Na Lucas Raphael,Urambo
Askari polisi na
Magereza wilayani urambo mkoani Tabora wamesema kuwa majeshi yote nchini yawe
na usawa katika utendaji pamoja na uwajibikaji wa wakazi zao.
Wakitoa maoni ya katiba
mpya mbele ya tume ya maoni ya kukusanya maoni kundi la Tabora walisema kuwa
Askari polisi na Askari Magereza wapewe haki zinazo fanana na Askari wa jeshi
la wananchi(JWTZ).
Akizungumuza katika kikao
hicho cha kutoa maoni Osca mwenye namba E 7276 askari magereza alisema kuwa
usawa huo ni kutokana na kipato cha Askari wa Jeshi la wananchi (JWTZ)
nikikubwa tofauti na Askari wengine wa majeshi mengine ikiwa na Jeshi la Polisi
pamoja na Jeshi la Magereza.
Aliongeza kuwa Askari hao
wanafanya kazi kwa pamoja na kutumikia Taifa hili pamoja hivyo usawa katika
utendaji kazi utekelezwe.
Osca akitoa maoni yake
alisema kuwa Majeshi yote yalipwe stahiki sawa kutokana na kiapo chao kuapa
kulitumikia taifa hili kwa pamoja.
’’Tulipwe kwa sawa nasisi
tunafanya kazi kama hizo kama ikitokea vita tutaenda wote hivyo ni bora tukawa
tunalipwa posho sote ili kutoa utabaka katika majeshi hivyo katiba hii
izingatie hilo’’alisema Askari huyo .
Wakizungumuza kwa nyakati
mbalimbali Askari hao walisema kuwa upandishwaji wa vyeo haufuati taratibu za
kisheria kutokana na upendeleo kwa baadhi ya viongozi wa ngazi za juu.
Wakitoa maoni yao walisema
kuwa vyeo hivyo vipandishwe kila baada ya miaka mitatu kama ilivyo kuwa hapo
awari ili kila Askira aweze kupandishwa vyeo vyao na kuongeza kuwa sheria
zilizopo katika majeshi zifuatwe na utekelezaji wake utekelezwe kiusawa.
Joakimu Nindi Mratibu wa
Jeshi la Magereza wilayani Urambo akitoa maoni yake alisema kuwa majeshi yote
yasifungamane na siasa ili kila jeshi lifanye kazi yake kwa uhuru zaidi.
Tume hiyo kundi la tabora
limehitimisha zoezi hilo wilayani Urambo ambapo likitarajia kuelekea wilayani
sikonge kuendelea na mchakato huo wa kukusanya maoni hayo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment