiya ya umoja wa vijana ccm wilaya ya Tabora mjini  wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kufanyika mbinu chafu za kutaka kuwazuia kuendelea na mikutano hiyo hatua inayodaiwa kufanywa na Kigogo huyo kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi bila kujali CCM ina nafasi gani kwa wananchi wa Tabora.

Hata hivyo duru za kisiasa zinasema kuna kila dalili kwa CCM hapa mjini Tabora itaendelea kutokuwa na mvuto wa kisiasa kwa kile kinachodaiwa kuwa kuwepo kwa dhana potofu kwa baadhi ya vigogo kwamba chama hicho kinapendwa na wananchi tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere jambo ambalo wanasahau kuwa hivi sasa watu waliowengi wamekuwa na mwamko na zaidi ya yote pale vyama vya upinzani vinapotumia udhaifu wa utendaji wa Viongozi wa chama tawala ambao ndio kinaongoza serikali.

Wakati vyama vya siasa hapa mjini Tabora vikiendelea kuvuta kasi ya kujiimarisha kisiasa lakini jambo la kushangaza zaidi Chama cha Mapinduzi,Chama tawala, kimekuwa katika mivutano isiyokuwa na tija kwa Chama hicho hatua ambayo inafikia eti mmoja wa viongozi anatafuta namna ya kuzuia wenzake wasiweze hata kukutana na wananchi kusikiliza matatizo yao akihofia kuwa anaweza akapoteza nafasi yake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Baadhi ya wanaccm baada ya kutolewa amri ya kusitishwa shughuli za mikutano ya hadhara inayofanywa na Jumuiya ya UVCCM wilaya ya Tabora mjini,wameamua kutelekeza shughuli zote za chama hicho huku wakieleza kuwa liwalo na liwe hata ikibidi chama kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.





  

Monday, September 23, 2013

HAPPINESS WATIMANYWA NDIYE MLIMBWENDE WA TANZANIA BAADA YA KUTWAA TAJI LA REDD'S MISS TANZANIA

 
Happiness Watimanywa akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa mwaka huu.Kushoto ni mshindi wa pili, Latifa Mohamed na kulia ni mshindi wa tatu,
HAPPINESS WATIMANYWA | MISS TZ 2013
Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa Onyesho la Taifa la Urembo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakifungua shindano la mwaka huu kwa kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki. Shindano la mwaka huu ambalo limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji Tanzania.Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji cha Redds limefanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali,vyuo nk wameshiriki.
Warembo walioingia hatua ya kumi na tano bora 
Jaji Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Dkt. Ramesh Shah akitangaza Warembo walioingia hatua ya tano bora. 
Warembo walioingia hatua ya tano bora,toka shoto ni Happiness Watimanya,Elizabert Peter,Clara Bayo,Lucy Tomeka pamoja na Latifa Mohamed.
Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakipita jukwaani na mavazi ya aina mbali mbali wakati wa Onyesho la Taifa Redd's Miss Tanzania 2013 linalofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam usiku huu. 
Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya hapa nchini,Lady Jay Dee akitoa burudani kwenye Onyesho la Redd's Miss Tanzania 2013,linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.

Fainali za Miss Tanzania 2013 ndio zinaendelea usiku huu ndani ya Mlimani City jijini Dar es Salaam. Gari ndo hilo hapo Je nani ataingia ndani na kuliendesha? Tusubiri Majaji. Hadi sasa Top 5 ndo ishatajwa.

Wadau wakifuatilia shindano la Redds Miss Tanzania lililomalizika kwa Kumpata Mlimbwende Happyness Watimanywa Kutoka Dodoma
PICHA ZOTE: CATHBERT KAJUNA (Kajunason Blog) NA OTHMAN MICHUZI (Mtaa kwa Mtaa Blog)

TAMKO KWA UMMA JUU YA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI VYA UMMA NCHINI TANZANIA


 Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu hivi karibuni ulikamilisaha ziara ya kuangalia na kutathmini mahitaji ya watetezi wa haki za binadamu yaani mashirika yanayotetea haki za binadamu wakiwamo waandishi wa habari. 

Kwa mujibu wa mazungumzo na maelezo tuliyoyapata katika dodoso zilizojazwa na waandishi wa habari wa vyombo vya umma inaonekana kuna uhasama mkubwa unaojengeka baina ya waandishi wa vyombo vya umma na wananchi ama na vyama vyao vya siasa. 

Mgogoro huu wa kiusalama baina ya wananchi na vyama vyao dhidi ya waandishi wa habari wa vyombo vya umma umejitokeza mara nyingi kwenye mikutano ya kisiasa na kwenye mivutano ya raia kwa upande mmoja na serikali na wawekezaji kwa upande mwingine. 

Mtandao umebaini kuwa hali hii tete ya kiusalama kwa waandishi wanaoripoti katika vyombo vya umma unazidi kukua na huenda ukawa na madhara makubwa kwa wanahabari hawa hadi kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. 

Matukio ya kufukuzwa, kupigwa mawe na kudhalilishwa kwa waandishi hawa yamekuwa ni mengi kwa mujibu wa viongozi wa Vilabu 16 vya waandishi wa habari ambavyo Mtandao ulivitembelea kujua hali ya usalama kwa waandishi.

Mifano halisi ni kama ifuatavyo; takriban katika mikoa yenye rasilimali au upinzani mkubwa wa kisiasa kama Mbeya, Iringa, Arusha, Kigoma , Dar es Salama kumekuwepo na matukio ya kuwadhalilisha waandishi wanaoripoti katika vyombo vya umma.

Matukio haya ni kama yale yaliyomkuta mtangazaji wa Shirika la Utangazi la Taifa (TBC), Bw. Marin Hassani Marini pale alipozongwa na wananchi siku ya uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Dk Willibrod Slaa mwaka 2010 eneo la Jangwani Dar es Salaam, baada ya matangazo ya shirika hilo kukatika ghafla.

Matukio kama hayo yanaonekana kuzidi na hadi kufikia chaguzi zijazo huenda waandishi hawa wakashindwa kufanya kazi katika vyombo hivi vya umma vinavyotumia kodi ya Watanzania.
 

Kukatika ama kukatishwa kwa matangazo kumekuwa mwiba kwa waandishi wa habari kwa kuwa watazamaji na wananchi wanahisi kuwa waandishi ndio wahusika wa matukio haya bila kufahamu kwamba wao hupokea maelekezo kutoka kwa viongozi wao na wahariri. 

Tukio kama hili lilimkumba mwandishi mwingine wa TBC mwezi mei 2013 katika mvutano wa serikali na wananchi wa Mtwara. Baada ya mitambo ya TBC kukatika wakati wananchi hao wakiwa katika maandamano, moja kwa moja wananchi waliamua kumuadhibu mwandishi Kassimu Mikongolo kwa kumchomea nyumba yake na gari kwa kuamini amehusika na kukatika kwa matangazo ya TBC mkoani humo. 

Matukio mengine yamekuwa yakijitokeza Mkoani Arusha. Mfano waandishi wa TBC toka chaguzi ndogo zilizofanyika Mkoani humo wamekuwa wakifukuzwa na kukatazwa kuhudhuria mikutano ya siasa hasa mikutano ya CHADEMA. 

Hali imewafanya waandhishi wa vyombo vya umma kuwatumia waandishi wa vyombo vingine kuwachukilia taarifa katika mikutano ya kisiasa. Waandishi waliojikuta katika wakati Mgumu kufanya kazi zao ni pamoja na Leornard Manga, Sechela Kongola na Khalifan Mshana na Ben Mwaipaja. Kwa upande wa Kigoma, waandishi wa vyombo vya umma wanadai kuwa wanafanya kazi vizuri na viongozi wa vyama vyote vya upinzani, isipokuwa wananchi ndiwo bado hawana imani na utoaji wa taarifa katika vyombo vya umma. 

Dotto Elias TBC Kigoma aliwahi kujikuta katika wakati mgumu katika mkutano wa CHADEMA kutokana na wananchi kutaka kumdhuru, kilichomsadia ni viongozi wa CHADEMA kuongea na wanachama wao wasifanye lolote na wamruhusu aendelee na mikutano. 


Katika Mkoa wa Ruvuma, Mwandishi Gervas Msigwa wa TBC mara nyingi amejikuta akipata wakati mgumu kuhudhuria mikutano ya siasa hasa ya CHADEMA, mfano uchaguzi mdogo kata Lisabon Songea Mjini 2011 Msigwa alipigwa na kukimbia. 


Mkoani Iringa mwandishi wa magazeti ya umma Habari Leo na Daily News Frank Leonard , alipigwa na walinzi wa CCM (Green Guard) kutokana na misimamo yake ya kuandika ukweli katika chaguzi za ndani za CCM mwaka 2010. 


Tukio hili linadhirisha kuwa viongozi wa chama tawala wakati mwingine hulazimisha waandishi wa vyombo vya umma kuandika kile wanachokitaka na wasipofanya hivyo hujikuta katika hali utata kiusalama. Matukio haya kwa waandishi wa umma ni mengi wengine walishashushwa kwenye ndege kwa kuhisiwa kuwa wanaandaa taarifa zisizotakiwa na chama fulani. 


Waandishi wa habari wa TBC, wakati mwingine wamelazimika kutoa nembo za TBC kwenye magari yao au kamera zao ili kunusuru maisha yao. Mfano katika hatua ya kufuatilia kesi zinawahusu Shekh Issa Ponda na Alfred Rwakatare wa CHADEMA waandishi George Kasembe na Nora Uledi walijikuta wakitaka kunyang’wa kamera zao na kuzomewa na wafuasi wa watuhumiwa hawa. Chanzo cha Mitafaruku Hii

 
• Katika uchunguzi wetu tumebaini kwamba tatizo inawezekana lisiwe katika ngazi ya chini yaani wanahabari ambao wameaajiriwa katika vyombo vya umma kwa sababu wao wanalazimika kufuata sera za vyombo vyao au maelekezo wanayopewa na viongozi wao kazini. Historia inaonyesha kwamba wanahabari wakati mwingine wanajikuta wakiwa njia panda na kushindwa kufahamu wasimamie wapi mara wanaposhitukizwa katika mivutano kati ya serikali kwa upande mmoja na wanajamii yaani wananchi kwa ujumla kwa upande mwingine.

• Changamoto nyingine ni pale baadhi ya watendaji serikalini kama vile wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi wa maendeleo katika ngazi hizo za wilaya na mikoa wanapoamua kuwatumia waandishi wa vyombo vya umma na hata magazeti yanayomilikiwa na umma kwa manufaa yao binafsi au ya kiserikali/chama tawala. Watendaji hao huona kwamba wanahabari wa TBC na vyombo vingine vya umma ni maafisa habari wao. Jambo hilo hufanyika kwa njia ya ushawishi wa aina mbali mbali ikiwamo malipo ya ziada, kupewa ofisi ndani ya ofisi za wakuu wa mikoa au wilaya, lakini wakati mwingine hata kwa kuwalazimisha kuripoti kile ambacho watendaji hao wanakitaka.
 

• Kwa upande mwingine ipo changamoto, kwani baadhi ya taasisi wakati mwingine hazitaki kuwashirikisha wanahabari kutoka katika vyombo vya umma kwa madai kwamba hawatarajii vyombo hivyo vitaripoti taarifa yoyote ile inayokosoa serikali na yenye maslahi kwa umma. Hii inamaanisha kwamba, baadhi ya wananchi, vyama vya siasa na taasisi binafsi au hata za umma zimekosa imani na vyombo vya habari vya umma.
 

Kutokana na mazingira haya waandishi wa vyombo vya umma hufanya kazi kwa mashaka mashaka kwa kutofahamu hatma yao iwapo wataripoti kinyume na matarajio ya mashabiki wa kisiasa katika maeneo hayo au kinyume cha matarajio ya wananchi. 
 
Hivi karibuni Mtandao huu ulifanya mazungumzo na TBC ambapo ilikiri kuhusu taarifa za baadhi ya vitisho kwa waandishi wao, na mfano halisi ukawa ni suala la Kassimu Mikongolo. Viongozi wa TBC walisema wanaongoza chombo kutokana na sera na kanuni zao za kazi, hivyo walikanusha uvumi kwamba TBC ni chombo chenye kuelemea upande mmoja kwa maana ya kwamba kimelalia upande wa serikal na chama tawala, walilisitiza kwamba hicho ni chombo cha umma na kina ripoti kwa usawa na pia kutii mamlaka iliyopo. Nini Kifanyike
 

• Kuhusu suala la usalama wa waandishi, TBC huwa wanatoa mafunzo mara chache hasa mara Uchaguzi Mkuu unapokaribia, lakini imeonekana kuna umuhimu wa Mtandao kuanzisha ubia na TBC na kuwatembelea wanahabari wake kwa ajili ya mafunzo ya usalama hasa katika mikutano ya kisiasa na maeneo yenye mivutano kati ya serikali na raia.

• Ipo haja ya kuboresha miongozo ya vyombo vya umma ili kuendana na nyakati hizi za vyama vingi na kupunguza maamuzi binafsi ya baadhi ya watendaji.

• Kuna haja pia ya kuwa na mkutano wa pamoja kati ya vyombo vya umma, vyama vya siasa na Mtandao ili kujadili usalama wa waandishi hawa katika chaguzi zijazo.

• Mtandao unawasihi watanzania wote na vyama vya siasa kuacha kuwadhalilisha waandishi hawa wa vyombo vya umma wanapokuwa katika maeneo au mikutano yao na kuchukua hatua dhidi ya menejimenti pale wanapohisi kwamba wamekosewa.

• Tunawashauri waandishi wote wa vyombo vya umma na menejiment zao kuwa vyombo vya umma ni mali ya umma hivyo wanapaswa wakati wote kuwatumikia watanzania na si serikali wala chama chochote.

• Tunashauri pia vyombo vya umma vipewe rasilimali ya kujenga ofisi zao nje ya majengo ya viongozi wa kiserikali. Kufanya hivyo kutarudisha imani kwa wananchi na kuondoa dhana iliyojengeka kuwa wao wamekuwa ni maafisa habari wa viongozi wa serikali.

• Tunawashukuru TBC kwa kumsaidia Kassim Mikongolo kutoka katika eneo ambalo lilikuwa hatari kwake kimaisha na Mtandao unaunga mkono hatua hiyo kwa kumsaidia Mikongolo kurudisha baadhi ya gharama wakati akiendelea kusaidiwa na TBC ili kupata fidia ya nyumba yake.

• Tunawasihi viongozi wa siasa kutoa elimu ya haki za mwandishi kwa wanachama wao na kuimarisha ulinzi na usalama wa waandishi wanapokuwa katika mikutano yao.

• Tunawasihi sana viongozi wa serikali na wanasiasa wote hasa wa chama tawala, waache tabia ya kuwagawa waandishi wa habari kwa matabaka kwa malengo ya kutaka kuwapata waandishi wa habari amabao wataandika kile wanachokitaka kiandikwe na sio kuandika ukweli na hali halisi. Tabia hii imewafanya waandishi wawe njia panda na kujikuta wakiwatumikia viongozi na wanasiasa kama maafisa habari wao na kujiweka katika mazingira magumu ya kiusalama.
 
Imeletwa kwenu kwa niaba ya Mtandao na: Onesmo Olengurumwa Mratibu Taifa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRD-Coalition).  Onesmo Olengurumwa  MRATIBU MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU

"ACHENI TUIMARISHE CHAMA CHETU,MANENO MANENO YA NINI?-MWAKASAKA

 
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka akipeana mkono na mmoja wa Chipukizi kata ya Ntalikwa manispaa ya Tabora baada ya kumkabidhi Kadi ya uanachama  wapya wa Chipukizi Tabora,wakati wa ziara rasmi ya kukijenga CCM kupitia jumuiya ya UVCCM Wilaya ya Tabora mjini. 
Mmoja kati ya viongozi wa UVCCM Wilaya ya Tabora mjini Bi.Rosemary Cloud akionesha furaha yake katika ziara hiyo ya UVCCM kata ya Ntalikwa ambayo imeonesha mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi wa wanachama wa CCM kupitia jumuiya hiyo ya Vijana.
Katika ziara hii Mjumbe wa kamati kuu ya CCM wilaya ya Tabora Bw.Mwakasaka mbali ya kukabidhi Jezi za mpira wa miguu,alikabidhi pia fedha zaidi ya shilingi Mil.moja kusaidia shughuli za miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo ya Ntalikwa.
 Na Mwandishi wetu Tabora.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka amewataka wanachama wa CCM wakiwemo viongozi kuelekeza nguvu zao katika kukijenga chama hicho badala ya kuendekeza majungu na manung'uniko yasiyo na msingi.

Bw.Mwakasaka ameyasema hayo katika kata ya Ntalikwa manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kukiimarisha CCM iliyoandaliwa na Jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Tabora.

Katika ziara hiyo Mwakasaka alifikia kutoa tamko hilo baada ya kuwepo kwa baadhi ya kauli za wanaccm kutafsiri vibaya malengo ya  ziara hizo ambazo zinafanyika mara kwa mara wakidai kuwa ni kampeni za maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

"Jamani acheni tukijenge chama,...tusingoje wakati wa uchaguzi tu ndio tuanze kuwa karibu na wananchi hii sio nzuri kwetu,...na mnaoona kuwa ni kampeni jueni kuwa tunapoteza muda wenzetu wa vyama vya upinzani wanafanya sana mikutano karibu kila siku"alisema Mwakasaka.

Sambamba na hilo Bw.Mwakasaka alisisitiza kuwa ni vema tukaendelea kukijenga chama chetu hatua ambayo itatusaidia kukabiliana na vyama vya upinzani kwa sisi kupata ushindi mkubwa wakati wa uchaguzi utakapowadia.

Aidha CCM kupitia Jumuiya ya UVCCM wilaya ya Tabora hivi sasa kimekuwa kikifanya mikutano ya mara kwa mara hatua ambayo inadaiwa kuwa inazidi kukiimarisha Chama hicho na kurejesha imani kwa wananchi wilaya ya Tabora.  

"NGOMA YA MIZIMU YA JADI YA WABISA IPO HATARINI KUPOTEA TABORA?

 

WABISA


Na Mwandishi wetu Tabora.
 
ZAMANI  wakati nikiwa mdogo nilikuwa nikiambiwa kuwa Wabisa wakati mwingine usiku huwa wanageuka Simba,Jambo hili lilikuwa likinihofisha sana hata kufikia hatua ya kuwaogopa kabisa watu hao ambao kutokana na utamaduni wao hupandisha mizimu wakati wakitekeleza Mira zao hizo za Jadi.

Ingawa nilikuwa nikishuhudia wakifanya shughuli zao katika matukio mbalimbali kama  Matambiko,Harusi na tiba mbalimbali za Jadi,lakini hilo halikuondoa dhana ya mimi kuendelea kuwaogopa kwani watu waliokuwa wakinihadithia kuwa hiyo ni mizimu ambayo hujigeuza kuwa simba walikuwa ni watu wazima na wenye akili zao timamu.

Lakini haikujalisha kwa wale waliokuwa wakithibitisha kuwa mizimu hiyo husaidia kwa kutoa tiba za Jadi kwa kutumia mitishamba na hata kufanya hayo matambiko kwa kupiga na kucheza ngoma kwa zaidi ya mwezi mzima usiku na mchana kwa maana kwamba Mbisa akipandisha mizimu yake huchukua zaidi ya siku 30 bado anakuwa yupo katika hali hiyo pekee huku akiongea Lugha ambayo wanayoielewa wao wenye kushiriki Utamaduni huo wa Wabisa.

Kwa siku za hivi karibuni ngoma hii ya mizimu ya Jadi ya Wabisa  imeanza kuonekana kwa nadra sana ukilinganisha na miaka ya 1985 kurudi nyuma,kwani mbali ya kukutana na mtu ambaye amepandisha hiyo mizimu ya Wabisa,hata  kabla hujamuona lakini unaweza kusikia sauti ya kengele za miguuni ambazo huambatana na vazi rasmi lenye rangi nyekundu lililonakshiwa na rangi nyeusi na nyeupe huku machoni akiwa amejipaka rangi nyeupe kuzunguuka ukingo wa jicho hali inayofanya macho yao kuonekana mekundu kupindukia.

Kama ikiwa ndio mara yako ya  kwanza kukutana nao halafu hujawahi kuwaona wala kusikia habari zao unaweza kukimbia kwakuwa huwa hawasalimii mtu wasiyemjua na mara nyingi wawapo barabarani katika safari zao hutembea mstari mmoja kwa kiongozi mmoja kuwepo mbele na mwingine nyuma kabisa na hakuna kitu kinachosikika zaidi ya kengele za miguuni.

Ni wazi kwamba unaweza kuamini kuwa ni mizimu maana hata kama kuna mtu anafahamiana na mtu huyo aliyepandisha mizimu huwa hawezi kuongea naye zaidi ya kutizama kwa macho makali kabisa mithiri ya mtu anayekusudia kufanya kitu kibaya na cha hatari.

Pamoja na hayo yote lakini Jadi hii ya Wabisa ilikuwa ni sehemu ya utambulisho wa watu hao na kwakweli walikuwa wanapendeza sana hasa wakati ukiwakuta wanafanya mira zao ambazo kwa maana moja ama nyingine zilikuwa zikionesha ustaarabu walionao pamoja na maadili ya kudumu.

Sasa hapa nakusudia kuangalia namna gani hii asili ya utamaduni wa Wabisa inavyoenndelea kutoweka kwa kile ninachobaini kuwa siku hizi siwaoni hata wakiitwa kufanya burudani kwenye harusi au sherehe nyingine yeyote iwe ni ya serikali au vinginevyo.

Lakini pia zamani tulikuwa tukishuhudia hata matambiko yakifanyika mara kwa mara katika kaya mbalimbali na Wabisa wanakuwa ndio wahusika wakuu jambo ambalo sasa halipatikani kabisa sijui ni kwa hii hatua ya kuzagaa kwa utandawazi na pengine watu kujiona kuwa wamestaarabika na hivyo hawaoni umuhimu wa matambiko hayo.

Sikusudii kuhamasisha watu warudie matambiko ambayo kwasasa wameyatelekeza,lakini dhamira yangu ni kutaka kujua nini kimebadirika na hata kufikia hatua ya kuona masuala haya ya Jadi hayana nafasi tena kwetu?

Mtu mmoja ambaye umri wake umekwenda kiasi nilipokuwa nikimuuliza kuhusu jambo hili alinijibu kwamba kila JAMBO NA WAKATI WAKE,wewe jaribu kuangalia tu hata maadili kwa watu yakoje kwasasa,...kisha uangalie matukio mbalimbali yanayojitokeza,...Yaliyo ya maana hayapewi nafasi kwa umuhimu wake na yasiyo ya maana yanakumbatiwa,hii ni dalili tosha kuwa WAKATI UKUTA.

Hapa tena mimi sikuwa na namna ya kuendelea kuuliza  ila ninachosikitikia ni kupotea kwa Mira na Desturi ambazo kumbe ndio chimbuko la Maadili kwa baadhi ya Mira na Desturi hizo.

        

Monday, September 16, 2013

VIONGOZI HAWAPIGI KELELE WAKULIMA KUIBIWA!!!-SAID NKUMBA



 

Na Hastin Liumba,Sikonge.

MBUNGE wa jimbo la Sikonge mkoani Tabora,Said Nkumba anasikitishwa na kusononeka kutokana na baadhi ya viongozi wenzake kukaa kimya na kushindwa kupiga kelele wakulima wa nchi hii wanavyoibiwa.

Nkumba alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kupokewa kwa maandamano na wananchi wa jimbo lake siku chache zilizopita,maandamano yaliyoanzia kata ya Pangale hadi Sikonge mjini hadi nyumbani kwake.

Alisema kutokana na kauli yake bungeni ya kutaka mswada wa sheria za ushirika usainiwe na rais  Dkt Jakaya Kikwete,na kutaka Apex ifutwe kutokana na kukosa msaada, uzalendo wa kweli kwa wakulima nchini hususani wa zao la tumbaku ndicho kiini cha wananchi wa jimbo lake kumlaki kwa maandamano.

Alisema umefika wakati sasa kwa viongozi wenye dhamana kujipanga upya ili kuweza kusaidia wakulima wa nchi hii ili wasibaki kama yatima kwenye haki zao za msingi kwani taarifa za sasa zinaonyesha wakulima wengi hawajitambui katika uwezo wao wa kuendesha ushirika.

“Wanaushirika wote ndiyo wenye nguzo za kuendesha ushirika na ifikie mahali viongozi wote wasio waaminifu na wezi kuondolewa mara moja na hii ni njia mbadala ya kumkomboa mkulima kwani kupewa madaraka isiwe sehemu ya kujitajirisha.”alisema Nkumba.

Alisema mkulima angefikia mahali pazuri endapo kungekuwa na maamuzi ya kuwajibishana na itakuwa haina maana kuwa na vyombo vya ushirika vinavyoendelea kukaa kimya wakati wizi,dhuluma dhidi ya wakulima inaendelea.

Nkumba alisema ana imani kubwa kwa rais Dkt Jakaya Kikwete atausaini mswada ule…..na hiyo itakuwa ni ishara tosha sasa mkulima wa nchi hii anakombolewa cha msingi tu kuwepo na utekelezaji wa maamuzi waliyopewa baadhi ya viongozi.

Hata hivyo siku chache baada ya mswada huo kupitishwa na kutaka kufutwa kwa Apex wameibuka baadhi ya viongozi wanaolalamika na kuitisha vyombo vya habari kutaka rais Dkt Jakaya Kikwete kutosaini mswada huo.

“Haya yanayolalamikiwa na wale wanaotaka rais asisaini ule mswada inaonyesha kuna maslahi yao hapa kwa hawa wanaojiita wanaushirika……napata mashaka sana na hawa watu na hapa jamii inawaona hawajui mbona hawalalamiki mkulima kubeba mzigo mzito kwa muda mrefu lakini hawakuitisha vyombo vya habari kulalama.”alisema.

Alisema kamwe hataacha kupiga kelele kumsaidia mkulima hasa wa zao la tumbaku na sasa moto kauwasha hatauzima na hakuna atayemziba mdomo.

Mbunge huyo anasema anawashukuru wakulima na wananchi kwa ujumla kwani toka ametoka bungeni amekuwa akipokea simu nyingi za pongezi toka wananchi wa baadhi ya mikoa na kumtaka aendelee na mapambano katika kumkomboa mkulima wa nchi hii.

Alisema wao kama wabunge hawana mipaka ya kutetea wananchi zaidi ni kutetea makundi yote ya jamii hivyo mtu mwenye kuona kuna mipaka basi huyo ni sehemu ya wale wanaotaka mkulima aendelee kubeba mzigo mzito hasa wa madeni makubwa na wizi.



!!LOWASSA AINGIA NGOME YA SITTA,WANANCHI WAMKUBALI KUWA MTETEZI WA WANYONGE!!


Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli Bw.Edward Lowassa akikabidhiwa mkuki kama ishara ya kukabidhiwa majukumu ya kuwa mlezi wa Machifu Tanzania,Kulia ni Mtemi ya Unyanyembe Chifu Msagatti Ngulyati Said Fundikira wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mtemi Isike MwanaKiyungi yaliyofanyika Itetemia  katika ukoo ambao Waziri wa Afrika Mashariki Bw.Samwel Sitta ni ndugu wa karibu.
Mtemi Msagatti akimkabidhi Cheti Bw.Lowassa kama hatua ya kumtunuku kuwa Kiongozi bora anayejali maisha ya wanyonge ambao kimsingi ni watanzania wenzake na kuwa sasa ni Mlezi kamili wa Machifu wa Tanzania.
Bw.Lowassa pamoja na kupokelewa kama Mfalme lakini pia ngoma za Dola ya Wanyanyembe ambazo zilikuwa zikitumbuiza katika Maadhimisho hayo.
  Bw.Lowassa akijaribu kushika Kibuyu cha matambiko kwa kinadada walikuwa wakimuimbia nyimbo za Kinyamwezi
Bw.Lowassa aliweka jiwe la msingi mahali ambako panatakiwa kujengwa mnara wa Ngome ya Mtemi Isike MwanaKiyungi Itetemia Tabora mjini.
.