Hii sasa ina ashiria hatari kwa watoto kutumia muda mwingi katika kuperuzi picha za ngono kwenye mtandao.
Kwa mara ya kwanza nilipokuwa
nikifika kwenye Internet Cafe ili niweze kuangalia mambo mbalimbali
yaliyojiri ulimwenguni,nilikuwa nikishuhudia watoto nao wanaingia na
kuomba muda wa kuperuzi kwenye mtandao kwa muhudumu kati ya dakika 30
hadi dakika 120.
Suala la kulipia muda huo kwa
watoto niliobahatika kuwaona haikuwa shida sana,na kila ninapowakuta
kwenye kompyuta wanakuwa bize sana hali iliyonilazimu nianze kuwafuatlia
na kutaka kujua nini wanafanya kwenye mitandao hiyo.
Wapo niliowakuta wakiangalia picha
za wachezaji wa mpira wa miguu na wasanii maarufu duniani,hilo
halikunipa shida kama lile la baadhi yao tena waliowengi walikuwa
wakitumia mitandao ya kijamii kama FACEBOOK.
Nilipojaribu kumuuliza mmoja
niliyekumbana nae,..hakuwa tayari kunijibu bali alikuwa kimya huku
akizidi kuangalia kile kilichomleta hapo kwenye Internet Cafe.
Kwakuwa jicho halina mpaka,na kwa
vile nimekaa kwenye kiti kilichopo jirani naye, nilijionea kitu ambacho
sikufikilia kama mtoto mdogo kama yule angeweza kutafuta mambo makubwa
kama hayo kupitia mtandao wa Google.
Ni picha za Ngono,tena chafu zisizosatahili hata kuangaliwa na mtu mzima tena mwenye akili timamu.
Pasipo shaka yoyote mtoto huyo aliendelea kujivinjali kwenye picha hizo zikiwemo za mnato na zile za video.
Jamani,jamani,jamani,......tena
kibaya zaidi nikamsikia vizuri akimlalamikia yule mhudumu wa Cafe
hiyo..."Dada mbona hii kompyuta haina sauti,...sasa mi ntaangaliaje
video za bila sauti?''alikuwa akisema mtoto huyo wakati akiangalia
kupitia Youtube huku akionesha kana kwamba ile ilikuwa haki yake ya
kimsingi ambayo hajatekelezewa.
No comments:
Post a Comment