BAADHI
ya wananchi wa kata ya tutuo na sikonge mjini wilayani sikonge mkoani Tabora
wamesema kuwa katiba mpya ijayo iwe ya serikali ya umoja wa kitaifa kulingana
na mfumo wa vyama vingi uliopo hivi sasa.
Wakitoa
maoni ya mabadiliko ya katiba mpya wakati tume hiyo ilipo tembelea kata hizo
kwa nyakati tofauti wilayani hapa walisema kuwa katiba ijayo iwe na serikali ya
umoja wa kitaifa kutokana na mfumo wa vyama vingi vilivyopo hapa nchini.
Walisema
kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa unapaswa kuwa na serikali ya umoja wa
kitaifa ili dhana hiyo ya vyama vingi iweze kutimia pamoja na kuepusha
machafuko yanayo weza kujitokeza.
Walisema
nchi zilizo endelea ambazo zinajali mfumo huo wa vyama mvingi vinatumia mfumo
huo wa serikali ya umoja wa kitaifa katika kuendesha shuguli zote za
kiserikali.
Sabina
kiwinga mkazi wa kata ya tutuo alisema kuwa serikali ya umoja wa kitaifa italeta
sura mpya katika katiba endepo pendekezo hilo
litakubaliwa na kufanyiwa kazi.
Alisema
kuwa utawala huo utaongeza wigo wa viongozi bora kutoka vyama mbalimbali
tofauti na sasa baadhi ya viongozi hawatendi haki kwa wananchi wao.
Alisema
kuwa serikali hiyo ya umoja wa kitaifa itatoa fursa ya kusikiliza kero za
wananchi bila kujali itikadi za dini wala kisiasa pamoja na kuhakikisha sheria
za nchi zinalindwa kwa kufuata taratibu na kanuni ya katiba hiyo itakayo
pendekeza.
Wananchi
hao wakifafanua serikali hiyo ya umoja wa kitaifa itakavyo kuwa ni chama
kitakacho pata kura nyingi kitapata kiti cha urais,makamu wa kweanza wa rais
atatoka chama pinzani ambapo makamu wa pili wa rais atatoka chama tawala.
Wakipanga
kazi za viongozi hao kwanayakati mbalimbali wananchi hao walisema kuwa makamu
wa kwanza wa rais atapangiwa wizara maalumu za kufanyia kazi pamoja na kuwa
mshauri wa rais huku makamu wa pili wa rais atakuwa mtendaji mkuu wa serikali.
Hirida
kamba alisema kuwa mawaziri na rais wote katika katiba itakayoyo undwa
mishahara yao
wote iwe hadharani ili kila mwananchi aweze kufahamu tofauti na sasa mishahara
hiyo haifahamiki kwa wananchi hao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment