Thursday, October 25, 2012

YANGA YAITANDIKA POLISI MOROGORO MAGOLI 3-0, AZAM FC YANG’ANG’ANIWA CHAMAZI

Mchezaji wa timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam David Luhende akimiliki mpira mbele ya Nicholas Kabipe beki wa timu ya polisi ya Morogoro wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliokutanisha timu hizo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii mpira umekwisha  Yanga imeshinda magoli 3-0 dhidi ya polisi ya Morogoro, magoli ya Yanga yamefungwa na wachezaji Simon Muva na Didier Kavumbagu, na Hamis Kiiza kufunga idadi ya magoli kwa kufunga goli la tatu dakika ya 56 kipindi cha pili, mchezaji Haruna Niyonzima alikosa penati iliyotolewa na mwamuzi kwa madai ya golikipa wa Polisi kumchezea vibaya Simon Msuva jambo ambalo limelalamikiwa sana na wachezaji wa timu ya Polisi Morogoro
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya Vodacom uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi  kati ya Azam FC na Ruvu Shooting, matokeo ni kwamba timu hizo zimetoka sare ya kufungana magoli 1-1 na kugawana pointi moja kila timu.
 
Wachezaji wa timu ya Yanga Jerry Tegete kushoto na Didier Kavumbagu wakishangilia kwa staili ya kucheza mayenu baada ya mchezaji Kavumbagu kuifungiaYanga goli la pili katika kipindi cha kwanza.
Wachezaji wa timu ya Polisi Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mcheo huo na kubugizwa magoli mawili katika dakika tano tangu kuanza kwa mchezo huo goli la mwisho la Yanga limefungwa na Hamis Kiiza

No comments:

Post a Comment