Wednesday, October 24, 2012

SITAKI KUGOMBEA UBUNGE!!!...MJUMBE WA NEC JOHN MCHELE

Na Hastin Liumba,Tabora

MJUMBE wa halmashauri kuu ya CCM taifa,(MNEC),John Mchele,amesema pamoja na kupata nafasi hiyo,bado hana nia ya kuwania ubunge kama inavyotafsiriwa sasa kuwa anajipanga.

Kauli hiyo aliitoa jana kwenye hafla fupi ya kuwashukuru wanaCCM,na wananchi baada ya kumpa nafasi aligombea ya ujumbe wa NEC wilaya ya Tabora mjini.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu zaidi ya 600 ambao ni wanachama wa CCM,viongozi wa madhehebu ya dini,viongozi wa taasisi za serikali na wafanyabiashara.

Mchele pamoja na kuweka rekodi ya mjumbe wa NEC wa kwanza toka wilaya ya Tabora mjini,alisema pamoja na kutoa shukrani hizo kwa wanaCCM,nafasi aliyonayo anataka kuwatumika wanachama wa chama cha mapinduzi kamwe hana wazo la kuogombea ubunge.

“Nafasi niliyopata ya ujumbe wa NEC inatosha sitaki kujaza vyeo vingi pekee yangu nataka na wanachama wenzangu wapate nafasi ya kukitumikia chama na wananchi…..nafasi hii inanitosha sana ndugu zangu.”alisema.

Alisema atawatumikia watu wote bila ya kujali makundi,itikadi za vyama kwani anatoka katika nafasi ya uenyekiti wa TCCIA nafasi ambayo ni sekta binafsi.

Mchele aliongeza kuwa anaipongeza na kuishukuru, CCM mkoa wa Tabora na taifa, kwa kuweza kurejesha jina lake na hatimaye kuwa mjumbe wa NEC,na kamwe hatowaangusha wanachama wenzake.

Hata hivyo aliwataka wanaCCM wenzake mkoani Tabora kuachana na makundi ambayo yamekuwa yakikimega chama cha mapinduzi na zaidi tukifanya mema watanzania wanayotarajia tunaweza kuongoza dola milele.

Alisema kazi ambayo anaamini sasa ni kujenga CCM mpya na iliyobora ili chama chetu kiweze kuongoza dola kila chaguzi zinapowadia.

Alisema nafasi aliyopata ataitumika vyema kwa kutoa ushauri wenye busara na kamwe makundi yasipewe nafasi ya kuweza kuwapa hoja wapinzani kushambulia.

No comments:

Post a Comment