Monday, August 25, 2014

SHANI AKILA KIAPO MBELE YA MKEWE NA WAUMNI WA KANISA HILO

MAKAMU ASKOFU MKUU WA KANISA LA FPCT LAZARO AKIMWAPISHA MCHUNGAJI WA KANISA LA KILOLENI PETER SHANI KUWA MGUNGAJI WA KANISA HILO KILOLENI

FPCT YAPATA KANISA LA 18 KILOLENI TABORA

MAKAMU ASKOFU MKUU WA KANISA LA FPCT WILSON LAZARO WAKATI AKIZUNDUA UFUNGUZI WA KANISA HILO KILOLENI TABORA MJINI JANA

AKIKATA UTEPE KUHASHIRIA KUFUNGUZI RASMI WA KANISA HILO LA FPCT

MTOTO FARAJA MUSA MWANAFUNZI WA SHULE YA AWALI KILOLENI AKISHEREHESHA UFUNGUZI WA KANISA HILO


WAUMINI WA KANISA HILO WAKIWA KATIKA MISA MAALUMU KWA AJILI YA UFUNGUZI RASMI WA KANISA HILO



Na Lucas Raphael,Tabora

KANISA la Free Pentecostal Church Tanzania (FPCT) limelaani vikali vitendo vionavyofanywa na baadhi ya watu kuwakata mikono walemavu wa ngozi Albino kwa imani za kishirikina.

Kauli hiyo ilitolewa  na Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa hilo nchini Wilson Lazaro kwenye sherehe za uzinduzi wa Kanisa la FPCT Palishi ya Kiloleni mjini Tabora.

Akizungumza katika uzinduzi huo Askofu Lazaro alisema vitendo vinaendelea kufanywa na watu kuamua kukata mikono ya mlemavu kwa tama ya kupata utajili wa haraka havina budi kulaaniwa na watu wote.

Askofu Lazaro aliiomba Serikali kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwanyima dhamana watu wanaofikishwa katika vyombo vya sheria kwa tuhuma za kuwafanyia ukatili watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, lengo nikudhibiti matukio kama hayo yasiendelee kutokea katika jamii.

“Wewe kama huna fedha za kuendesha maisha yako hapa duniani nenda shamba ukalime sio kuamua kumkata mwenzako mikono eti tu umedanganywa na mganga wako wa kienyeji” alisema Askofu Lazaro

Kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya, Askofu huyo aliwaomba watanzania kuliombea kwa Mungu bunge la kutunga katiba, ili liweze kutunga katiba ambayo  itaweza kukidhi mahitaji, majawabu na matarajio ya watanzania wote.

Aliwataka wajumbe wa bunge la katiba kuweka pembeni tofauti zao za kiitikadi ya vyama vyao ili waeze kujadili kifungu kwa kifungu, ukurasa kwa ukurasa na hatimaye siku ya mwisho waweze kuwaletea watanzania katiba bora inayolenga kuinua uchumi wa kila mtanzania.

Katika sherehe hizo za uzinduzi wa kanisa hilo, pia uliambatana shughuli za kusimikwa kwa mchungaji kiongozi wa Kanisa la FPCT Kiloleni Peter Shani ambaye ndiye atakuwa mchungaji mkuu wa kanisa la mahali pale.

Mwisho




WAKULIMA WAWAFYEKA MIGUU NG'OMBE 14 KULIPA KISASI KWA WAFUGAJI-KIGOMA

 
Na Magreth Magosso,Kigoma

IMEELEZWA kuwa,ng`ombe 14 wapo hatarini kupoteza uhai,baada  ya kukatwa miguu yote minne na jamii ya wakulima wa Kijiji cha mgambazi kata ya Igalula wilaya ya uvinza mkoani hapa.huku viongozi 11 wa chama cha Chadema walala lupango.

Hali hiyo inachangiwa na mgogoro uliopo baina ya  kundi la wafugaji wa kisukuma kukaidi kwenda kuishi kwenye maeneo yaliyotengwa kwa malisho katika kijiji hicho ,ili kuondoa mgogoro wa mifugo hiyo kutoendelea  kuharibu  mashamba ya wakulima.

Pia  changamoto hiyo,imepelekea diwani wa kijiji cha mgambazi Abel Chiza(chadema) na mtendaji wa kijiji hicho kuswekwa mahabusu kwa siku nne ili kutoa ufafanuzi juu ya jeuri  inayofanywa na wafugaji  kugoma kuhamisha mifugo katika maeneo ya wakulima na kuathiri  uhai wa ng`ombe hao.

Akizungumzia  hilo  Katibu  Mkuu wa chama cha chadema Mkoani hapa Shaban Madede  alisema,alipewa taarifa na wananchi wa kijiji hicho kuwa viongozi wa chama cha Chadema watiwa nguvuni kutokana na mgogoro mkubwa wa wakulima na wafugaji .

“leo ng`ombe 200 zimeingia kinyemela bila idhini ya kijiji ,wakulima wanawafukuza ,mkurugenzi aliwapa siku 14 wafugaji wakaishi katika maeneo yao lakini hawataki mkuu wa mkoa na katibu tawala wawajibike waache siasa” alisema Madede.

Jamboleo likazungumza na Kamanda wa Polisi wa hapa Jaffar Mohamed  juu ya hilo alisema  watu saba wapo mahabusu ambapo wakulima watatu na wafugaji wane kwa upande wa wafugaji wamekiuka sheria na taratibu za mazingira kwa kupeleka mifugo  maeneo yenye vyanzo vya maji na kwa upande wa wakulima wamehukumu mifugo kinyuume cha sheria na taratibu husika.

Mohamed alisema,hawajakamata viongozi wa chadema ila waliokiuka sheria na hilo lilipelekea kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo  kuweka ulinzi kwa raia kwa kupeleka  askaripolisi  kutoa kituo cha kati na  uvinza  katika kijiji cha mgambazi kwa ajili ya kulinda usalama wa raia na mali zao .

Pia  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Nicholas Kombe kama  alitoa siku 14 wafugaji kuondoa mifugo katika maeneo ya wakulima , Kombe  akiri hilo na kudai shida  ipo kwa wafugaji kukiuka sheria,taratibu na kanuni za kijiji hicho na kusisitiza sheria izingatie uhalisia wa chanzo cha kukatwa miguu kwa ng`ombe hizo.

Kijiji kina mpango  bora wa ardhi katika kijiji cha mgambazi na Lukoma kata ya igalula  ambao ni mahususi kwa jamii ya wakulima na wafugaji kwa lengo la kuondoa mgogoro wa kuvamiana kulingana na shughuli zao.

Hivyo,kuswekwa mahabusu kwa diwani wa chadema na mtendaji wa kijiji ni moja ya hatua ya kubaini uihalisia wa mgogoro usioisha kwa wakazi hao,ambapo wao ni watendaji wakuu wa kijiji hicho na kudai uwepo wa askaripolisi kule ni kuimarisha ulinzi wa umma.

10 BORA YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) WAVAMIA STUDIO ZA TIMES FM 100 JIJINI DAR-ES-SALAAM


 

Waendeshaji wa Kipindi cha Filamu Monata kinachorushwa na Kituo cha Redio cha TIMES FM 100.5 wakiendelea na majukumu katika studio za kituo hiko cha Redio Kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam wakati wa Kipindi cha Filamu Monata leo wakati washiriki 10 Bora wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) walipotembelea Studio hizo 
Jaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) na Presenta wa Kipindi cha Filamu Monata cha TIMES FM, 100.5 Dar Es Salaam akiendelea na kipindi wakati washiriki 10 bora walipotembelea Kituo hiko leo kwaajili ya Mahojiano na waendeshaji wa Kipindi hiko.
 Mmoja wa Washiriki 10 Bora wa Tanzania Movie Talents (TMT) akijibu maswali kutoka kwa Waendeshaji wa Kipindi cha Filamu Monata kinachorushwa na Kituo cha Redio cha TIMES FM, 100.5 Dar Es Salaam.
Mshiriki Wa Tanzania Movie Talents (TMT) akijibu maswali.
 Washiriki 10 Bora wa Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa ndani ya Studio za TIMES FM, 100.5 Dar es Salaam.Picha Zote na Josephat Lukaza
Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kufanyika tarehe 30 August 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City kuanzia Saa 7.30 Usiku huku viingilio vikiwa Shilingi elfu 50 kwa VIP na Elfu 30 kwa kawaida
Burudani Kali kutolewa siku hiyo ya Fainali Huku Mc Pilipili akitoa burudani na Christian Bella

KAMPUNI YA VINYWAJI BARIDI YA SBC YAZINDUA MIRINDA MPYA AINA YA GREEN APPLE

 

Kinywaji cha mirinda Green Apple kikiwa katika chupa.
Maofisa wa Kampuni hiyo Godlisten Mende (kulia), na Omari Madaya wakionesha kinywaji hicho kwa waandishi wa habari.
Meneja Mauzo wa SBC, Godlisten Mende (kulia), akionesha kinywaji hicho kwa waandishi wa habari. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Meneja Mauzo wa Kanda, Omar Madaya (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kuzindua kinywaji hicho iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Meneja Mauzo wa SBC, Godlisten Mende (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakionja kinywaji hicho.
Mwanahabari huyu kama anasema “jamani mirinda hii ni tamu”.

Wanahabari wakichangamkia kinywaji hicho.
Wanahabari wakichukua taarifa kutoka kwa maofisa wa SBC.
Mmoja wa maofisa wa SBC (kushoto), akiwaelekeza jambo wenzake.


"CCM WAMKATAA KATIBU WA WILAYA YA TABORA MJINI,WAMEDAI ANAKIPELEKA CHAMA PABAYA"

 

Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bw.Idd Ame akitoka nje baada ya kuahirishwa kwa mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo wajumbe walianza kwa kumkataa Katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini  Bw.Bakari Mfaume na kushinikiza uongozi wa ngazi ya juu ya chama hicho kumhamisha katibu huyo ambaye walidai kuwa amekuwa chanzo cha migogoro ndani ya Chama. 
Pamoja na kuahirishwa kwa mkutano huo lakini wajumbe hao bado wameendelea kusisitiza kuwa hawatakuwa tayari kufanyakazi na Katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini ambaye tayari malalamiko ya wajumbe hao walishayafikisha kwa Katibu mkuu wa CCM Taifa Bw.Abdulrahman Kinana licha ya kuwa hadi sasa wajumbe hao  hawajaona mafanikio.Hata hivyo Chama cha mapinduzi wilaya ya Tabora mjini kimekuwa katika sekeseke la mvurugano wa wanachama na viongozi hali ambayo imeelezwa na baadhi ya wanaCCM imetokana na Katibu huyo kudaiwa kuwa anatumiwa na baadhi ya vigogo hasa kwenye maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 Na Mwandishi wetu 

Sakata la Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini kuendelea kumkataa Katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini bado linaendelea kuchukua kasi na hivyo kuanza kusikika hadharani baada ya wajumbe hao kutoka nje ya kikao cha kupokea utekelezaji wa ilani ya Chama hicho,mkutano uliowakutanisha wajumbe hao na timu ya wataalamu kutoka halmashauri ya manispaa ya Tabora.
Katika mkutano ulioanza majira ya saa nne na nusu ulifanyika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bw.Idd Ame,mara baada ya hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo wajumbe walinyoosha mikono na kudai kuwa hawamtaki Katibu wa CCM wilaya ya Tabora Bw.Bakari Mfaume kutokana na kukosa imani naye na hivyo kuhitaji aondolewe katika mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya wilaya ya Tabora.
Hata hivyo pamoja na Katibu wa CCM mkoa wa Tabora  Bw.Ame kuingilia kati na kujaribu kuwatuliza wajumbe kwa kuwafahamisha kuhusu lalamiko lao dhidi ya Katibu wa wilaya lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda kutokana na baadhi ya wajumbe kuanza kutoka nje ya kikao hicho.
"Tafadharini wanaCCM wenzangu suala la Katibu inaeleweka wazi kuwa linashughulikiwa na makao makuu kwahiyo sisi tuvute subira,tusubiri maamuzi ya Katibu mkuu Kinana,nawaombeni tuliache kwa muda ili tuendelee na kikao chetu hili lisituharibie mipango yetu jamani"alisisitiza Bw.Ame
Pamoja na rai hiyo ya Katibu wa mkoa Bw.Ame Wajumbe waliendelea kutoka nje ya kikao hicho mmoja baada ya mwingine licha ya kuwa baadaye kililazimika kuahirishwa kutokana na kutokuwepo kwa Meya wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij ambaye alikuwa kwenye ziara ya kichama jumuiya ya Wazazi mkoa wa Tabora.
Kufuatia kuendelea kuwepo kwa sakata hilo la wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini na baadhi ya wanachama wa chama hicho kumkataa Katibu wa wilaya ni wazi kwamba Chama cha Mapinduzi kimekwishaingia kwenye mgogoro ambao suluhisho la  msingi wake ni kuondolewa kwa Katibu huyo wa CCM wilaya ya Tabora Bw.Bakari Mfaume kama madai ya baadhi ya wanachama wa chama hicho wanavyoeleza.
''Sisi tunachojua Katibu huyu anatumiwa na viongozi wachache wenye pesa kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu,mpaka viongozi hao wamefikia kuwa wanachangishana wanamlipa mshahara mwingine nje ya mshahara anaolipwa na CCM,sasa tunasema hatumtaki,atuachie chama chetu,kwanza amekwishafanya madudu kwenye Wilaya karibu zote za Tabora,anakiharibu chama jamani"    
Aidha kwa upande mwingine baadhi ya Wazee wa Tabora mjini ambao hawakutaka kutajwa majina yao wameeleza kuwa endapo viongozi hawatakuwa makini kuhusu madai ya wajumbe na wanaccm kwa ujumla,kuna wasiwasi mkubwa wa kupoteza viti vingi vya serikali ya mtaa na pengine hata nafasi za udiwani na ubunge pia.
Hata hivyo kabla ya kuanza kwa mkutano huo Katibu huyo wa CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Mfaume aliwafukuza waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mkutano huo kwa madai kwamba yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuwaita waandishi endapo kama watahitajika na kuwatishia kuwa anaweza akawalalamikia kwa kuharibu mkutano huo jambo lililoleta tafsiri mbaya kwa waandishi wa habari na watu walioshuhudia kitendo hicho.
"Sasa huyu Katibu anataka kuficha nini wakati hiyo taarifa itakayosomwa kwa wajumbe wa halmas  hauri kuu inatakiwa wananchi wajue nini Serikali yao imefanya,au ana ajenda za siri?baadhi ya watu waliokuwa nje ya ukumbi huo walisikika wakihoji uhalali wa Katibu huyo Bw.Mfaume kuwafukuza waandishi wa habari eneo la mkutano huo.