Na Lucas Raphael,Sikonge
.
WANANCHI
wa kata ya ipole na kitunda wilayani sikonge mkoani Tabora wamesema
katiba mpya itakayoundwa ifute kodi za pikipikpi kutokana na usafiri huo kuwa
ni rahisi vijijini katika kutoa huduma mbalimbali kwa jamii hiyo.
Wakitoa
maoni ya mabadiliko ya katiba mpya wakati tume hiyo ilipo tembelea kata hizo
kwa nyakati tofauti wilayani hapa walisema kuwa usafiri huo utolewe uwe kama
usafiri wa Baiskeli ambao hauna kodi za shurti kama
pikipiki.
Walisema
baadhi ya Askari polisi wilayani humo huwa shurutisha wananchi hao wakati wa
kukamata kodi hali ambayo baadhi ya wakazi hao hushindwa kumudu ghalama hizo.
Walisema
kuwa Askari hao huwafukuza wananchi kwa pikipiki ili wapate kodi hiyo na kama wananchi huyo hana kodi hunyanganywa pikipiki hiyo
mpaka alipe kodi hiyo.
Walibainisha
kodi za kero ambazo wanapendekeza zifutwe ili usafiri huo uwe kama
Baiskeli ni pamoja na kodi ya Leseni ya udreva Daraja (A),Bima,sitika za ya
ukaguzi pamoja na kofia(helment).
Walisema
kero hizo zimewasukuma kudai katiba itakayo uindwa pikipiki iwe huru kama baiskeli ilikodi za kero katika usafiri huo zifutwe
pamoja na kuondokana na kukimbizana na Askari polisi ambao wame kuwa kero kwa
wananchi hao kutokana na kukamatwa kwa vyombo vyao.
’’Maoni
yetu ni kwamba pikipiki iwe huru kama Baiskeli
kodi zake zote zifutwe kwani ndio usafiri wetu waharaka sisi wananchi wa
vijijini pamoja na kupunguza kero ya polisi wetu ambao tunakimbizana mitaani
kwa kudai kodi ambazo hata faida pengine hazina katika pato la ndani’’alisema
mkazi mmoja wa ipole.
Sophia
Maganga (63) mkazi wa kata ya kitunda akichangia maon hayo kwan iaba ya wanawake wa kata hiyo ambaye alijitokeza pekee alisema kuwa usafiri huo
unawasaidia wanawake hususani wakati wa kujifungua pamoja na maeneo mengi ya
vijijini kukosa usafiri mwingine zaidi ya huo.
Sophia
alisema kuwa katiba mpya itakayopendekezwa ihakikishe kodi za shurti za
pikipiki zifutwe ili wananchi waweze kunufaika na usafiri huo pamoja na
kupunguza kero za polisi na maofisa wa T R A.
’’kama
kweli mme kuja kupata maoni yetu mimi kama
mwanamke pekee niliyeongea katika kikao hiki tunaomba kodi zote zifutwe ili
wananchi tunufaike na usafiri huu’’alisema mkazi huyo wa kitunda’’.
No comments:
Post a Comment