Friday, July 25, 2014

WANAWAKE WATWANGANA SOKONI HUKU WAKIWA NA SWAUMU-TABORA

 







Baadhi ya wanawake watatu katika soko la mkulima Tabora mjini wamejikuta wakipeana kipigo kikali mchana kweupe wakati walipokuwa wakifanya biashara za mbogamboga hatua ambao ilisababisha kuharibu sehemu ya bidhaa wanazouza ambapo muda mfupi baadae waliamuliwa ugomvi huo na askari polisi Fakih Abdul aliyekuwa akipita sokoni hapo,hata hivyo chanzo cha ugomvi huo kimetokana na mmoja wa wanawake hao kuwa mbabe kwa wenzake na hivyo kushindwa kumvumilia kutokana na vituko vyake. 

MAUAJI YA VIKONGWE YASHIKA KASI MLELE- KATAVI



???????????????????????????????
(Picha zote na Kibada Kibada –Mlele Katavi)

Na Kibada Kibada –Mlele Katavi.
 
Wimbi la mauaji kwa watu wenye umri kuanzia  miaka 60 na kuendelea  Wilayani Mlele Mkoani Katavi linaonekana kushika kasi na kutishia hali ya ulinzi na usalama kama hatua za makusudi hazitachukuliwa.

Hii ni kwa Mujibu wa Taarifa ya Hali ya ulinzi na Usalama Wilayani humo  iliyotolewa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa wilaya hiyo , Zabron Ibeganisa kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Madiwani uliokuwa ukipokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizotekelezwa kwa kipindi cha mwaka  wa 2013/2014.

Mkuu huyo wa upelelezi wa makosa ya jinai alieleza kuwa changamoto zitokanazo na matukio ya mauaji ni kubwa katika wilaya hiyo  na watu wanaolengwa na mauaji hayo ni wale wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea ambapo kwa sehemu kubwa mauaji hufanyika nyakati za usiku kwa kuwavamia walengwa kwenye makazi yao.

Alisema katika matukio 24 yaliyotokea, watu 24 kwa kipindi cha januari hadi juni mwaka 2014   wameuwawa na waliolengwa hasa ni watu wa umri huo.

Alisema kuwa wauaji hao hutumia silaha zenye makali kama panga,shoka, na sime kuwakata waliowalenga na kisha kutoweka bila kuchukua kitu chochote.

Mauaji haya yanafanana sana na jinsi yanavyotokea katika mikoa ya Shinyanga kwa kuwaua vikongwe kwa imani kwamba ni wachawi.

Aidha akifafanua zaidi alieleza kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita kuanzia mwezi januari hadi juni 2014 ,  yametokea mauaji 24 na watu 24 wameuwawa  ambapo kati ya mauaji hayo watuhumiwa sita walikamatwa.

Akibainisha hali ya uhalifu katika wilaya hiyo alieleza kuwa matukio mbalimbali ya makosa madogo ya kuwania mali yalikuwa 107 makosa makubwa dhidi ya binadamu kwa mauaji yalikuwa 24, kubaka 23,kulawiti mawili ,makosa madogo dhidi ya Binadamu yalikuwa 194, makosa madogo dhidi ya uvunjwaji wa maadili yalikuwa 108,  ajali zilizosababisha vifo ni mbili,ajali zilizosababisha majeruhi zilikuwa 39, ajali za kawada 17, makosa mengine 844.

Makosa makubwa dhidi ya maadili ya jamii kama kupatikana na bangi yalikuwa manane, kupatikana na pombe ya moshi 8, makosa ya kupatikana na nyara za serikali yalikuwa matatu na kupatikana na silaha moja
Ipo changamoto kutokana na ugumu uliopo wa kuwatambua wauaji ,hata hivyo jeshi la polisi linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo na kuwaasa  wana jamii  kuendeleza  ule utaratibu wa  daftari la wakazi kwa kuwaorodhesha wakazi kwenye maeneo kwa kuwa ni muhimu na litasaidia kuwatambau wageni wanaoingia kwenye maeneo na iwapo watakuwa na nia mbaya watabainika.

"MWANDISHI WA HABARI WA REDIO YA MHESHIMIWA RAGE MBARONI KWA KUJIFANYA USALAMA WA TAIFA,UONGOZI WA V.O.T WAMKANA


Kijana mwandishi wa habari  akiwa mbaroni baada ya kukamatwa na makachero wa Jeshi la Polisi Tabora mjini akijifanya ni Afisa usalama wa Taifa,Mwandishi huyu ambaye anafahamika kwa jina la Mussa Mbeko(24)aliwahi kufanya kazi katika kituo cha Redio Voice of Tabora kinachomilikiwa na Mheshimiwa mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Ismail Rage ambapo hata hivyo Uongozi wa VOT umesema kuwa tayari ulikwisha mfukuza kijana huyo kwa makosa mbalimbali ya Utapeli hasa kujifanya usalama wa taifa.  
Kitambulisho alichokuwa akikitumia Mussa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu

Uongozi wa Jeshi la Polisi wilaya ya Tabora ulimfikisha  Mwandishi huyo mbele ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP  Suzan Kaganda
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha waandishi wa habari kitambulisho kilichokuwa kikitumiwa na Mussa Mbeko akijifanya ni Afisa Usalama wa Taifa.

"AJIRA YA VIJANA KWA USAFIRI WA BAISKELI TABORA NI MOJA KATI YA AJIRA TULIZOZITEGEMEA"

 
Usafiri baiskeli mkoani Tabora wazidi kuimarisha ajira kwa vijana hatua ambayo sasa imefanya kuwepo kwa ongezeko la vijana wengi mjini kuliko ilivyokuwa hapo awali,kwa hivi sasa imeshuhudiwa baadhi ya vijana wa vijiji jirani na Tabora mjini wamekuwa wakijidamka mapema asubuhi kuja mjini kufanya kazi ya kusafirisha abiria kwa usafiri huo wa baiskeli na kujipatia fedha kwa ajili ya kujikimu kimaisha wakati huu wa majira ya kiangazi ambapo vijijini hakuna shughuli za kilimo.Hata hivyo licha ya vijana hao kupata fursa ya kujiajiri wenyewe lakini wamekuwa katika mazingira hatarishi kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawajui sheria za usalama barabarani na hivyo kujikuta wanavunja sheria na kusababisha ajali zinazochangia vifo visivyo vya lazima au kubaki na ulemavu wa kudumu.Jambo hili linahitaji kuchukuliwa hatua ya kuwadhibiti vijana hao bila kuathiri mwenendo mzima wa ajira zao kwakuwa wengi wao kutokana na ajira hizo wanategemewa na familia zao.Ajira za vijana kwa kutumia usafiri wa baiskeli katika mtazamo wa harakaharaka ni dhahiri kwamba ni ajira tulizozitegemea kwa kile kinachoonekana katika fikra za haraka kwa vijana waliowengi ni kujipatia fedha za chapchap kupitia mpango huo usio rasmi.Aidha kwa upande mwingine ni kweli kwamba kwasasa mkoa wa Tabora hakuna viwanda au kazi nyingine zaidi ya kupata vibarua kwenye majengo ya watu binafsi ambayo malipo yake ni kati ya shilingi 3000 na 5000 kwa kutwa nzima.Ukiachilia mbali ajira kwenye makampuni ya ulinzi imekuwa na usumbufu kwa vijana kutokana na kutolipwa mishahara kwa wakati jambo ambalo linawafanya vijana wengi kuona ni bora zaidi aendeshe baiskeli kuanzia majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu usiku ambapo hujipatia wastani wa kiasi cha shilingi elfu kumi.Hii inawafanya idadi kubwa vijana kuingia kwenye ajira hii bila kikwazo kwani kwa wanaoishi mjini huweza kumudu kulipa kodi ya pango ya shilingi elfu kumi kwa mwezi lakini hata kuendesha maisha yake na familia ya watu wanne yaani Mke,watoto wawili na yeye mwenyewe.Kuendesha baiskeli hakuhitaji leseni wala kikwazo chochote kinachowabana kisheria zaidi ya kujaza upepo kwenye tairi za baiskeli na kuanza kunyonga pedeli kulingana na uzito wa mteja aliobebwa kwenye usafiri huo.Ni kazi nyepesi kama waionavyo vijana wenyewe.Lakini kwa wachunguzi wa mambo wanasema kuwa hata wimbi la vibaka katika maeneo mbalimbali Tabora mjini limepungua kwa kiasi kikubwa kwakuwa kijana anayejihusisha na ajira hiyo ya usafiri wa baiskeli anapomaliza muda wake hiyo saa tatu usiku huwa amechoka sana hata hawezi kwenda kukaa  vijiweni na kujihusisha na vitendo viovu. 

SERIKALI YASAINI MIKATABA MIWILI YA UJENZI WA BARABARA ZA JUU KWA JUU

 


1 (4)Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya mikataba miwili ya ujenzi wa barabara za juu kwa juu katika makutano ya TAZARA na usambazaji umeme jijini Dar es salaam leo zenye thamani ya zaidi ya bilioni 128.
2 (4)Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakisaini hati ya makubaliano ya mikataba miwili ya ujenzi wa barabara za juu kwa juu katika makutano ya TAZARA na usambazaji umeme jijini Dar es salaam leo zenye thamani ya zaidi ya bilioni 128.
3 (4)Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akionyesha michoro ya itakavyonekana barabara za juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam leo wakati wa kusaini hati ya makubaliano ya miradi miwili zenye thamani ya zaidi ya bilioni 128 na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia).

"KILA MTU ANA HAKI YA KUGOMBEA UBUNGE,KAMA ULIWAJIBIKA VIZURI KWA WANANCHI WATAKUCHAGUA TENA"-MH.MUNDE


 

 
Na Mwandishi wetu.

"Hakuna mtu mwenye haki miliki ya Ubunge,kwani hiyo ni dhamana tu tuliyopewa na wananchi,lakini kwanini ifikie hatua ya watu kuhitilafiana na kugombana pasipo sababu za msingi"hii ni kauli ya Mbunge wa vitimaalumu  mkoa wa Tabora Mheshimiwa Munde Tambwe wakati akizungumza na mtandao huu.

Wakati huu kabla  ya kuelekea kwenye mchakato wa kura za maoni  kwa Chama cha Mapinduzi kumekuwa na hali ya kupigana vikumbo kwa baadhi ya makada wa Chama hicho hatua ambayo imebadili kabisa ukurasa wa maisha ya kawaida ya kibinadamu na kujenga sura mpya ya siasa za chuki kwa mtu mmoja kumchafua mwingine au kikundi cha watu fulani kumchafua mtu mmoja jambo ambalo linadhihirisha watu wamesahau kabisa majukumu yao na kugeuza kuwa ni ajenda muhimu ya katika maisha.

Jambo hili limemsukuma Mbunge wa vitimaalum Mheshimiwa Munde Tambwe na kuona kuwa watu wanakoelekea siko ambako CCM inataka kutekeleza malengo yake katika kuwahudumia wananchi ambao kimsingi ndio wamekiweka madarakani chama hicho.

"Ninavyofikiri mimi kwa muda huu sisi kama wanaccm ni vema tushirikiane,tujenge mshikamano katika kutekeleza Ilani ya Chama chetu badala ya kukaa tunajengeana chuki zisizo na msingi,yaani huyu kamsema yule na yule kamsema huyu,hii haitusaidii kabisa itatufanya tushindwe kujibu maswali ya msingi ya wananchi watakapo tuuliza nini tumefanya tangu tuwe madarakani"alisema Mheshimiwa Munde

"Ubunge si haki miliki ya mtu,kwani yeyote anahaki ya kugombea muda ukifika lakini kwasasa tunatakiwa kuwasaidia wananchi,wewe kama umewajibika ipasavyo kwa wananchi, wenyewe watakuchagua hata kama ni vipindi vitatu,lakini kama umepewa dhamana ya kuwa mbunge halafu unashindwa kutekeleza majukumu yako huna sababu ya kugombana na watu,wananchi wenyewe wataamua na wewe utavuna ulichopanda"msisitizo wa ziada wenye lengo la kujenga.

Kwa kauli hii ni vema pia watu waliopewa dhamana au ridhaa na wananchi ya kushika wadhifa walionao wapate fursa ya kujipima,je,wanayo nafasi tena ya kujitosa wakati wa kura za maoni utakapowadia?au ndio kuanzisha chuki na vurugu kwa kila mtu mwenye uwezo wa kifedha unayemuona amevaa sare ya Chama na kutoa misaada kwa watu  unamhisi anataka kuchukua nafasi yako?

"Hakuna mtu anakatazwa kushirikiana na wengine katika kufanya kazi za chama ni vema tukafuata taratibu na kanuni za chama chetu na muda ukifika refarii atapuliza kipenga kila mmoja wetu ataona kama anauwezo wa kuomba nafasi anayoitaka kuliko kuanza kujipitisha huku na kule na kujinadi,binafsi sitofanya hivyo isipokuwa nawaombeni makada wenzangu tushirikiane kutekeleza Ilani ya chama chetu ili wenzetu wa vyama vya upinzani wakose la kuhoji"alisema Mheshimiwa Munde

"Chama cha Mapinduzi kina utaratibu mzuri sana katika kuwapata viongozi wa kada mbalimbali wakiwemo wabunge ni dhahiri kwamba mtu akifuata taratibu na kanuni za chama chetu atakuwa na haki ya kuwania nafasi anayoitaka na si kweli kwamba kutumia fedha kwa maana ya kuwahonga wapigakura inaweza ikawa sababu ya kuchaguliwa hilo si kweli"alisema huku akitahadharisha wanachama hasa makada ni vema wakashirikiana katika kutekeleza majukumu ya chama katika kutimiza ahadi zilizotolewa na viongozi wakati wa kuomba ridhaa kwa wananchi uchaguzi wa mwaka 2010.

"KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KUUJENGA MKOA WETU,VIONGOZI TUWASAIDIE  WATU WAONDOKANE NA UMASIKINI WA KIPATO,CCM DAIMA"      

POLISI APONGEZWA BAADA YA KUKATAA RUSHWA YA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA-TABORA


Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akimpongeza na kumpa zawadi ya pesa Mkaguzi wa Polisi Harun Kasubi baada ya kufanikiwa kuwakamata watu wapatao kumi na wawili waliokuwa wamejifungia ndani ya Guest house inayofahamika kwa jina la KENIOS wakiwa wanajidunga dawa za kulevya ambapo watu hao walitaka kumpa rushwa ya shilingi 90,000/=ili waachiwe huru.
Baadhi ya dawa za kulevya na vifaa vya matumizi ya dawa hizo zilizokamatwa zikiwa zinatumiwa na watu hao kumi na wawili waliokamatwa KENIOS GUEST HOUSE huko eneo la kata ya Isevya manispaa ya Tabora.
Kamanda wa Polisi ACP Suzan Kaganda ameuambia mtandao huu kuwa waliokamatwa katika operesheni ya kuwasaka watumiaji,wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya mkoani Tabora ni Hamisi Athuman Mbao(39) ,Issa Abdallah(22),Ally Bakar(34),Densi Petro(34)Mrisho Shaban(22)Ramadhan Mbade(40)Haji Muki(40),Said Kasumari(24),Shaban Haruna(25)David Male(43)Ramadhan Hamis na Paschal Robert.

Kamanda Suzy amesema watu hao baada ya kukamatwa walitaka kutoa rushwa ya shilingi elfu tisini kwa kiongozi wa timu ya makachero wanaofuatilia dawa za kulevya mkoani Tabora ambaye ni mkaguzi wa Polisi Harun Kasubi ambapo alikataa na kuwafikisha kituo kikubwa cha Polisi Tabora.

TRA YAFUTURISHA BAADHI YA WANANCHI TABORA



Baadhi ya waalikwa akiwemo Meneja wa kanda wa Bima ya Afya mkoa wa Tabora Bw.Emmanuel Adina wakishiriki hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya mapato Tanzania TRA katika hotel ya ORION Tabora mjini.
Baadhi ya viongozi wa Serikali na vyama vya siasa akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake UWT mkoa wa Tabora Bi.Mwanne Mchemba walishiriki katika hafla hiyo ya Futari
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tabora mjini Bw.Moshi Abraham maarufu Nkokota naye alikuwa ni mmoja kati ya wageni waalikwa
Baadhi ya walipa kodi ambao ni wamiliki wa makampuni ya mabasi Tabora kushoto ni  Bw.Medd Nassor Hamdani,mmiliki wa mabasi ya NBS na Bw.Humud Nassor ambaye ni mmiliki wa mabasi ya SUPER SONIC nao walikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa 

Baadhi ya walipa kodi wafanyabishara wa Tabora
Baadhi ya watumishi wa TRA Tabora nao walishiriki hafla hiyo ya Futari
Mkurugenzi wa Fedha  wa TRA Tanzania Bw.Salehe Mshoro akizungumza katika hafla hiyo ya Futari ambapo alizungumzia mafanikio makubwa ya ukusanyaji wa kodi ya mapato nchini huku akitumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyabishara kwa ushirikiano wanaoitapatia TRA
Katibu wa ccm mkoa wa Tabora Bw.Idd Ali Ame akizungumza katika hafla hiyo ya Futari
Mmoja kati ya viongozi wa dini ya kiislam Tabora mjini Sheikh Issa Bilali akisoma dua maalum wakati wa hafla hiyo.
Mjumbe wa NEC Bw.John Mchele akipeana mkono na Mkurugenzi wa fedha wa TRA nchini Bw.Mshoro,pembeni ni Meya wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij

Friday, July 18, 2014

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUIELIMISHA JAMII KUHUSU DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA LINALOTUMIA TEKNOLOJIA YA BVR

Makamu Mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzi  ambaye pia ni  Jaji mkuu  Mstaafu wa Zanzibar  Mh. Hamid Mahmood Hamid akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Tabora kuhusu uboreshaji wa daftari la mpiga kura litakalotumika kwa mwaka 2014-2015.
Baadhi ya waandishi wa habari pamoja na maafisa wa tume ya uandikishaji wa daftari la mpira kura katika mkutano wa tume hiyo na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora ambapo waandishi waliaswa kuwa mstari wa mbele katika kuihabarisha jamii kujitokeza wakati wa uandikishaji wa daftari la mpiga kura utakapo wadia.

BENKI YA EXIM YAFUNGUA MILANGO KUSAIDIA MICHEZO KWA VIJANA TABORA

Meneja masoko wa Benki ya Exim Jeremia Majebele akikabidhi cheti cha mafunzo ya ualimu wa mpira wa miguu ngazi ya kati kwa mmoja wa wahitimu wa kozi hiyo ya siku 14  ambaye pia ni afisa wa Jeshi la Polisi Tabora mjini Hussein Juma Katanga
Meneja masoko wa Exim tawi la Tabora Jeremia Majebele akifunga mafunzo hayo ambapo alisema  kuwa Benki ya Exim inaunga mkono juhudi za kuibua michezo mkoani Tabora na kuahidi kuwa ipo tayari kusaidia michezo kwa vijana.
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya walimu wa soka mafunzo yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
Mkufunzi wa mafunzo hayo ya walimu wa soka Meja mstaafu Omari Mingange akitoa maelezo mafupi wakati wa hafla ya ufungaji mafunzo hayo
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo akipeana mkono na Meneja Uendeshaji  huduma wa Benki ya  Exim Philip Metusela na Meneja masoko  wa Exim Jeremiah Majebele  akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Makocha mkoa wa Tabora TAFCA Mohammed Mozi muda mara baada kukamilika kwa hafla fupi ya kufungwa kwa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja wahitimu wa mafunzo ya ualimu wa soka,viongozi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora TAREFA,TAFCA pamoja na maafisa kutoka Benki ya Exim hali inayoonesha ni jinsi gani Exim ilivyo karibu na wadau wa michezo.


 

21 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA WA SOKA TABORA

Meneja masoko wa Benki ya Exim tawi la Tabora Jeremia Majebele akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya ualimu wa mpira wa miguu John Kilowoko ambaye ni mtumishi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora baada ya kuhitimu kozi ya ualimu wa soka ngazi ya kazi.
Na Allan Ntana, Tabora

WAALIMU 21 wanaofundisha timu za mpira wa miguu kutoka mikoa ya
Simiyu, Shinyanga, Mbeya na Tabora wamehudhuria na kuhitimu mafunzo ya
ukocha (intermediate course) yaliyofanyika katika uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi mjini Tabora.

Mafunzo hayo yaliyochukua muda wa wiki 2 yaliendeshwa na Mkufunzi
mahiri hapa nchini Meja mstaafu Abdul Omar Mingange toka jijini DSM,
ambapo washiriki 22 walitoka mkoani hapa huku 2 wakitokea Shinyanga, 1
Simiyu na 1 jijini Mbeya.

Akikabidhi vyeti kwa waalimu hao, Meneja Masoko wa benki ya EXIM tawi
la Tabora Jeremia Bajebere aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Meneja
wa tawi hilo Edwin Poul aliwataka wahitimu hao kujiendeleza zaidi ili
wawe na kiwango kikubwa kwani ukocha ni ajira nzuri sana siku hizi na
inalipa.

Mwenyekiti wa Chama cha Makocha (TAFCA) mkoani Tabora Mwl Mohamed Ali
Mozi alisema lengo la mafunzo hayo ni kuinua viwango vya makocha toka
ngazi ya awali kwenda ngazi ya juu ili waweze kutoa elimu bora
itakayosaidia kuinua kiwango cha soka kwa vijana katika mikoa yao.

‘Hawa waalimu wamepata taaluma nzuri sana ya mpira wa miguu, naamini
watasaidia sana kuinua soka la vijana mashuleni na katika vilabu
mbalimbali ikiwemo kutambua vipaji vya wachezaji na kuviinua’,
aliongeza.

Aidha alisema changamoto kubwa inayowakabili waalimu wa soka hapa
nchini ni uhaba wa vifaa vya michezo vya kufundishia sambamba na vyama
vya soka kutowatambua na kuwatumia ipasavyo makocha wazawa kama mtaji
wa kuinua vipaji katika mchezo huo.

Mkufunzi wa mafunzo hayo Meja mstaafu Abdul Omar Mingange amesifu
mwitikio mkubwa na kiwango kilichoonyeshwa na waalimu hao wakati wa
mafunzo hayo yaliyoendeshwa kwa nadharia na vitendo jambo ambalo
limewawezesha kufaulu kwa alama za juu.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani Tabora Yusuph Kitumbo
amepongeza hatua ya waalimu hao kujitokeza kwa wingi katika mafunzo
hayo kwani itaongeza idadi ya makocha wa soka mkoani humo huku
akiahidi kulipa gharama zote  za vyeti vya wakufunzi hao.

Alisema kuwa kuanzia sasa timu zote hapa Tabora kuanzia daraja la nne
na kuendelea ni lazima zifundishwe na makocha waliopitia mafunzo
maalumu yaliyoandaliwa na chama cha Makocha TAFCA ili waweze kutumia
elimu yao vyema.

WASIO NA KADI YA BVR KUTOPIGAKURA 2015-KIGOMA,TUME



Na Magreth Magosso,Kigoma


IMEELEZWA kuwa,wananchi wasiokuwa na vitambulisho vya mfumo wa Biomertic Voter Registration hawatahusika katika mchakato wa kupiga kura wa maoni  na uchaguzi mkuu 2015.


Akifafanua hilo Kamishana wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Hamid Mahmoud  alisema  wanananchi hawana budi kupokea mfumo huo,ambao ni tiba ya kuondoa changamoto ya uchakachuaji wa mtu mmoja kupiga kura zaidi ya mara mbili.


“huu mfumo wa BVR inachukua taarifa za kibailojia ya muhusika hivyo si rahisi kuibika inatambua tabia,alama za vidole,sura,mpangilio wa mikono,mboni ya jicho,sauti  na harufu ya mtu na kuhifadhiwa katika kanzi data na  jamii ishiriki  kujiandikisha.” A libainisha Mahmoud.


Alisema mchakato upo kwa watu wote, walio na kadi ya kupigia kura za awali zenye mfumo wa `optical mark recognition’  kutoa picha papo kwa papo na wale ambao wanatarajia kutimiza miaka 18 ifikapo 2015 wanawajibika kushiriki  kupata kadi ya `BVR’ ili kuboresha daftari la kudumu la kupiga kura.


Kwa  upande  makam Mwenyekiti wa tume  ya Uchaguzi Taifa Mohamed  Kiboko alibainisha changamoto za awali ni pamoja na kushindwa kubadilisha taarifa za mtu kwa wakati husika,majina kujirudia zaidi ya mara moja,kuwepo na majina ya marehemu na kutoonekana kwa majina ya wapigakura.


Alisema  wananchi walio na kadi za awali wanahitajika waende na vitambulisho hivyo ili wapewe vitambulisho vya kisasa na endapo atakuwa amehama au kubadilisha taarifa zake inabidi atoe taarifa husika kwa mwandishi mapema ili kurekebisha na kumwezesha kupiga kura eneo husika.

Aliongeza kwa kusema wananchi wasio raia wa hapa watabainika kupitia wadau wao kama tasisi ya Rita na Nida katika kuthibitisha data za muhusika na kuomba wananchi wawe wazi kuwafichua wahamiaji wasio rasmi ili wasitumie fursa hiyo.


Aidha itambulike kuwa,taifa hili si ya kwanza kuanza kutumia mfumo huo kutokana na nchi kadhaa wanatumia mfumo wa BVR ikiwemo Zanzibar(2009),mali(2005),Nigeri(2007)Ghana(2009),Uganda(2008),Kenya(2013),Liberia(2005),Zambia(2008),Afrika kusini (2009),guinea(2005.


Alisema changamoto zilizojitokea katika mataifa hayo hayahusiani na mfumo huo wa Biometric na kudai mfumo huo ni tiba sahihi ya changamoto za awali ambazo ziliikwaza tume hiyo na serikali husika.

JENGO LA MAABARA YA KISASA LA NIMR LAFUNGULIWA TABORA


Mkurugenzi wa NIMR Tabora Dr.Joseph Swila akionesha baadhi ya vifaa vya kisasa katika chumba cha maabara hiyo ambayo inatajwa kuwa huenda ikasaidia mikoa yote ya kanda ya magharibi.
Baadhi ya watumishi wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu NIMR pamoja na viongozi wa ngazi za juu  wa NIMR katika picha ya pamoja wakati ufunguzi wa Jengo la maabara ya utafiti wa kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu mjini Tabora.
Jengo la maabara ya utafiti katika kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu lililogharimu zaidi ya shilingi milioni.297.8
Mkurugenzi wa tume ya sayansi na teknolojia Dr.Hassan Mshinda akifungua jengo la Kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu kwa niaba ya naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof.Makame Mnyaa Mbarawa lililopo mjini Tabora. 
Dr.Hassan Mshinda akiangalia moja ya mashine ya kupimia magonjwa ya binadamu wakati akikagua jengo hilo na kuangalia vifaa tiba vilivyomo katika jengo hilo.

Mkurugenzi wa NIMR Tabora Dr.Joseph Swila akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la maabara ya Tabora
Mkurugenzi mkuu wa NIMR Dr.Mwele Malecela wakati akisoma taarifa fupi tangu kuanzishwa kwa maradi wa Jengo hilo la maabara ya kisasa.
Mwenyekiti wa Bodi ya NIMR ,Prof.Samwel Masele Akizungumza wakati wa sherehe fupi ya ufunguzi wa jengo la maabara ya kisasa.
Mkurugenzi wa tume ya Sayansi na Teknolojia Dr.Hassan Mshinda akisoma hotuba kwa niaba ya naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ambapo alipongeza kazi kubwa inayofanywa na NIMR katika kuhakikisha inakabiliana na magonjwa mbalimbali kwa kufanya utafiti wa magonjwa na kupata ufumbuzi wake.
Mwandishi wa habari mkongwe wa Redio Tanzania Bw.Benkiko ambaye alipata fursa ya kusalimiana na mgeni rasmi wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo hilo
Wadau mbalimbali wa afya walihudhuria katika sherehe za ufunguzi wa Jengo hilo.Picha zote na TABORALEOhabari.COM