Thursday, May 29, 2014

KAMPUNI YA UNUNUZI YA ALLIENCES ONE YATOA MSAADA WA MAWADAWATI



NA LUCAS RAPHAEL
AFISA MAHUSIANO WA KAMPUNI YA ALLIENCES ONE HAMIS LIANA AKIONGEA NA WALIMU NA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA MADAHA WILAYA YA UYUI WAKATI AKIKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 75

AFISA MAHUSIANO HAMIS LIANA AKIMKABIDHI MWENYEKII WA HALMASHAURI YA WILAYA YA UYUI SAID NTAHONDI MADAWATI 75 YALIYOTOLEWA NA KAMAPUNI YA UNNUZI WA TUMBAKU MKOANI HAPA YA ALLIENCES ONE KWENYE  SHULE YA MSINGI YA MADAHA KIJIJI CHA MPENGE WILAYA YA UYUI


BAADHI YA WANANFUNZI WA SHULE YA MSINGI MADAHA KATIKA KIJIJI CHA MPENGE KATA YA ILOLANGULU WAKISIKILIZA WAGENI WALIOFIKA KUTOA MSAADA WA MADAWATI KWA AJILI YA KUPUNGUZA UHABA WA MADAWATI KATIKA SHULE HIYO

Kampuni ya ununuzi wa tumbaku ya Allience One imetoa msaada wa madawati 75 yenye thamani ya shilingi milioni 4,875,000/= katika shule ya msingi Madaha iliyopo katika kijiji cha Mpenge kata ya Ilolangulu wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora.

Akikabidhi msaada huo Afisa mahusiano wa kampuni hiyo Hamis Liana amesema msaada huo wa madawati utasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Alisema msaada huo wa madawati uwe chachu kwa walimu kuongeza juhudi za kufundisha na wazazi kujikita zaidi katika shughuli za kilimo kwa kuwa wamepunguziwa mzigo wa kuchangia ununuzi wa madawati katika shule hiyo.

Liana alibainisha kuwa kampuni ya Allience one imejiwekea mkakati wa kuchangia katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na sekta ya elimu kwa kutoa madawati na vitabu.

Afisa huyo mahusiano alisema kampuni yake imekuwa ikichangia katika miradi hiyo katika maeneo ambayo wananunua tumbaku kupitia vyama vya msingi vya ushirika ambavyo vinaiuzia tumbaku kampuni hiyo.

“Wakulima kupitia vyama vya msingi wamekuwa wakionesha jitihada za kuwauzia tumbaku, hivyo nasi tunalazimika kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo yao”. Alisema Liana.

Akipokea msaada huo Mwalimu mkuu wa shule hiyo Catherine Mmbando alisema anashukuru kwa kupata msaada huo wa madawati kwani umeondoa tatizo la upungufu wa madawati katika shule hiyo.

Alisema kuwa shule hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 71 lakini kampuni hiyo imefanikiwa kuwapatia madawati 75 ikiwa ni zaidi ya asilimia 100 ya mahitaji ya shule.

Mwalimu huyo alisema shule yake yenye jumla ya wanafunzi 391 na walimu 13 kwa pamoja watahakikisha wanatumia madawati hayo kwa uangalifu ili yaendelee kuleta tija kitaaluma shuleni hapo.

MWISHO

Monday, May 12, 2014

SHEREHE YA KUWATUNUKU SHAHADA YA UDAKIRI WA FALSAFA PHD DKT SHANI NA MKEWE



Maaskofu wa kanisa la Evangelistc assemblies of God Tanzania(EAGT)kushoto Askofu Dkt,Ebison Katongo wa Zambia akifuatiwa na Dkt,Timoth Kasembe wa kutoka Lusaka Zambia watatu kushoto ni Askofu Dkt,Emmanueli Shani na mkewe Hosana Shani na Dkt,Stephan Nzowa baada ya kumutunuku udakitari wa Falsafa  ya PHD,Mei 11 mwaka huu katika kanisa hilo mjini Nzega

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUJIENDELEZA KI ELIMU





 NA LUCAS RAPHAEL,NZEGA

VIONGOZI WA Dini  mbalimbali  hapa nchini wametakiwa  kujiendeleza kiEleimu  wasilizike  na Elimu waliyo nayo kutokana na mabadiliko ya kisayansi na Teknolojia nayo jitokeza hivi sasa katika Nyanja mbalimbali za kijamii ikiwa na kiu Tamaduni.

Kauli hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Eangelistic Assemblis of God Tanzania(EAGT) Stephano Nzowa  wakati wa sherehe za  Kuwatunuku Udakitari wa Falisafa PHD  Askofu Emmanuel  Shani na mkwe Hosena Chales katika Viwanja vya kanisa hilo wilayani Nzega Mkoani Tabora.

Amepata PHD  hiyo katika Chuo Kikuu cha Africas  Graduate University  kutoka  Nchini   Senegal  na  Bregedia General Dk,Timothy  Kasembe  mbele ya  waumini wa kanisa hilo.

Dk,Nzowa alisema kuwa  Elimu ni Bahari pana  ambayo inapaswa kila mtu kuogerea humo kwani  bila Elimu hakuna maisha hivyo kila nyakati yapaswa kupata nafasi ya kujifunza kwa bidiii.

Askofu Nzowa alisema viongozi wa makini hususani wachungaji na maafisko wanapaswa kusomea Elimu mbalimbali ikiwemo ya kidini ili waweze kukabiliana na mabadiliko  ya kisanyans na Teknolojia katika jamii mbalimbali.

Alisema kuwa Viongozi wa Dini wakisoma wataweza kubadilisha Jamii inayo wazunguka kupitia Elimu hiyo na kuongeza kuwa jamii imebadilika kwa kias kikubwa tofauti na hapo zamani.

Alisema kuwa suala la Elimu limeelezwa katika vitabu vya mungu kwa nyamba mbalimbali hivyo Viongozi wa kidini wanapaswa kuyatenda hayo iliwaweze kufikia malengo kwa Nyanja mbalimbali kadri uwe zavyo.

Dk,Askofu Mkuu wa kanisa hilo Stephan Nzowa aliwataka Vijana kuiishika Elimu kama walishikavyo neon la Mungu iliwaweze kufikia malengo yao ya kimaisha ikiwa na kufanya mambo mema kwa jamii inayo wazunguka.

Alisema kuwa jamii ya watu waliosoma hufanya matendo mema kwa wananchi ikiwa na kuendeleza mema na kupinga mabaya kama maandiko yanavyo sema dhidi ya suala hilo la Elimu.

Mara baada ya kukabidhiwa Cheti cha udakitari wa Falisafa PHD Dk,Askofu Emmanueli Shani aliwataka wazazi na walezi kufanya juhudi kupeleka watoto shule ikiwa na kusimamia maendeleo ya wanafunzi iliwaweze kufikia malengo.

Akizungumzia mchakato wa kupata Elimu Dk,Emmanueli Shani  alisema kuwa suala la Elimu lina changamoto nyingi katika kufikia malengo na kuwataka wazazi na walezi kuvumilia changamoto hizo iliwaweze kufikia malengo husika.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo walisema kuwa Elimu nikitu muhimu katika maisha ya mwanadam hivyo wananchi na jamii kwa ujumla inapaswa kujikita katika kuendana na mazingira husika ili kuweza kuleta mabadiliko makubwa.

Alisema kuwa Elimu ya sasa ni ile ya chuo kikuu na vyuo mbalimbali ikiwa na kusomea fani furani ambayo itaweza kukutoa sehem moja hadi kukufikisha sehemu nyingine ya kimaisha ikiwa na kuisaidia jamii husika.

Mwisho.

"BASHE ANG'ARA ZIARA YA KINANA WILAYANI NZEGA,WATU WAMSHANGILIA KILA ANAPOTAJWA"

20Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw. Abdulrahman Kinana akimpongeza mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Bw. Hussein Bashe mara baada ya kukabidhi kwa viongozi wa kata  pikipiki kwa ajili ya watendaji wa chama cha Mapinduzi.
Katibu mkuu wa CCM Bw.Abdulrahman Kinana akimsikiliza Kada wa CCM Bw.Hussein Bashe wakati akitamka na kutoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya kata mojawapo huko wilayani Nzega ambapo Bw.Kinana alifanya ziara ya siku mbili kwa ajili ya kuangalia uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa wananchi.
KIAPO
Kada wa Chama cha Mapinduzi Bw.Hussein Bashe akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kampala iliyopo wilayani Nzega,ambapo wanafunzi hao walionesha kumshangilia sana kwa kile kinachodaiwa kuwa Bashe amekuwa karibu sana na Shule hiyo katika kukabiliana na Changamoto za elimu kwa wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na kutoa misaada mbalimbali.
10 Mbunge wa jimbo la Nzega Mh. Khamis Kigwangala akimpongeza Mjumbe wa mkutano mkuuu wa CCM Bw. Hussein Bashe mara baada ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Nkiniziwa, katikati ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.

"MUNDE ANAFAA KUCHAGULIWA,KWAKUWA YUPO KARIBU SANA NA WATU"-KINANA


Katibu mkuu wa CCM Bw.Abdulrahman Kinana na mbunge wa vitimaalum mkoa wa Tabora Bi.Munde Tambwe wakiweka mchanga kwenye mashine ya kufyatulia tofali za Saruji katika Mradi wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM wilayani Nzega ambapo Mradi huo unafadhiliwa na Bi.Munde kwa thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15.
Katibu mkuu wa CCM Bw.Abdulrahman Kinana akikata utepe ikiwa ni Ishara ya kufungua Mradi  wa kufyatua matofali wa Jumuiya ya UWT wilaya ya Nzega wakati wa ziara yake wilayani humo,ambapo mfadhili mkuu wa mradi huo ni Bi.Munde Tambwe.

KINANA AFUNIKA NZEGA,BASHE NA KIGWANGALLA WACHUANA KUTOA MISAADA MBELE YAKE

unnamed
unnamed (1)
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa wilaya ya Nzega kwenye mkutano uliofanyika Nzega mjini na kuwaambia wananchi hao kuwa wasisumbuke na wapinzani kwani wapinzani hawapo kwa ajili ya maslahi ya maendeleo ya wananchi.
unnamed (2)
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akifafanua masuala mbali mbali yanayohusu wachimbaji wadogo wa wilaya hiyo kwenye mkutano wa hadhara ambao uliongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
unnamed (3)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma moja ya mabango aliokabidhiwa na wachimbaji madini wadogo wa Nzega wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Nzega mjini,wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Bukene Ndugu Sulemani Zedi na Mbunge wa Jimbo la Nzega Dk.Hamisi Kigwangalla.
unnamed (4)
Baadhi ya Wachimbaji madini wadogo walikifuatilia kwa makini hotuba za viongozi  kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Nzega mjini.
unnamed (5)
Mbunge wa Jimbo la Nzega Dk.Hamisi Kigwangalla akihutubia wananchi wa Nzega  kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Nzega ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mbunge wa Nzega aliwaambia wananchi jimbo lake kuwa  viongozi wanapaswa kuwajibika kwa wananchi.
unnamed (6)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono wa pongezi kwa mbunge wa jimbo la Nzega Dk. Hamisi Kigwangalla kwa kutoa mashine ya kutotolea vifaranga wa kikundi cha vijana jimboni hapo.
unnamed (7)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli kwa viongozi wa kata ambapo zaidi ya baiskeli 163 kwa makatibu wa matawi yote na 36 kwa makatibu wa vijana ngazi ya kata na pikipiki tatu kwa Jumuiya ngazi ya wilaya ambazo zimetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa wilaya ya Nzega Ndugu Hussein Bashe.
unnamed (8)
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga ngoma wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye viwanja vya mikutano vya Ndala.
unnamed (9)
Mbunge wa jimbo la Nzega Dk.Hamisi Kigwangalla akihutubia wakazi wa kata ya Ndala kwenye mkutano wa hadhara wa CCM ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana yupo Nzega kwa ziara ya siku mbili ambapo atashiriki shughuli za kimaendeleo na kukagua uhai wa chama.
unnamed (10)
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora Mhe. Munde Tambwe akiwasalimia wakazi wa Ndala wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM.
unnamed (11)
Maabara ya shule ya sekondari Kampala ikiwa imekamilika kabisa, shule hii ni moja ya shule za kata zilizpo wilayani Nzega.
unnamed (12)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya namna vifaa vya maabara vinavyotumika kutoka kwa Mwanafunzi Amos Kashindi ,wengine pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa.Katibu Mkuu wa CCM alitembelea maabara hiyo iliyopo kwenye shule ya sekondari Kampala iliyopo kata ya Ndala ambayo imekamilika ,Serikali imeahidi kujenga maabara katika shule zote za Kata.

Thursday, May 8, 2014

RAGE AZOMEWA MBELE YA JANUARI MAKAMBA,KISA MJADALA WA KATIBA KUINGIZA LIGI YAKE BINAFSI

Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Mheshimiwa Ismail Aden Rage akizungumza katika kongamano la Katiba lililohusisha wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Tabora.
Naibu waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Bw.Januari Makamba akisikiliza namna ambavyo wanafunzi wa vyuo vikuu walivyokuwa wakimzomea mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Mheshimiwa Ismail Rage.
Wanafunzi vyuo vikuu Tabora mjini
Na Lucas Raphael Tabora



Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Aden Rage amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na wanafunzi wa Umoja wa Vyuo Vikuu mkoani Tabora.

Rage alipatwa na mkasa huo kwenye Kongamano la vijana kuhusu rasimu ya katiba lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mtakatifu August(SAUT)tawi la Tabora ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba.

Katika Kongamano hilo baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vya SAUT,THEOFILO KISANJI,CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA,MUSOMA UTALII NA TABORA NETWORK walianza kumzomea mbunge huyo baada ya kuwaeleza anataka kuanzisha Ligi ya mpira wa miguu RAGE CUP.

"Nataka nijitambulishe kwenu nafasi yangu nyingine mimi ni Mwenyekiti wa Simba pia nataka nianzishe mashindano ya Rage cup katika vyuo kumi na moja ili wapate timu ya mpira iliyo bora hapa kwetu,au mnasemaje vijana?...alisema Rage

Baada ya kusema hivyo tu ndipo aliamsha kelele kubwa kwa wanafunzi hao huku wakimtaka akae kimya na wengine wakimtaka aondoke ukumbini kwakuwa kikao hicho inasemekana Rage alidandia.

"Nenda kawaongoze Simba sisi hatukutaki,kwanza hapa tunaongelea masuala ya msingi ya Katiba sasa wewe unatuletea mambo ya mpira nenda bwana,kwanza hujui hata thamani ya maisha ya mtanzania,na tutaona wakati wa uchaguzi mkuu labda CCM wampange mtu mwingine lakini wewe tunauhakika watapoteza jimbo"walisikika wakisema hayo.

Hatua hiyo pia ilienda samabamba na kumweleza  mbunge huyo kuwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake ya kuwawakilisha wananchi bungeni ikiwa ni pamoja na kutokuwa na muda wa kusikiliza kero za wananchi akiwa jimboni kwake.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya alilazimika kuingilia kati sakata hilo lililokuwa likifanyika mbele ya Naibu waziri January Makamba ambapo aliwasihi wanafunzi hao kuto zomea juhudi ambazo ziligonga mwamba  hadi wanafunzi hao walipoacha wenyewe kwa kutulizwa na viongozi wao.

"Hivi mnavyofanya zomea zomea mimi nasema kama kiongozi wa Serikali si sahihi hata kidogo,mnatakiwa muwe wavumilivu na kusikiliza na kujenga hoja na siyo kuzomea" alisema kumchaya 

"Hata tukizomea wewe inakuhusu nini mbona Wabunge wanazome na wanalipwa laki tatu kwa siku bungeni,sisi tumeamua kuzomea bila malipo tatizo liko wapi mtu kujitolea bila malipo kukomesha uongo wa viongozi  wasio waadilifu"walisikika tena wakimjibu mkuu wa wilaya katika ukumbi huo.