Na Lucas Raphael,Tabora
BAADHI ya wananchi wilayani Nzega Mkoani Tabora
wamewalalamikia baadhi ya Askari polis wilayani hapa kwa kutumia nafasi
zao kuwa tendea kinyume na maadili ya kazi hiyo.
Wakizungumza na ukurasa huu kwanyakati tofauti
wilayani hapa wamesema kuwa baadhi ya Askari hao hutumia nafasi zao kwa kuwa
nyanyasa wananchi ikiwa na kuwa bambikizia makosa mbalimbali ambayo yapo
kinyume na sheria za hapa nchini.
Mkazi mmoja wa nzega mjini akizungumuzia mikasa ya
Askari hao kuwa baadhi yao hufanya makosa lakini raia akifanya kosa kama
alilofanya Askari huyo huchukuliwa sheria ikiwa na kubambikiziwa kesi
mbalimbali.
‘’mfano Askari anaendesha pikipiki bira kofia tena
kalewa Askari huyo akimuona raia anaendesha pikipiki bila kofia anamchukulia
hatua kari na kumbambikizia makosa je hapo ni haki? Nani awe mfano kwa
mwenzie’’alisema mkazi huyo jina lake limehifadhiwa.
Wameeleza kuwa kitendo hicho kinawafanya wananchi
hao kutokuwa na imani na baadhi ya Askari katika utendaji wao wa kazi.
Walisema kuwa baadhi ya Askari Polis wilayani hapa
wanafanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi hiyo hali ambayo mahusiano mema na
wananchi wanapata hasa katika suala la polis jamii na kuongeza kuwa Askari wa
polis jamii waweke mahusiano mema na wananchi ili kuweza kupata taarifa
mbalimbali za wahalifu.
Waliziomba taasisi husika wilayani hapa kufuatilia
suala hilo iliwananchi hao waendelee kuwa na imani na Askari hao pamoja na
kutiisheria za nchi.
Kaim kamanda wa polisi mkoa ambaye ni mkuu wa
upelelezi mkoa Edward Bukombe aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa ofisi ya
mkuu wa polis wilaya ili hatua kali zi chukuliwe dhidi ya Askari huyo.
‘’Askari Polis ni kioo cha jamii hivyo wanatakiwa
kufuata maadili yao ili raia afurahi na huduma hiyo paolis anapaswa kutii
sheria ili raia afuate polis wangu waache tabia hiyo vinginevyo sheria
itachukua nafasi yake’’alisema Mkuu wa upelelezi huyo.
Bukombe alisema kuwa Askari polisi atakaye bainika
anafanya kazi kinyume na maadili ya hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwa
na kufikishwa mahakamani.
Aliwataka Askari polisi mkoani hapa kufanya kazi
kwa kuzingatia maadili ya jeshi hilo pamoja na kuweka mahusiano bora na
wananchi ili kudumisha polis jamii.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment