Ramani inayoonyesha
ulipo Mto Igombe ambao ni tuzo ya
“Kilimo Kwanza” mkoani Tabora
1.0
Utangulizi
Katika
kikao cha Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kilichofanyika tarehe 8 Novemba 2013,
Mkuu wa Wilaya alimkabidhi Mwenye Kiti barua kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya
serikali za mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ikiwataarifu wana
Kaliua, kupitia Halmashauri yao, kuwa Serikali imeridhia maombi ya Kamati ya
Siasa ya Chama cha Mapiduzi, CCM Kaliua,
yaliyo wakilishwa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu
na Mwenye Kiti wa CCM, kuomba
wilaya yake ihamishiwe Mkoa mpya wa Katavi. Madiwani wengi walishangazwa na
taarifa iliyokuwa ikielezwa na barua hiyo, kwa vile hawakuwa na taarifa ya maamuzi ya
kikao chochote cha Halmashauri yao mpya ya Kaliua au hata ya halmashauri ya
Wilaya ya Urambo walikokuwa, kupitisha
uamuzi wa Wilaya ya Kaliua kuhamishiwa Katavi. Hata hivyo Mwenye Kiti, John Kadutu, akiungwa mkono na madiwani,
aliyapokea maagizo ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya kutaka kulifikisha suali hili
kwenye kamati za maendeleo za kata, ili kupitia kamati hizo, wananchi wapate
nafasi ya kulijadili suala zima la kuhamia Katavi na kulikubali au kulikataa.
Maoni na mapendekezo yoyote yatakayopatikana kutokana na vikao hivyo vya kata
ndiyo yatakayokuwa msingi sahihi wa mjadala wa Baraza la Madiwani, yaani
Halmashauri ya Kaliua na kamati zake.
2.0 Hoja ya Kuhamia Katavi
Kumekuwapo
na maelezo mbali mbali kuhusu suali la Wilaya ya Kaliua kuhamishiwa Mkoa wa
Katavi. Mheshimiwa Profesa Juma Kapuya,
Mbunge, ndiye kiongozi pekee ambaye amekuwa akilielezea jambo hili kwenye
majukwaa na kutangaza kuwa ni uamuzi wa Serikali unaopaswa kutekelezwa bila
kuchelewa. Inasemekana anaamini kufanya hivyo “kutaiwezesha wilaya ya Kaliua
kuharakisha maendeleo yake” . Anaamini
Katavi kuna maendeleo kuliko Tabora!
Wilaya
za Mkoa wa Tabora
3.0 Uchambuzi wa Hoja ya Mheshimiwa Kapuya
Haikuweza
kuelewaka mara moja nini maana ya hoja hii kwa vile kimsingi inajulikana maendeleo
yanahusu maisha mazuri ya jamii kuwa na chakula cha kutosha na lishe bora, afya
bora na usalama wa maisha yao na mali zao, miundo mbinu imara na mawasiliano ya
kisasa kupitia barabara, reli na kadhalika. Uhuru wa vyombo vya habari; utawala bora na uhuru wa wananchi
kushiriki katika maamuzi yanayohusu maisha yao, na kadhalika. Ingawa Serikali
ina nafasi kubwa katika kuwawekea wananchi wake mazingira mwafaka ya kuwezesha mambo haya yote yashamiri, bado ni jukumu la
wananchi wenyewe, mmoja mmoja na kama jamii, kuamua kujiletea maendeleo mahali
walipo. Watu wanapofikiria na kupanga mambo yao, Serikali kupitia wawakilishi
wake, (madiwani, wabunge, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na mashirika ya
dini) huona umuhimu wa kuwaletea misaada mbali mbali pamoja na fedha, maji ya
bomba, hospitali kubwa na madaktari bingwa, shule na vyuo, viwanda, na
kadhalika. Maendeleo hayafuatwi nchi
nyingine au mkoa mwingine.
4.0 Hoja za Kubaki Mkoa wa Tabora.
4.1
Historia
Hoja
ya kufikiriwa kwanza ni ile ya kihistoria. Wilaya ya Kaliua, hususani tarafa ya Ulyankulu , ndiyo chimbuko
la Wanyamwezi. M ji wa Tabora una
historia ndefu – biashara ya utumwa na utawala wa waarabu, utawala wa
Wajeremani na Waingereza, uanzilishi wa Chama ca TANU, na kadhalika. Yote
haya yameifanya Serikali ya awamu ya nne
iheshimu nafasi ya Mkoa waTabora katika utamaduni wa nchi mpaka ikaweka
makumbusho ya Mtemi Miranbo kule Uyankulu. Hivyo kuipekleka Ulyankulu Katavi ni
kuupunguzia hadhi Mkoa wa Tabora bila sababu ya msingi.
4.2
Barabara ya Kigoma
Kwa
vile sasa kuna barabara kuu itokayo Tabora kwenda Kigoma, mawasiliano kati ya
Wilaya ya Kaliua na Mkao makuu ya mkoa, yaani mji wa Tabora, yatakuwa mazuri zaidi.
Kwa upande wa tarafa ya Ulyankulu, sasa hivi si rahisi kusafiri kutoka
baadhi ya kata za Ulyankulu kwenda Kaliua – barabara si nzuri. Inawapasa
watendaji kutoka Mwongozo[1],
kwa nfano, kupitia Tabora mjini (Tazama
kielelezo cha raani ukurasa wa 5) ili kupata usafiri wa haraka wa kuwafikisha
wilayani Kaliua. Hivyo umbali ni kigezo kimojawapo tunachopaswa kukizingatia
tunapotaka kuwahudumia wananchi wa sehemu yeyote kwa karibu zaidi.
4.3 Kilimo Endelevu
Wilayani Kaliua
Wilaya ya Kaliua ina ardhi nzuri, mito na mabonde [2]
yanayofaa kwa kilimo cha umwagilizaji. Uendelezaji wa kilimo hicho katika mabonde haya utahitaji juhudi za mkoa wenye
uzoefu, kama Mkoa wa Tabora. Wilaya ya Kaliua ikihamia Katavi ittachelewa
kupanga maendeleo yake; sio kuyaharakuisha,
kwa vile mkoa mpya bado unandaa mikakati yake ya maendeleo kabla
haujaanza kuitekeleza.
Rmani inayoonyesha jinsi
wilaya za Kaliua na Urambo Mashariki zinavyowiana na wilaya zingine za Mkoa wa Tabora kijografia
4.4 Mradi wa Mto Igombe
Tarafa ya Ulyankulu ina mipango ya kushirikiana
na wawekezaji siku zijazo kuendeleza matumizi ya mto Igombe. Mto huu unapita
katikati ya Ulyankulu na sehemu kubwa ya tarafa Uyowa, ukianzia sehemu za Uyui
na Itaga karibu na mji wa Tabora. Serikali kupitia Wizara ya Maji,
walipotengeneza bwawa la maji kwenye chanzo cha mto huu (Tabora Igombe Dam), walibadilisha
mtiririko wa maji ya mto huu. Maji sasa mengi yanabaki kwenye bwawa. Maji kiasi
tu ndio yanaenda ndani ya mto.
Walipokuwa wakijenga bwawa la kupeleka maji
Tabora Mjini, walipaswa pia kujenga
bwawa la kina kidogo (gravity dam Tazama mchoro wa kushoto hapo juu) kilometa
100 hivi magharibi mwa Mto Igombe, kama reservoir (hifadhi ya maji ya mto). Kwa
kufanya hivyo matumizi ya mto huu kwa watu wa Ulyankulu na Uyowa yangeendelea
kuwapo. Hii ingewezesha maji kuendelea kuwapo muda wote.
Matokeo
ya makosa yaliyofanyika Tabora yamekuwa mabaya kwa Ulyankulu na Uyowa: Hakuna
tena samaki wanaovuliwa kwenye mto huu, kwa vile maji sasa yanabaki Tabora Dam!
Hata wale viboko na wanyama wengine wanaopatikana kwenye maji sasa wametoweka.
Utekelezaji
wa mradi huu unaweza kufanyika kwa ufanisi mkubwa zaidi Wilaya ya Kaliua
akishirikiana kwa karibu zaidi na mdau mkubwa wa maji ya Mto Igombe, ambaye ni Mji wa Tabora.
5.0 Sheria na Utaratibu wa Kuihamisha Wilaya
Kaliua
Umekuwako uvumi na minong’ono kuwa wazo la
kuhamia Katavi limeletwa na mbunge Profesa Juma Kapuya, ambaye amekuwa
akilieleza kila apatapo wasaa wakufanya hivyo. Wananchi wamekuwa
wakijiuliza kwa nini Mheshimiwa Profesa Juma
Kapuya amelivalia njuga jambo hili? Je, ana masilahi gani nalo?
Si vizuri kuamini maneno
yanayosemwa semwa na watu jimboni kwa mbunge huyu; lakini pia si vizuri pia
kuyafumbia macho, kwa vile wananchi ndio wapiga kura na wachaguzi wa mwisho.
Kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, ibara ya 8, kifungu kidogo cha (1) (b) hadi kile
cha (c), vinasema “wananchi ndio msingi
wa mamlaka yote ya Serikali; na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba
hii.” Kifungu (b) ”Lengo kuu la Serikal
litakuwa ni ustawi wa wananchi. (c)
Serikali itawajibika kwa wananchi wake na (d) wananchi watashiriki katika
shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.” Hivyo tangu
mwanzo Mbunge Kapuya angekuwa amepata ridhaa ya wananchi kwanza baada ya kuwashirikisha,
kuwaelimisha na kuwashawishi kwa semina na vikao halali katika ngazi ya kata,
kama inavyoagiza Ofisi ya Waziri Mkuu sasa.
Katika suala hili zima la
wilaya ya Kaliua kuhamia mkoa wa Katavi,
bado kuna masuali mengi yanayohitaji maelezo:
·
Ombi la kamati ya siasa ya Chama Tawala CCM,
lilipelekwa Serikalini na Mwenye Kiti wa
CCM kwa misingi gani?
·
Kikao cha
kamati hiyo hakikuwashirikisha wajumbe wa Halmashauri ya Kaliua. Kikao hicho kilikaa lini na kwa kanuni au
sheria ipi?
·
Kikao hicho kilipata mamlaka ya kuwasilisha ombi
Serikalini kwa mujibu wa kanuni au
sheria gani?
·
Makadirio ya asilimia 80 ya wananchi wa Kaliua
wanaopendelea wilaya yao ihamie Katavi
yalipatikana vipi?
6.0 Matarajio ya
Wilaya ya Kaliua Ikibaki Tabora
Wilaya ya
Kaliua, hususani tarafa ya Ulyankulu, imejiwekea malengo mbali mbali ya
kimaendeleo, ambayo utekelezaji wake utategemea ushirikiano uliojengwa mkoani
Tabora. Muhimu katika miradi ya
maendeleo ni pamoja na hii:-
·
Kuendeleza kilimo, hususani
kilimo cha umwagiliaji, kwa kitumia mto
Igombe, ili kuongeza uzalishaji wa chakula. Chakula cha ziada kitauzwa nje ya wilaya yetu ya Kaliua..
·
Kujenga barabara za taarafa
zote za Wilaya ya Kaliua, hususani barabara
zinazoziunganisha kata na tarafa za Kaliua na makao makuu ya mkoa,Tabora, na wilaya
jirani za Kahama, Urambo, Uyui.
·
Kuboresha huduma ya afya kwa
wakaazi wa Wilaya ya Kaliua, hasa afya ya akina mama wazazi na watoto, kwa mujibu
wa yale Malengo manane ya Milenia. Mkazo
utakuwa kupunguza au kutokomeza magonjwa ya kuambukiza, hususani malaria,
ukimwi, na kifua kikuu.
·
Kuboresha miundo mbinu ya
mawasiliano, yaani mawasiliano ya simu, radio, tv, na magazeti.
·
Kuendeleza miradi ya kuchimba
visima ili kuwapatia wananchi maji safi
na ya uhakika. Wilayani Kaliua hakuna mipango-majiendelevu inayo weza kuleta maji
muda wote hata kiangazi
·
Kuunda vikundi vya ushiriki ikiwa ni pamoja na Saccos, Vicoba na
vyama vya ushirika wa mazao ya biashara, hususani tumbaku na pamba.
Mipango ya matarajio haya yanaendana na mipango ya Mkoa wa
Tabora; hivyo utekelezaji wake utazorota Wilaya ya Kaliua ikihamishiwa Tabora
sasa.
7.0 Angalizo
Yote haya yameelezwa vizuri kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Utekelezaji wake utachelewa Kaliua ikihamia Katavi. Wachunguzi wa siasa
wanatabiri kuwa Chama tawala CCM
kitapoteza imani ya wananchi wa Kaliua na wanachama wake kikiwalazimisha
kuhamia Katavi kwa shinikizo la mbunge wa sasa Mheshimiwa Profesa Juma Kapuya. Wanachama
wa CCM na wananchi wa Wilaya ya Kaliua hawakubali suala hili liwagawanye: wanao
taka kuhamia Katavi nawanaotaka kubaki Mkoani Tabora. CCM kitakosa kura muhimu ya wanaKaliua.