Sunday, June 30, 2013

DIAMOND ALIVYOWAPAGAWISHA WANYAMWEZI PALE ALLY HASSAN MWINYI

Rommy J akiwagongeshea miutamu
Ni shangwe kila kikitoka kitu kinaingia kitu
full mang'ang'aaaaaa! Shangweeeeee
Nyomi hii ilihappen maeneo ya uwanja wa Ally Hassan Mwinyi-Tabora
ikiwa ni sho ya pili toka ipigwe ile ya usiku wa 28-06-2013 ndani ya ukumbi maarufu kwa jina la Frankman Palace na ilikuwa PALACE kweli 

MKUTANO WA KWANZA WA CG FM RADIO UKIJADILI UZALISHAJI WA VIPINDI VIPYA VYA KIJAMII


Mkutano wa kwanza wa wadau wa CG FM Radio unaendelea katika ukumbi wa Kalindimya -Moravian hostel Tabora ukiwa na lengo la kujadili juu ya uanzishwaji wa vipindi vipya vya kijamii vya Nufaika na Fumbuka.Vipindi hivi vya kijamii vinatarajiwa kuanza kurushwa hivi karibuni kupitia CG FM Radio.Mkutano umehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia,vyama vya ushirika na makampuni mbalimbali

MKURUGENZI WA 89.5 CG FM RADIO BW.CHARSE GEORGE
MENEJA WA 89.5 CG FM RADIOBW. TITUS PHILIPOSAMADA MADUHU | MSHAURI WA VIPINDI KATIKA KITUO CHA MATANGAZO CHA 89.5 CG FM RADIO CHA MKOANI TABORA AKITO MAWASILISHOYAKEYALIYOTOA MWONGOZO WA NINI KIMEWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI MKOANI HAPO TABORA
WADAU WAALIKWAWADAU WAALIKWA
wazee wa mitambo

Meneja wa mamlaka ya haliya hewa Tabora na Mpanda
 Wadau wakisikiliza kwa umakini
 Meneja wa mamlaka ya hali ya hewa akitumia mchoro kuelezea hoja
 Ibrahim Haruna-Mtangazaji na muandaaji wa kipindi cha FUMBUKA | Akikitambulisha kipindi hicho kipya.
(PICHA NA Aloy-Son-Blog)
-------------------------------
CG FM RADIO IMEKWISHA ONESHA KIPINDI KIPYA CHA NUFAIKA KITAKACHOLENGA KUJIHUSISHA NA MAMBO YA WAKULIMA KWA KUWAPA ELIMU, UTOAJI TAARIFA ZA HALI ZA HEWA, KUSHIRIKISHA WATAALAMU NA WADAU WAKIWEMO WAKULIMA WENYEWE KUJADILI MAMBO YAHUSUYO KILIMO KWA MANUFAA, TAARIFA ZAAIDI ZITATOLEWA KUHUSU BEI NA MASOKO, TAARIFA ZA TAFITI ZA KILIMO.
-----------------------------------------------------------------
MAWASILISHO YA WADAU
====================================
MKUU WA CHUO CHA KILIMO CHA TUMBI
  • Aina mpya ya mpunga iitwayo AMKA/NERICA- Mradi wa Wajapani
  • Kilimo SHADIDI (Mazao maradufu
MRATIBU WA KILIMO MIRADI VIIJIJI VYA MILENIA-MBOLA
  • Kanuni bora za kilimo
  • Matumizi sahihi ya mbolea
  • Ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi ya kilimo
  • Mikopo naafuu kwa mkulima
  • Usisitizaji wa mbegu stahimilifu za maeneo ya Tabora.
MENEJA WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TABORA NA MPANDA.
  • Upimwaji wa hali ya hewa na uwasilishaji wake kwa jamii kupitia vyombo vya habari
  • Matumizi ya hali ya hewa kwenye kilimo, usafirishaji, maji, nguvu za uzalishaji, utalii.
  • Utoaji wa taarifa za hali za hewa kwa misimu (siku 10 na kuendelea) 
  • Umuhimu wa hali ya hewa kwa kilimo (utambuzi wa udongo n.k)
  • Madhara ya hali ya hewa- ukame, migogoro ya wafugaji na wakulima, ugomvi wa maji, mafuriko,n.k
MUWAKILISHI WA CHUO CHA ARDHI
  • Umuhimu wa sheria za usimamizi na matumizi bora ya aridhi
  • Kujua taratibu za kisheria ya aridhi zilivyo na mamlaka zake
  • Mpango wa matumizi bora ya aridhi na faida zake.
  • Hati za haki miliki za aridhikama zakimila na nyinginezo.
MUWAKILISHI CHUO CHA NYUKI-TABORA
  • Umuhimu wa nyuki kiuchumi na kibaolojia.
  • Teknolojia ya ufugaji nyuki na tafiti.
  • Ubora wa asali na mabadiliko ya mbinu zaufugaji nyuki kupitia teknonojia.
  • Mbinu bora za kisasa katika uvunaji asali (Teknolojia Mwafaka).
  • Zana na aina zake za uvunaji asali (Gun-boot, Kofia,groves n.k)
  • Faida za ufugaji nyuk
  • Umuhimu wa mimea kwa nyuki

MAWASILISHO YA WADAU YALIKUWA YAKILENGA UPATIKANAJI WA NAMNA UBORESHWAJI WA VIPINDI VIPYA VIMLENGAVYO HASA MKULIMA WOTE NA WAFUGAJI KWA KUTOA MWANGA NA MWELEKEO HATA PIA KATIKA KUSHIRIKIANA KUIKOMBOA JAMII YA WANATABORA KWA WAO KUUONA UMUHIMU WA KITUO CHA RADIO KWA MANUFAA YAO.

TFDA YATEKETEZA ZAIDI YA TANI 2 ZA VIPODOZI TABORA

 

Mkaguzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa TFDA kanda ya Kati na Magharbi Bw.Aberl Deule akifumua baadhi ya vipodozi kwa ajili ya matayarisho ya kuteketeza kwa moto zoezi linaloendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Tabora.    
 
 NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
 
MAMLAKA ya chakula na dawa nchini (TFDA), kanda ya magharibi na kati,imeteketeza bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu, zenye thamani ya sh milioni 3.2.
Zoezi la kuteketeza bidhaa hizo lilifanyika mkoani Tabora baada ya kufanyika ukaguzi maalumu kwa wiki mbili kwenye maduka,majengo,Phamacy bohari ya dawa na maeneo mengine muhimu.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la kuteketeza bidhaa hizo,mkaguzi kanda ya kati na magharibi,Abel Deule,alisema ukaguzi huo ulihusisha watalaam toka ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Tabora na halmashauri ya manispaa Tabora na ukaguzi huo ulihusisha biashara ya chakula,dawa,vipodozi na vifaa tiba.
Deule aliongeza jumla ya majengo 192 yalikaguliwa na ambapo lengo lake ni kuangalia majengo hayo,usafi,hali ya usajili na vibali toka mamlaka ya chakula na dawa,(TFDA),hali ya ubora wa bidhaa za chakula,dawa,vipodozi, vifaa tibauwepo vifaa bandia zenye viwango duni na uwepo vipodozi vyenye viambata vyenye sumu.
Aidha Deule alisisitiza kutokana na ukaguzi huo,licha wafanyabiashara hao kuwa na uelewa,bado wamekuwa wakiuza vipodozi vyenye viambata vyenye sumu vilivyozuiliwa kuuzwa na ktumika nchini kwa mujibu wa kifungu namba 88 (a) cha sheria ya chakula, dawa na vipodozi namba 1 ya mwaka 2003.
Alisema bidhaa zilizokamatwa na kuteketezwa ni bidhaa za chakula tani 0.129 ya thamani ya sh 775,000,bidhaa za vipodozi zilizoisha muda wa matumizi na zenye viambato vyenye sumu tani 0.245 vya thamani y ash sh milioni 2,298,400 na dawa za binadamu tani 0.001 zenye thamani ya sh 158,000.
Aidha aliongeza kwenye ukaguzi huo pia kulikutwa maziwa ya watoto ,Lactogen namba 1 na 2 na NAN ambayo ni bandia, dawa ya chanjo ya mifugo ya Newcastle (1-2) iliyositishwa kuuzwa,dawa bandia aina ya Doxycycline Capsules gramu 100,pombe kali iitwayo Shujaa gin ambayo haijapata usajili toka mamlaka ya chakula na dawa.
“Kutokana na hali hiyo tumechukua hatua za maduka yaliyokutwa na vipodozi vyenye viambata vya sumu….. wamiliki walilipa ada ya vibalivya kuteketeza,wateja ambao majengo ambayo hayajapata usajiliwalijaza fomu na kulipia ada kwa vibali husika ikiwemo duka moja kufungwa kutokana na mmiliki kuwa mkaidi kwa maafisa.” alisema Deule.
Aliongeza hata hivyo wakati wa ukaguzi wafanyabiashara walielimishwa kuhusu bidhaaza vyakula,dawa.vipodozi,ikijumuishwa bidhaa za vipodozi zenye viambato vyenye sumu,na bidhaa duni na bandia ya chakula (Lactogen 1/2 na NAN 1/2.

DIAMOND AFANYA SHOW YA BEI KUBWA TABORA WENGI WASHINDWA KUHUDHURIA

 


 Msanii maarufu nchini Diamond hapa akiwa katika Show yake iliyofanyika ukumbi wa Frankman Hotel mjini Tabora.
 Mapenzi sasa basi yana-run sana
 Diamond wakati akiamua kucheza na kuonesha namna anavyoweza kujiachia katika Jukwaa la ukumbi wa Frankman Hotel.

 Hii ilikuwa lazima kwa wapenzi wa muziki wa BongoFleva kuchukua picha za msanii nguli Diamond kwa kutumia camera za simu.
 
 Kazi na dawa
 Tabora piga keleleeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.........!
 Wadau mbalimbali wa TABORALEOHABARI .COM nao walihudhuria katika show hiyo ya watu wa heshima kwa viwango vya juu vya kiingilio.
 wadau hao waliotokelezea kisafi zaidi
Haikuwa vibaya kwa wadau hawa kushindwa kuzuia hisia zao kama ilivyoonekana kwa Mwanadada huyu ambaye alilazimika kujiachia pasipo kutarajia ndani ya Show hiyo ya heshima.
 "YES ni SISI"
 six pillars wakicheza
Six Pillars | Tabora Dancers wakibadilishana mawazo na Dancer wa Platinum

Friday, June 21, 2013

HAUSIGELI ATAKA KUJIRUSHA GHOROFANI ..ANGALIA PICHA

 

HAUSIGELI ambaye jina lake halikupatikana mara moja, nusura ajirushe chini kutoka ghorofa ya pili kwa kile kilichodaiwa kuwa aliogopa moto mkubwa uliozuka katika jengo la jirani na ghorofa alilokuwemo.

Tukio hilo lilijiri mapema asubuhi ya Juni 18, mwaka huu kwenye makutano ya Mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa majirani, baada ya kuona moto huo ulioambatana na wingu zito la moshi ukitoka kwenye jengo la jirani, hausigeli huyo alitoka dirishani na kutaka kujirusha chini bila kujali nguo zilizokuwa zikimvuka katika purukushani hiyo.


Alifanikiwa kukaa kwenye sehemu ya ukingo wa ghorofa hilo na kujiandaa kwa tukio la kwenda chini akiamini atakuwa amejiokoa na moto huo.


Hata hivyo, bosi wa hausigeli huyo alipoona zoezi hilo la hatari alitoa mkono dirishani na kumvutia ndani mfanyakazi wake huyo tukio ambalo lilijiri muda mfupi kabla ya Kikosi cha Zima Moto kufika na kufanikiwa kuuzima bila kujeruhi mtu.


Source:GPL

HATARIIII.....ANGALIA PICHA ZA MAJERUHI MAPOKEZI YA BECKHAM CHINA


Beckham stampedeVurugu tupu: Ofisa wa usalama na watu wengine wakijaribu kumbeba askari wa kike aliyepata majeruhi katika mapokezi hayo yaliyojaza nyomi kubwa sana
David BeckhamKabla ya fujo: Maelfu ya watu wamejitokeza kumpokea nyoa Beckham katika chuo kikuu cha Shanghai
PolicewomanMaskini askari: Askari wa kiume akiwa amelala chini ya sakafu baada ya kujeruhiwa katika mapokezi hayo
Beckham crushFujo zaanza:  Maofisa wa polisi wameshindwa kuwazuia maelfu ya watu katika mapokezi hayoNa Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Nyota wa zamani wa Manchester United,  Los Angel Galaxy, Real Madrid, PSG na timu ya taifa ya England, David Beckham amewasili leo nchini China na kusababisha wanafunzi watano kujeruhiwa vibaya katika harakati za kumpokea  katika chuo cha Tongji University ambapo umati mkubwa ulifurika kupita kawaida.
Beckham ameenda kuwatembelea wanachama wa klabu ya mpira wa miguu ya chuo hicho kama sehemu ya ziara yake ya siku saba nchini humo yenye lengo la kuiamusha ligi kuu ya China.
Licha ya watu wengi waliofurika kuhitaji kushikana mikono na nyota huyo, imekuwa ngumu sana kulingana na watu kusukumana na kusababisha watu kujeruhiwa wakiwemo maaskari polisi.
Lengo la Beckham kuzungumza na wanachama hao limeshindwa kutimia kufuaia fujo hizo za watu wengi waliofurika, lakini ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Facebook akiwaomba radhi mashabiki wake kwa kile kilichotokea.
Samahani sana jamani, nimeshindwa kuiona timu ya chuo kikuu pale uwanjani, kiukweli ilikuwa ngumu sana kupenya umati ule. Nimesikia watu wachache wamejeruhiwa, natumaini wanaendelea vizuri na nawatakiwa kheri wapone salama”. Alisema Beckham baada ya kuondoka uwanjani hapo.
Takribani watu elfu moja walikuwepo katika mapokezi hayo na kuhitaji kumshika nyota huyo,na tayari jeshi la polisi limethibitisha kuwa maofisa wake watu wamejeruhiwa katika fujo zoezi hilo.
Beckham mwenye umri wa miaka 38 amestaafu kucheza soka msimu uliopita ambapo aliwasaidia PSG kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa, Ligue 1.

MWANAFUNZI APIGWA RISASI TUMBONI CHUO KIKUU CHA UDSM USIKU WA KUAMKIA LEO


Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.

Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha,  na majambazi kuanza safari yao.

Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.

Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi. Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka, ingawa FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia suala hilo ili kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.

Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar es salaam na kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya kikatili chuoni hapo. Endelea kufuatilia katika mtandao huu amboa umefunga safari ya kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia nini kinaendelea.

Mbali na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi wa hadharani katika shule za Chuo hicho ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa wakiporwa komputa zao mchana kweupe maeneo ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasilinao ya Umma (SJMC).

Suala hizi limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.

SAKATA ZIMA LA KUPIGWA KWA MBUNGE WA KASULU ( MOSES MACHALI) AKIWA DODOMA JANA JIONI


Habari kutoka Dodoma zinasema Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. Moses Machali (pichani), amelazwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma kuuguza majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jana  jioni  mjini Dodoma.

Tukio hilo lilitokea jana jioni  wakati Mh. Machalli akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita ....

Kitendo hicho  kilionekana kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni ....

Baada ya kushuka,  vijana hao walimtolea  matusi kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa hasira ndipo kipigo kikali kilipoanza.

Shuhuda  aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema  Mh. Machalli alipigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.

Mhe Mbatia amesema leo mjini Dodoma kwamba amemtembelea Mhe. Machali asubuhi hii na kumkuta anaendelea vyema na matibabu.

Thursday, June 20, 2013

MWANAMKE ANA NAFASI KUBWA YA KUCHANGIA MAENDELEO


 NA LUCAS RAPHAEL,TABORA


IMEELEZWA KUWA Suala la kijinsia halina budi kupokelewa ili kumpa nafasi mwanamke yakuweza kuchangia maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla .

Kauli hiyo ilitolewa na mmoja ya wakazi wa kijiji cha Kigwa AZIZA RAMADHANI wakati akichangia mdahalo wa Mwanaume na mwanamke.

Kauli hiyo, waliitoa jana kijijini hapo kwenye mdahalo  wa usawa wa kijinsia na maendeleo, ulioandaliwa na Shirika la mtandao wa mandeleo ya jamii wilayani Uyui (UCODEN) kwa ufadhiri wa The Foundation for Civil Society kutoka Dar es Slaam.

Alisema kwamba mwanaume na wananmke washauriane katika shughuli mbalimbali ili kujiletea maendeleo.

“Mwanaume asijione kuwa yeye ndiyo binadamu na mwanamke ni mashine ya kufanya kazi katika jamii.alisema AZIZA

Alisema kwamba kila mtu ana sehemu yake katika kuleta maendeleo katika jamii.Tatizo ni kina baba kujiona kuwa wapo juu kuliko mwanamke bila kujali uwezo alio nao mwanamke.

Alisema kuwa baba pekee yake hawezi kuleta maendeleo ni lazima kuwepo na mchango wa mwanamke.


Amina Christopher Mjema:naye alisema kuwa  wazazi wengi wananchangia mtoto wa kike kushindwa kufanya vizuri katika elimu kutokana na tabia ya wazazi kuhamasisha watoto wao wa kike kuolewa badala ya kuhamasisha watoto hao kusoma zaidi.

Hata hivyo Diwani wa kata ya Kigwa Katyavi Salumu alisema kwamba kuna na changamoto nyingi katika masuala ya kijinsia mfano kipigo kwa kina mama limekuwa tatazi kubwa kwa jamii yetu.

Alisema kwamba mgawanyo hafifu wa mali,hii inatokana na kurithi tabia kutoka kwa mababu bila kuangalia athari za mila hizo za mababu.

Aliongeza kusema kwamba pia kina mama wanajirudisha nyuma kutokana na kushindwa kwao kutoa maamuzi ya jambo fulani na badala yake wamekuwa wakiwasubiri waume zao.

Kwa upande wa elimu, diwani huyo alisema watoto wa kike nao wamekuwa wakichangia katika kuwanyima fursa ya elimu kutokana na mabadiliko ya ukuaji ni vema jamii kuangalia kwa makini kuhusu malezi ya vijana.

Hata hivyo Mratibu wa UCODEN Christopher Nyamwanji aliwashukuru sana washiriki kwa maoni yao ambayo yameonesha uzoefu wa masuala ya kijinsia katika kata ya Kigwa na pia aliwasihi wakazi wa Kigwa kujitokeza tena siku nyingine katika shughuli kama hii.

MWISHO

MAJAJI MAHAKIMU WALALAMIKO KANDA YA MAGHARIBI



Na Lucas Raphael,Tabora




JUMLA  ya malalamiko 36 yalipokelewa na ofisi ya  maadili  kanda ya magharibi katika kapindi cha mwanka jana na mwaka huu kwa maafisa wa mahakama kwa kuchelewesha kesi na kupokea rushwa kwa lengo la kupendelea hukumu.

Maelezo hayo yalitolewa na kamishna wa sekretarieti ya maadili ya viongozi jaji mstahafu Salome Kaganda alipokuwa akimkaribisha mkuu wa mkoa wa tabora Fatma Mwassa wakati wa  kufungua mafunzo kwa mahakimu katika ukumbi wa mtemi Isike mwanakiyungi mkoani tabora jana .

Alisema kwamba katika malalamiko hayo 15 sawa na asilimia 41 .6 ni malalamiko  kwa maafisa wa mahakama ,wakiwepo majaji na mahakimu wa ngazi mbalimbali kwa kuchelewesha kesi na kupokea rushwa .

Jaji Kaganda aliendelea kusema kwamba idara ya mahamaka ni miongoni mwa  Idara za serikali zinazolalamikiwa sana kwa vitendo vya Rushwa ,kutokutenda haki na kukosekana kwa uadilifu.

Alisema kwamba mafunzo hayo lengo lake ni kuwajengea uwezo viongozi wa katika kuifahamu na kuitekeleza sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995 ambayo ndio sheria mama inayosimamia maadili ya viongozi wa umma nchini.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa tabora Fatma Mwassa akifungua mafunzo hayo katika hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Tabora Sulemani Kumchaya alisema kwamba utumishi wa umma kwa ujumla bado una matataizo na mapungufu mengi ya kimaadili ,utoaji wa huduma usioridhisha ,migongano ya maslahi matumizi mbaya ya madaraka hivyo vyote ni changamoto inayowakabilia watumishi walio wengi hapa nchini .

Alisema kwamba mafunzo haya yawe ni chachu ya mabadiliko kwa kada ya mahakimu mkoai hapa kwa kufanya kazi kwa kufuata maadili kanuni sheria na busara .

“hali hiiitakuza matumaini na imani ya wananchi kwa serikali na hususani mhimili wa mahakama kama chombo kikuu cha kusimamia haki kwa umma”alisema mwassa.

Mafunzo hayo yaklioandaliwa na ofisi ya maadili ya viongozi kwa mahakimu kwa wafawidhimkoa na wilaya na wale wa mahakama za mwanzo kutoka katika wilaya saba za mkoa wa  tabora .

Mwisho

MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WATOA TAMKO KAULI YA WAZIRI LUKUVI NA HALI YA USALAMA MKOANI ARUSHA


KAULI YA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KWA WAZIRI WILLIAM LUKUVI NA HALI YA USALAMA MKOANI ARUSHA TAREHE 19 JUNI 2013 

Mtandao wa Wateteziwa Hakiza Binadamu unaounganisha asasi za kiraia zinazotetea haki za binadamu zaidi ya mia moja, pamoja na mashirika wananchama Mkoani Arusha, tumesikitishwa na kushtushwa sana na kauli iliyotolewana Waziriwa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera, Uratibuna Bunge) William Lukuvi dhidi ya asasi zakiraia.
 

Katika kauli yake Bungeni tarehe 17 mwezi Juni, akizungumzia tukio la bomu dhidi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA), Lukuvi ameendeleza kile ambacho kwa muda mrefu serikalii liyopomadarakani imekuwa ikikifanya yaani kutumia lugha mbaya za kuwachonganisha wateteziwa hakizabinadamu na asasiza kiraia kwa ujumla na kuwaita kwamba ni wachochezi, vibaraka wa upinzani na lugha nyingine zenye dhihaka.
 

“Katika siku za karibuni, zimekuwepo jitihada za makusudi za baadhi ya vyama vya siasa, makundi ya kijamii na watu binafsi kupandikiza chuki kwa raia dhidi ya vijana wetu wa Jeshi la Polisi, kuwafanya raia wawachukie askari, kuwafanya raia wasiwaamini askari, kuwafanya raia wasiwape ushirikiano askari na hatimaye kuwa na taifa ambalo halitawaliki,” alisema Lukuvi
 

Kauli kama hii kutolewa kiongozi mkubwa wa serikali tena katika Bunge la Tanzania ni kejeli kwa waliopoteza ndugu zao Mjini Arusha, na ni kauli ya vitisho dhidi ya asasi zisizo za kiserikali nchini. 

Nchi yetu imekumbwa na kasumba ya viongozi kuacha kutatua dalili zinazoashiria upotevu wa amani na kutaka kuonyesha kuwa asasi za kiraia na makundi mengine ndio chanzo cha matatizo hayo. Kauli kama za Mh Lukuvi zimeshatolewa ndani ya miezi sita iliyopita na mawaziri na viongozi wengine wasiopungua watano. 

Waziri Kagasheki alizishutumu wazi wazi asasi za kirahia zinazotetea haki za wafugaji Loliondo kuwa ni wachochezi wa mgogoro huo, wakati huo huo Naibu waziri wa Ardhi aliendeleza shutuma na vitisho hivyo dhidi ya Asasi zinazotetea rasimali ardhi nchini. 

Tunamsihi Lukuvi, atambue kuwa imani ya wananchi dhidi ya jeshi la polisi nchini haijawahi kuondolewa na asasi za kiraia, bali huondolewa na matendo ya kidhalimu ya jeshi hilo dhidi ya wanachi na vyama vyao. Jeshi la polisi litaweza kurudisha imani kwa wananchi endapo tu litaacha kutumika na watawala kwa maslahi binafsi na kisiasa na sio kwa kauli za kubeza zitolewayo na viongozi wa serikali dhidi ya asasi za kiraia na makundi mengine.

 Itakumbukwa kwamba hivi karibuni katika uchaguzi wandani wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. JakayaKikwete, aliwatahadhrisha wana –CCM wasiendelee kulitegemea Jeshi la Polisi kamanguzo yake kisiasa.

 Viongozi waache mzaha katika hali ya usalama wa Taifa kwa sasa kwani hakuna anaependa amani ya Taifa itoweke. Hadi sasa matukio ya kutishia amani ya Nchi yamekuwa yakishika kasi bila kuona jitihada za makusudi za kukomesha hali hiyo. 

Toka kushambuliwa kwa wahariri Saed Kubeneana Ndimara Tegambwage, kutekwa na kuteswa kwa Dk. Stephen Ulimboka, kuuwa kwa Mwangosi, Mwenyekitiwa Jukwa la Wahariri Absalom Kibanda, kuuwa kwa mapadre na mashekh, mlipuko wa Olasit dhidi ya waumini wa Kanisa katoliki, migogoro ya kidini na mengineyo, hakuna hata limoja lillilopatiwa ufumbuzi wa kudumu.

 USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI
 

Mtandao pia unalaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuwanyima uhuru waandishi wa habari, na kuwafukuza waandishi wa habari katika mikusanyiko ya mjini Arusha.Mtandao unalisihi jeshi la Polisi kumwachia mwandishi wa Chanel Ten Ashiraf Bakari, aliyekamatwa tarehe 18/6/2013 katika eneo la Soweto alipokuwa akichukua picha za matukio ya jeshi la polisi dhidi ya raia waliopiga kambi katika viwanja. Tunaalani kitendo cha jeshi la polisi kumkamata bwana Ashirafu aliekuwa na vitendea kazi pamoja na kitambulisho chake cha uandishi wa habari.

WITO WETU
 

1. Tunamsihi Waziri Lukuvi aifute kauli yake dhidi ya asasi za kirai aambazo kimsingi kwamujibu wa utendaji kazi zao ni Watetezi wa Hakiza Binadamu katika fani mbalimbali na hawahusiki kwa namna yoyote ile katika hali ya sasa ya uvunjufu wa amani unaondelea nchini.
2. Aidha tunaomba asasi kwa upande wao zisijihusishe naitikadi yoyote ya kisiasa baliwaendelee kuwatumikia Watanzania waitikadizote bilaubaguzi wowote.
3. Jeshi la polisi mkoani Arusha limwachie mwandishi wa chanel Ten bwana Ashiraf Bakari, na kuwapa uhuru waandishi kureport habari yoyote.
4. Viongozi wote wakiwemo wa madhebu mabalimbali walaani vikali hali inaoyoendelea Arusha kwa sasa.
5. Balozi mbalimbali na Mashirika mbalimbali kukemea hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea Mjini Arusha.
6. Viongozi watambue kazi za asasi za kirai na kuzieshimu na kuacha kuwaita wachochezi
Tarehe, 19/06/2013 


Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania! 
Onesmo Olengurumwa 
Mratibu Wa Taifa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu

MWANDISHI WA HABARI WA CHANNELTEN CHARLES HILILA AFARIKI DUNIA MKOANI SHINYANGA


 

Aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Kituo cha Channelten Bw.Charles Hilila amefariki dunia  saa saba usiku katika Hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambako alikuwa amelazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya homa ya Malaria iliyokuwa ikimsumbua kwa muda wa siku chache zilizopita...MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU CHARLES HILILA ,AMENI

KADA WA CCM EMMANUEL MWAKASAKA AOKOA MAISHA YA MWANACHAMA WA CHADEMA


Mwanachama wa Chadema  Bi.Esther Moses  Ngoho mkazi wa kata ya Kakola manispaa ya Tabora ambaye amepatiwa msaada wa matibabu  na Kada wa CCM Bw.Emmanuel Mwakasaka ambaye alisema yuko tayari kumsaidia mama huyu ambapo aliweka ahadi ya kumpeleka katika hospitali yoyote duniani ilimradi aweze kupona magonjwa yanayomsumbua ambayo yamesababisha hali yake kuwa mbaya zaidi.
Baada ya Kada huyo wa CCM Emmanuel Mwakasaka  kuonesha moyo wa uzalendo wa kuwasaidia wananchi baadhi ya viongozi wa Chadema kata ya Kakola walivutika na kuamua kujiunga na CCM na wengine walidiriki kurejesha hata bendera za Chadema pamoja na kadi za Chama hicho.
Mmoja kati ya waliokuwa viongozi wa Chadema wakikabidhi bendera na kadi zao na kujiunga na CCM.
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Tabora mjini akionesha bendera ya Chadema iliyorudishwa na viongozi wa Chadema.