Sunday, November 2, 2014

SAFARI YA MWISHO YA BEN KIKO


NA LUCAS RAPHAEL,TABORA


Safari ya mwisho wa mwandishi wa habari wa siku nyingi Hamis Bakari kikoroma maarufu kama Ben kiko (70) ilitimishwa jana katika kijiji cha ndaukilo kitogoji cha usupilo wilayani sikonge mkoani Tabora katika mazishi yaliohudhuriwa  na watu mbalimbali mkoani hapa.

Mazishi hayo yakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Tabora Sulemani Kumchaya kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa tabora Fatuma  mwassa naambapo aliwataka waahdishi wa habari hapa nchini  kuinga yale yote yaliomema aliyofanya mwandishi huyo mkongwe hapa nchini

Alisema kwamba kwamba waandishi wa habari na vijana kwa ujuma wake  wanatakiwa kuwa wazalendo kwa nchi yao kama alivufanya marehemu katika uhai wake kwa kutumikia nchi yake katika vita ya kagera na sehemu mbalimbali ambazo alifanya kazi kwa kujituma .

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kila mtu anatakiwa kujitoa kwa ajili ya nchi yake na sio kuweka maslahi  ubinafsi mbele kwani huo sio uzalendo bali kutoa kwa nchi kama alivufanya ben kiko wakati wa utendaji wake wakazi.

Alisema kwamba licha ya kufanya kazi tbc kwa vipindi tofauti tofauti bali alikuwa ni mfanyakazi katika Redio ya Tabora VOT na kuwa mwalimu wa waandishi wa habari katika mchuo cha musoma Utalii Tawi la Tabora  .

Marehemu amepata elimu shule ya msingi misheni sikonge kabla ya kwenda chabutwa kusoma elimu ya kati mwaka 1959-1962 shule ya wavulana tabora kidato nne kabla ya kuhudhuri mafunzo ya ualimu ya miaka miwili katika chuo cha ulimu mpwapwa mkoani Dodoma na kufanikiwa kupata cheti cha  ualimu daraja A.

Aidha mwaka 1984-1985 alikwenda nchini India kupata mafunzo ya uandishi wa habari ya ngazi ya Diploma .

Ben kiko hadi mauti yanamfika alikuwa mwenyekiti wa mtaa wa uhazili uliopo katika kata ya kanyenye manispaa ya Tabora  ameacha wajane watatu na watoto kumi.

MWILI WA MWANDISHI WA HABARI ZA SIKU NYINGI BEN KIKO UKIINGIZWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE .
SHEKHE SALUM MAHARUKI AKIONGOZA SALA YA KUUONBEA   MWIILI WA MWANDISHI WA SIKU NYINGI NCHI HABARI BEN KIKO  NJE YA NYUMBANI YAKE KATIKA KIJIJI CHA USUPILO WILAYA YA SIKONGE MKOANI HAPA
WANANCHI KUTOKA TABORA MJINI NA WALE WA WILAYA YA SIKONGE WAKIWA KATIKA MKUSANYIKO WA KUKAMILISHA SAFARI WA BEN KIKO


Add caption