Tuesday, February 11, 2014

CHADEMA YAITUHUMU CCM KUPANGA KUVURUGA UCHAGUZI KILOLO


scaled1 1dad5
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepeleka malalamiko Jeshi la polisi mkoa wa Iringa juu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupanga kuvuruga uchaguzi wa udiwani kata za Ibumu na Ukumbi wilayani Kilolo.

Mwenyekiti wa CHADEMA nyanda za juu kusini, Dkt. Stephen Kimondo anasema wamepata taarifa kuwa CCM kati ya Februari 5 na 6 imepeleka walinzi wake (Green Guard) 50 kwenye kata hizo, 10 kata ya Ibumu wakiongozwa na Ali Simba na 40 kata ya Ukumbi.


Anaongeza kuwa wanafahamu kuwa kazi ya walinzi hao inayofanyika ni kupiga na kutesa wanachama wa CHADEMA lengo likiwa ni kuvuruga uchaguzi unaofanyika leo.

Katika barua yao kwa jeshi la polisi ambayo Mwananchi imepata nakala yake, inatahadharisha kuwa kama jeshi la polisi halitachukua hatua kuzuia walinzi hao wasifanye chochote hali hiyo inaweza kuhatarisha amani na kuwa iwapo jeshi halitachukua hatua za kuhakikisha usalama basi wanachama wao wataamua kujilinda wao wenyewe dhidi ya walinzi wa CCM jambo ambalo litavunja amani katika maeneo hayo.


Kwa mujibu wa jeshi la polisi Iringa CCM na CHADEMA wanatuhumiana kila mmoja kupeleka walinzi wake katika kata zinazofanya uchaguzi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi anasema wamepata taarifa hiyo na nyingine kutoka CCM wakidai CHADEMA kupeleka Red Brigade na kuwa hiyo ni joto la uchaguzi.


Anaongeza kuwa kazi ya kulinda usalama si ya red brigade wala green guard kama vyama vinavyofanya, ni ya jeshi la polisi na wanafanya hivyo.
 

Anasema hali ya usalama kwa vituo vyote ni nzuri ambapo kila kituo kitakuwa na askari, watu wajitokeza kupiga kura kwa amani.


Kumekuwepo na vurugu katika Kampeni za uchaguzi wa marudio wa udiwani katika kata tatu mkoani Iringa ikiwemo ya Nduli ambapo Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa alifikishwa mahakamani akituhumiwa kujeruhi kada wa CCM.  

Chanzo: Hakimu Mwafongo

CCM TABORA MJINI WAZIBUA MITARO YA MAJI MACHAFU HOSPITALI YA KITETE


Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Tabora mjini Bw.Moshi Nkonkota(kushoto) akifanya usafi wa mazingira katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya 37 ya Chama hicho.
Mjumbe wa NEC Bw.John Mchele akifukua mitaro ya maji machafu iliyoziba katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete.
Katibu wa siasa na Uenezi CCM Tabora mjini Bw.Rashid Ramadhani Maarufu KAMANDA TOLU akipiga jembe kufukua mitaro hiyo inayoizunguuka hospitali ya Kitete ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM nchini.
Baadhi ya viongozi wa kata wa CCM ambao walihudhuria katika tukio hilo la kufanya usafi wa mazingira hospitali ya Kitete.

"MAMA ASHAURIWA AMPE SUMU MTOTO WAKE MLEMAVU,AKAA NDANI KWA ZAIDI YA MIAKA KUMI NA MOJA"


Mtoto Tatu Hassan akiwa na mama yake mzazi Bi.Halima Mgelwa,mtoto huyu amekuwa kitandani kwa zaidi ya miaka kumi na moja kutokana na maradhi ya kichwa huko katika kijiji cha Magiri wilayani Uyui mkoani Tabora. 
Mama wa mtoto huyu anaomba msaada wa matibabu kwa wasamalia wema,tatizo kubwa kichwa cha mtoto huyu kimejaa maji na hivyo anahitajika kupelekwa hospitali ya Bungando jijini Mwanza.
Mama huyu kwa mujibu wa maelezo yake amekuwa akilazimika kumfungia ndani ya nyumba kila siku na kwenda kutafuta riziki kwa muda wote huo wa miaka kumi na moja na hivyo hata baadhi ya majirani zake wa karibu hawatambui kama kuna mtoto huyu hapo kijijini.Jambo baya zaidi baadhi ya watu wenye imani  potofu walithubutu kumshawishi mama huyu aweze kumpa SUMU mtoto wake eti kwa madai kwamba amekuwa akihangaika sana kumuhudumia.