Saturday, August 24, 2013

USIKU WA SERENGETI FIESTA 2013 TABORA MJINI

 
Tamasha la Serengeti Fiesta  2013 katika uwanja wa Aly Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Msanii machachari wa muziki wa bongofleva/filamu Shilole akiimba huku akiwa na shabiki wake,huku shangwe na miluzi za mashabiki zikiwa zimetawala kila kona.
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kucheza jukwaani,wakionesha umahiri wao wa kukata nyonga mbele ya umati mkubwa wa washabiki waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan.


Msanii  wa muziki wa Bongo Fleva Kassim Mganga- akiwa jukwaani



Umati wa watu

Diamond na Ney nao walikuwa kivutio kikubwa katika tamasha hilo lililohudhuriwa na Maelfu ya washabiki.


Juma Nature na wenzie
Joh Makini na weusi picha ya chini


Wacheza Show wanaoibuka kwa kasi mkoani  Tabora nao walipata nafasi ya kuonesha ukali na umahiri walionao.

kutoka kundi la Tip Top Connections,Msanii  wa muziki wa kizazi kipya Madee alipanda jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake katika tamasha la Serengeti Fiesta 2013 Tabora.

Abdul Kiba,msanii wa muziki wa bongofleva akiimba mbele ya umati mkubwa wa wapenzi wa muziki wa kizazi kipya  Tabora waliohudhuria  tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia mbele ya baadhi ya wapenzi wa muziki wa kizazi kipya waliohudhuria tamasha la Serengeti Fiesta 2013 katika uwanja wa Aly Hassan Mwinyi Tabora.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah akiendelea kuwapatia burudani maelfu ya watu waliofurika katika show hiyo ya Fiesta.
  Msanii Amin  akiwa jukwaani wakati wa show hiyo kubwa ya Serengeti Fiesta  2013 mkoani Tabora,
Mmoja kati ya wasanii  wa  muziki wa kizazi kipya anayefahamika kama Baba Levo ambaye alipata fursa ya kupanda jukwaani kutoa burudani katika tamasha la Serengeti  Fiesta 2013 lililofanyika uwanja wa Aly Hassan  Mwinyi mjini Tabora.
Wakali wa kudansi kutoka THT,wakijulikana kwa jina la Makomanda wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaani usiku wa tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wa muziki wa dansi  kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,liinalofanyika katika uwanja wa Al-Hassan Mwinyi.

Msanii wa muziki wa bongofleva,Rachael akicheza jukwaani na mmoja wa madensa wake,huku mashabiki wake wakipiga mayowe ya shangwe.


Wadau wa Muziki wa Dansi mkoani Tabora Eddy Ngwasuma akiwa na Christian Bela wakati wa tamasha hilo la Serengeti Fiesta 2013.

Wadau wa TABORALEOhabari.COM nao hawakubaki nyuma


PSI YAHAMASISHA UZAZI WA MPANGO KWA KILA KATA MKOANI TABORA





                        
NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
WANANCHI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI MKOANI TABORA WAKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MSIMAMISI WA BANDA LA PSI KWENYE VIWANJA VYA NANENANE MKOANI HAPA JUU YA UZAZI WA MPANGO
HATA WANAFUNZI HAWAKUWA MBALI KWA AJILI YA KUJIFUNZA MASWALA YA UZAZI WA MPANGO NA MAMBO MENGINE KWA AJILI YA MASOMA YA SANYASI

Shirika la Psi mkoa wa Tabora limetoa hamasa kwa wananchi juu ya umuhimu wa uzazi wa mpangona huduma hiyo utolewa bure kwa kina mama wanaotaka huduma hiyo

Huduma hiyo imekuwa ikitolewa kwa kushirikiana na wizara ya afya na ustawi wa jamii mkoani hapa katika zahanati zilizopo katika kata zaote za mahispaa ya Tabora

Akizungumza na watu waliofika katika banda hilo la PSI afisa mhamasishaji maswala ya uzazi wa mpango wa shirika  mkoani Tabora. Haika Msuya alisema  kuwa shirika hilo linafanya kazi kwa kushirikiana na Idara ya afya mkoa katika kutoa huduma hiyo kimkoa yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya nanenane mkoani hapa.

Alisema kwamba Katika kutoa huduma hiyo wanatembelea vituo vya afya  mbalimbali kwenye kata zote za mkoa wa Tabora na kutoa huduma hiyo bure  kwa akina mama wanao taka kupanga uzazi.
Afisa huyo aliwashauri pia akina baba waliotembelea banda hilo kwenye maonesho ya nanenane kukaa na wake zao na kupanga nao juu maswala ya uzazi wa mpango maana itawasaidia katika kupanga mambo ya kimaendeleo.

Pamoja na mambo mengine katika maonesho hayo banda la shirika hilo lilikuwa likitoa elimu ya ukimwi juu ya matumizi sahihi ya kondomu pamoja na kutoa elimu juu ya maswala ya uzazi wa mpango.

Katika wiki hiyo ya maonesho ya nanenane shirika hilo la Psi lilikuwa likitoa huduma hiyo bure ya kufunga uzazi kwa muda mrefu kwa njia ya vitanzi na vipandikizi katika zahanati ya Isevya mkoani Tabora.

mwisho

Wednesday, August 21, 2013

KALIUA HATUTAKIA HATI CHAFU -MWENYEKITI JOHN KADUTU



 
 NA LUCAS RAPHAEL KALIUA

Wataalamu na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya kaliua mkoani Tabora wameaswa  kufanya kazi kwa bidii na kuepuka vitendo vya ubadhirifu wa mali na fedha za umma ili halmashauri hiyo ipate hati safi wakati wote.

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo ,John Kadutu wakati akilihutubia baraza la kwanza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua lililokutana katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Kaliua.

Alisema watumishi hao wanapaswa kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kuifanikisha  halmashauri hiyo kupata hati safi na sio hati ya mashaka wala chafu kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi  mkuu wa hesabu za serikali nchini.

Kadutu amebainisha kuwa halmashauri hiyo haitawavumilia watumishi wazembe na wabadhirifu ambao wataisababisha halmashauri hiyo kushindwa kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

Alibainisha kuwa wafanyakazi hao watakuwa na uhalali wa kuendelea kufanya kazi katika halmashauri hiyo endapo watajituma kufanya kazi kwa juhudi na maarifa jambo ambalo litasaidi kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili wilaya hiyo mpya.

Kadutu amewataka wakuu wa idara kuweka taarifa zao vizuri na kwa usahihi kila mara na kuondokana na tabia ya ubabaishaji ambao umekuwa ukijitokeza katika halmashauri nyingine na kwamba madiwani hawatokuwa tayari kuburuzwa ili kupokea taarifa za ubabaishaji.

Hata hivyo amemtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kuwasimamia kwa karibu wakuu wa idara na watumishi wengine wa halmashauri hiyo katika utekelezaji wa majukumu yao na hivyo kuiepusha ubabaishaji.

Aidha mwenyekiti huyo amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kutimiza wajibu wao kwa kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo na fedha za umma zinazotengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali wilayani humo.

Alikemea tabia ya baadhi ya madiwani wanakumbatia maovu kwa kupitisha miradi iliyotekelezwa chini ya kiwango ikiwemo majengo ya idara mbalimbali katika maeneo yao jambo ambalo linapaswa kuachwa mara moja kwa kutofanya kazi kwa mazoea.

Mwenyekiti John Kadutu amekuwa mwenyekiti wa kwanza wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua baada ya kuchaguliwa kwa kura 25 za ndio zilizopigwa na wajumbe 25 wa kikao hicho cha baraza la madiwani.
Halmashuri ya wilaya ya Kaliua imezaliwa kutokana na kuundwa kwa wilaya mpya ya Kaliua kutoka ambapo awali ilikuwa wilaya ya Urambo.

MWISHO


Tuesday, August 20, 2013

MBOWE;KATIBA HAINA DINI,RANGI,KABILA




NA LUCAS RAPHAEL NZEGA 

MWENYEKITI wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa katiba haina dini,rangi wala ukabila kutokana na umuhimu wake kwa maisha ya wananchi ya kila siku.

Akiwahutubia wananchi wa Nzega mjini katika viwanja vya parking jana alisema kuwa wananchi wanapaswa kutoa maoni yao dhidi ya rasim ya katiba kabla ya Agust 30 mwaka huu.

Alisema chama hicho kinapiga kampeni ya kuhamasisha waTanzania kuangalia mambo ya msingi katika katiba hiyo ambayo yataleta tija kwa wananchi ilikatiba ijayo iwena masirahi kwa wananchi wote.

Alisema kuwa endapo wananchi wakipuuzia ushauri huo utawagharim kwa miaka kadhaa na kusababisha hali mbaya ya maisha dhidi ya katiba itakayo pita.

Alisema kuwa mchakato huo wa kukusanya maoni ya katiba hauna itikadi ya kisiasa,Dini,rangi wala kabila bali ni masirahi ya wananchi wote hapa nchini ambapo wanapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha ilikuweza kupata katiba itakayo wasaidia katika maisha yao.

Alisema kuwa watanzania waliobahatika kutoa maoni ya katiba katika duru ya kwanza ni wachache kuliko idadi iliyopo na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa watoe maoni yao katika kupata katiba waitayo yenye masirahi ya msingi kwa kila mtanzaia.

Mwenyekiti huyo aliipongeza Tume ya mabadiliko ya katiba inayongozwa na mwenyekiti wake Jaji sinde warioba kuwa imetoa rasimu ya msingi yenye maoni ya watanzania na kuongeza kuwa baadhi ya vyama vya siasa vinafanya utaratibu wa kuipinga rasim hiyo baadhi ya vipengele.

Kwa upande wake mnadhimu wa kambi ya upinzani Tundu Lisu alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM kinampango wa kupinga baadhi ya vipengele ikiwepo na mfumo wa serikali tatu.

Alisema kuwa maoni ya wananchi yaheshimiwe kimsingi kutokana na rasimu hiyo ya katiba hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kutoa maoni yao dhidi ya rasimu hiyo ya katiba.

Lisu alisema kuwa katika Bunge la katiba lijalilo litakuwa halitoshi kutokana na kuhakikisha haki za wananchi zinapatiwa ufumbuzi wa kutosha ili kila maoni ya msingi yawqeze kupita.

Alisema kuwa watahakikisha vipengele vyote vinasimamiwa kikamilifu kwa kuzingatia sheria na utaratibu na kuongeza kuwa wananchi wazingatie mambo yao ya msingi waliyoyataka katika maoni.

Shuguli za uzalishaji mali nzega mjini ikiwepo kufungwa kwa maduka,soko zilisimama zaidi ya masaa sita kutokana na wananchi kukusanyika kwa wingi kusubili msafara huo wa mwenyekiti wa chama hicho pamoja na mnazimu wa kambi ya upinzani Tundu Lisu.

Mwisho.


AFISA MTENDAJI KATA YA NG'AMBO MANISPAA YA TABORA AIBUKA MSHINDI WA BAJAJI YA TIGO


Afisa masoko wa Tigo Bw.Alex Msigara akikabidhi Bajaji kwa mshindi wa droo ya Miliki Biashara yako Bw.Elyasa Mvano ambaye ni Afisa mtendaji kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora.


 Bw.Mvano wakati alipokabidhiwa Bajaji yake ambaye aliahidi kuanza kufanyia biashara ya usafirishaji Tabora mjini.

SITTA;"TANZANIA HAIWEZI KUPATA KATIBA NZURI MPAKA WANANCHI WATAKAPOKUBALI KUWA WAZALENDO KWA NCHI YAO"


 

Waziri wa Afrika Mashariki Bw.Samwel Sitta akizungumza wakati wa kikao cha baraza la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Tabora,ambapo aliwataka  vijana kuwa wazalendo kwa kuipenda nchi yao kwa kuonesha msimamo wao wa kutowakubali watu wanaotaka madaraka kwa kutumia fedha walizonazo.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora Bw.Seif Ghulamali alizungumzia hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili Jumuiya hiyo kiasi cha kukosa hata fedha za kuendesha shughuli zake za kiofisi katika kuwahudumia wanachama wake.