Sunday, December 29, 2013

MAFURIKO YAPIGA HODI TABORA MJINI,FAMILIA KADHAA ZAKOSA MAKAZI


Baadhi ya watoto ambao wanaishi katika nyumba zilizokumbwa na mafuriko eneo la Kata ya Malolo manispaa ya Tabora,watoto hawa walifanikiwa kuokolewa na hivyo wamelazimika kukaa nje ya nyumba zao wakisubiri maji yapungue. 

Mmoja kati ya akina mama wakazi wa Malolo akitafuta baadhi ya vyombo vya kupikia ambavyo vilisombwa na maji wakati wa mafuriko hayo ambayo yamesababisha baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamekosa makazi na kuhifadhiwa kwenye nyumba za jirani ambazo hazikukumbwa na mafuriko hayo yaliyoanza majira ya saa moja na nusu asubuhi kufuatia mvua za masika zinazoendelea kunyesha mjini Tabora.
Nyumba ya mchungaji wa kanisa la Injili Afrika  Elias Mbagata iliyoko kata ya Malolo manispaa ya Tabora nayo ilikuwa ni moja kati nyumba zilizokumbwa na adha hiyo.
Nyumba hizi zilikumbwa na mafuriko hayo.
Kamanda wa Polisi  wilaya ya Tabora mjini Bw.Samwel Mwampashe akiwa eneo la Mafuriko kata ya Malolo ambapo nyumba kadhaa zilikumbwa na mafuriko hayo lakini imeripotiwa kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha zaidi ya uharibifu wa vifaa na mali mbalimbali.
Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw.Suleiman Kumchaya,Mkurugenzi wa manispaa ya Tabora Bw.Alfred Luanda pamoja na Meya wa Manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij walifika kushuhudia mafuriko hayo yaliyotokea kata ya Malolo na kusababisha familia kadhaa kukosa mahali pa kuishi. 


No comments:

Post a Comment