Na Lucas Raphael,Tabora
CHUO .cha Amuct
kimewaalika WADAU mbalimbali wa Elimu mkoani Tabora kwa ajili ya kushiriki
mwaka wa masomo kwa wanafunzi na kula chakula cha pamoja kwa lengo la kuwa
karibu na wanafunzi na wahadhiri wa chuo hicho na wadau.
Akizungumza jana na ukurasa huu makamu mkuu wa chuo hicho
mkoani hapa Dkt Eustard Tibategeza alisema kwamba chuo hicho kinautaratibu wa
kukutana na wadau wa elimu kwa ajili ya kupata maoni yao na kueliezea nin I chuo
hicho kinafundisha.
Alisema kwamba
licha ya kukutana na wadau hao pia wanakula chakula cha pamoja na wanachuo hao kwa lengo la kuwa karibu nao katika
matatizo mbalimbali ambayo yanawapata wanachuo kwa kipindi watakachuo kuwa hapa
.
Alisema kwamba
ufunguzi huo utafanyika octoba 13 mwaka huu kwenye viwanja vya chuo hicho kwa
kuelelezwa wanachuo hao na wadau juu ya malengo ya chuo hicho juu ya masoma
wanayatoa kwa kila mwaka wananchuo wake.
Alisema kwamba
watatoa malengo ya kitaaluma ,ushauri kwa wanafunzi ,mikakati ya kujisomea na
kuhakikisha wanafanikiwa katika malengo yaliyowaleta hapa na kujimuika kwa
wadau wetu wa elimu ..
Dkt Tibategeza
alisema kwamba kwa mwaka ujao wa masoma chuo hicho kimekusudia kutoa digrii ya
pili ya utawala na mipango kwa watu wakatakao hitaji kusoma masomo hayo ambao
mara nyingi muda wa masomo utakuwa ni jioni kwa wale wanafanyakazi katika sekta
mbalimbali mkoabni hapa.
Hata hivyo makamu
mkuu wa chuo hicho alisema kwamba hadi usajili utakapo kamilika kwa wanachuo
walipoa kwenye chuo cha AMUCTA ni 3500
Mwisho
No comments:
Post a Comment