Mhe.
Hamad Rashid Mohamed akifuatilia Mjadala wa kamati ya Chama cha Umoja
wa Mabunge Duniani (IPU) Mjini Quebec, Canada, kuhusu maswala ya umoja
wa mataifa. Mada kubwa ilikuwa kuangalia kama kweli Umoja wa Mataifa
unalichukulia swala la demokrasia duniani kwa dhati.Picha na Owen
Mwandumbya
……………………………………………………….
Mbunge wa
Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani
Mhe. Hamad Rashid Mohamed ameteuliwa na kamati tendaji ya chama cha
Mabunge duniani (IPU) kuwa mjumbe wa kamati ndogo ya ukaguzi wa ndani kwa mahesabu ya mwaka 2013 ya chama hicho.
Uteuzi huo ulifuatia pendekezo
la umoja wa Mabunge ya Afrika lililowasilishwa na katibu mkuu wake Koffi
N’Zi tarehe 22 Oktoba, 2012 kufuatia kikao cha wajumbe wa umoja wa
Mabunge ya Afrika kumchagua Mhe. Hamad kuwakilisha Afrika kuwania
pendekezo hilo mbele ya kamati tendaji ya chama hicho.
Mhe. Hamad Rashid Mohamed, hii
ni mara ya pili kuiwakilisha Tanzania na Afrika katika kamati mbalimbali
za IPU ambapo mwaka jana katika Mkutano uliofanyika Mjini, Benn, Uswis,
alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya IPU cheo
ambacho anakitumikia hadi hivi sasa.
Katika kamati hiyo ya ukaguzi wa
ndani, Mhe. Hamad Rashid atafanya kazi pamoja na mjumbe mwingine
aliyeteuliwa Mhe. Duarte Pacheko kutoka Ureno, ambapo wanatarajia kutoa
taarifa ya kazi yao mwaka 2014 katika mkutano mkuu wa IPU.
Katika hatua nyingine, Wabunge
vijana wametakiwa kuwa chachu ya maendelo katika nchi zao kwa kushawishi
kutengeneza mazingira ya upatikanaji wa ajira kwa vijana katika kipindi
hiki cha uchumi wa kitandawazi.
Hayo yamesemwa jana na Mtaalamu
wa maswala ya ajira kutoka shirika la la kazi la umoja wa mataifa (ILO)
alipo toa maada katika mjadala wa Wabunge Vijana kujadili na namna ya
kupunguza ajira kwa vijana hususani katika kipindi hiki cha uchumi wa
utandawazi.
Mtaalamu huyo amesema ni wajibu
wa wabunge kuwa na ushawishi mkubwa kwa serikali zao na baadhi ya
taaisisi zinazotoa ajira ili kuwa na sera madhubuti kwa ajira za vijana
hususani wanaomaliza vyuo kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira kwa
vijana.
No comments:
Post a Comment