Rais
JAkaya Mrisho Kikwete akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na
Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama
cha TNA, Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New
Ford Kenya, Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu
(kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA Bi Rachel Shebesh, na
Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge
wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar
es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012
Rais
JAkaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na
Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama
cha TNA. Kushoto kwa Rais ni Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene
Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya.
Wengine ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe.
Kambi Kazungu (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA Bi Rachel
Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda
(kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe
huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012
Rais
JAkaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Naibu Waziri wa Afya na mbunge
wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu. Wengine ni Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe
Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya, Naibu Waziri Mkuu wa Kenya
na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama
cha TNA. Kushoto kwa Rais ni Wengine ni (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa
chama cha TNA Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA
Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli
alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21,
2012
Rais
JAkaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe
Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya. Kulia kwake Naibu Waziri
Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni
Mwenyekiti wa chama cha TNA. Wengine ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge
wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha
TNA Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole
Sakuda (kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na
ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ametaka wananchi wa Kenya wapewe nafasi ya kuamua ni viongozi gani
wanawataka katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Machi mwakani.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kenya wanayo haki ya msingi
kabisa kuamua hatma ya taifa lao katika Uchaguzi Mkuu huo.
Mheshimiwa
Rais aliyasema hayo leo Oktoba 21, 2012 alipokutana na kufanya
mazungumzo na ujumbe wa wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya nchini
Kenya uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam.
Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa
chama cha TNA na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya. Wote wawili ni wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao.
chama cha TNA na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya. Wote wawili ni wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao.
Wengine
katika msafara huo walikuwa ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa
Mombasa Mhe. Kambi Kazungu, Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA Bi
Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda
na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli.
Rais
Kikwete aliwapongeza kwa kuamua kufanya kazi kwa pamoja licha ya kuwa
watakuwa washindani katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu huo.
Mheshimiwa
Rais ameitakia heri nchi ya Kenya katika uchaguzi huo ujao, na
kusisitiza kwamba nchi hiyo ya jirani ina umuhimu katika mustakabali wa
kiuchumi kwa nchi za Afrika Mashariki.
Rais
Kikwete wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alikuwa
miongoni mwa viongozi walioshughulika sana kutafuta ufumbuzi wa ghasia
na vurugu zilizozuka kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.
Rais
Kikwete alikaa siku tatu nchini Kenya akitafuta usuluhishi wa vurugu
hiyo ya kisiasa nchini humo, ambayo katika mazungumzo yake leo ameyataja
kama ajali iliyolipata Taifa la Kenya, na ambayo majirani wake
hawaitarajii kutokea katika uchaguzi ujao.
Mwisho
Imetolewa na:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
DAR ES SALAAM,
21 Oktoba, 2012
No comments:
Post a Comment