Na Lucas Raphael,Sikonge
Wanawake wa kata
ya kitunda wilayani sikonge mkoani Tabora wamesema katiba mpya itakayo undwa
ilinde kundi la wanawake wato nchini kutokana na kundi hilo kunyanyaswa na jamii inayo wazunguka.
Wakitoa maoni ya
mabadiliko ya katiba mpya tume hiyo ilipo temb elea kata hiyo walisema kuwa
kundi la wanawake likumb ana na changa moto mbalimbali za kijamii ikiwa na
kunyanyaswa kijinsia na kundi la wanaume kwa ngazi mbalimbali.
Issa siraji
Mohamedi (51) mkazi wa kata hiyo ali sema wanawake wengi husani vijijini
wananyanyaswa na wanaume wao kutokana na kutofaham sheria zinazo walinda.
Alisema kuwa
wanawake hupigwa,kubakwa ikiwa na kufanya kazi ngumu kila wakati hali ambayo
wanawake hao hushindwa kujua haki zao wazipate wapi kutokana na kutofahamu
sheria zao.
Issa akitoa
maoni yake alisema kuwa katiba mpya itakayo undwa iwalinde wanawake ikiwa na
kuwapatia elimu juu ya haki yao
ili kutoa fursa ya kuwapatia haki za msingi ambazo wanapaswa kuzipata.
Alisema kuwa
sheria kali ziwekwe za kuwa Linda wanawake kwa lika zote ikiwa na kuwabana
wanaume wanao wanyanyasa wake hao.
Kundi hilo la wanawake katika mikutano mbalimbali ya kutoa maoni
ya katiba mpya wanawake wamekuwa hawajitokezi kwa wangi ilikuja kutoa maoni yao juu ya katiba itakayo
undwa.
Aginnes kapamila
(56) mkazi wa kata hiyo kitoa maoni yake alisema kuwa katiba mpya iwalinde
wanawake hasa kwa kuwaangalia kuwa wengi wao hawajitokezi kutoa maoni na mwanya
huo usitumike kuwakandamiza.
Akibainisha
changamoto zinazo wakabili wanawake kuwa ni pamoja na kufanya kazi
ngumu,kubakwa,kunyimwa mirasi pamoja na kupigwa na waume zao ,Katiba hiyo
izingatie mambo muhimu yanayo wagusa wanawake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment