NA LUCAS RAPHAEL TABORA
Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Tabora Christian Youth Network imetoa
wa maada wa vifaa vya shule kwa watoto waishio
katika mazingira hatarishi katika kata za kakola, Uyui na Gongoni katika wilaya
ya tabora .
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo ,Adriano Kalisti, alisema
kuwa kwa ufadhili wa shirika la kimarekani liitwalo SAVE AFRICAN’S CHILDREN
.
Alisema kwamba shirika hilo limekuwa
litoa huduma za vifaa vya shule kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi
kama vile madaftari na kalamu.
Alisema kwamba kutoa msaada wa
kisaikolojia kwa watoto waishio na virusi vya ukimwi na walioathiriwa wapato 75
na kuanzisha clubs maalumu zinazowakutanisha
watoto hao kila mwezi kwa ajili ya kupata elimu ya afya, kupata huduma za
kisaikolojia kwa kucheza michezo mbalimbali.
Alisema kuwamba changamoto mbalimbali wanazopitia kulingana na
hali zao pamoja na kupata chakula cha pamoja chenye lishe kwa ajili ya ujengaji
wa afya zao.
Kalist alisema kuwa wanakusudia kusaidia jumla ya watoto 500
katika kipindi cha miaka mitatu yaani 2013-2016 katika maeneo ya
kuwajengea walezi/wazazi wao kiuchumi, Afya, elimu, ulinzi na kutoa msaada wa
kisaikolojia.
Alisema mnamo mwezi January 2013 CYN
inajarajiwa kuendesha program maalumu ya kukusanya watoto zaidi ya 300 ili
luwashirikisha, upendo, Furaha kwa kula chakula cha pamoja, kucheza michezo
mbalimbali, kuwezesha watoto kutoa hisia zao kwa jamii juu ya matatizo
wanayopitia.
Alisema kuwa wanatarajia kuzindua
kampeni maalumu ijulikanayo kwa jina la “ HURUMIA WATOTO WAISHIO KATIKA
MAZINGIRA HATARISHI KATIKA ENEO LAKO, BEBA MZIGO” Kampeni hii imelenga
kuhamasisha jamii kuwa na moyo wa dhati/ mzigo wa kusaidia watoto waishio
katika mazingira katarishi katika maeneo waishio bila kutegemea wahisani.
Alisema kwamba shirika la Christian
Youth Network inakaribisha wadau wengine kama vile makampuni na watu binafsi
katika kudhamini shughuli hii muhimu inayotarajiwa kufanyika Mwaka mpya 2014
katika tarehe za mwanzoni.
Mwisho
No comments:
Post a Comment