Mwenyekiti
mpya wa UVCCM Sief Hamisi Ghulamali muda mfupi mara baada ya kutangazwa
mshindi katika uchaguzi mkuu mkoani Tabora,Ghulamali atashika wadhifa
huo kwa muda wa miaka mitano.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UVCCM mkoani Tabora wakishangilia ushindi wa mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya umoja wa vijana Seif Ghulamali.
Baadhi ya wajumbe wakiwa wanasubiri kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo baada ya kupiga kura katika ukumbi wa chuo cha utumishi wa umma Uhazili mjini Tabora.
Mjumbe mmoja akiwa ametoka kuchukua chakula wakati akisubiria kwa hamu kubwa matokeo ya uchaguzi huo.
Mgombea wa nafasi ya uenyekiti UVCCM, Sunday Kabaye akitoa neno la shukrani katika uchaguzi huo baada ya kushindwa na kukubali matokeo.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UVCCM mkoani Tabora wakishangilia ushindi wa mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya umoja wa vijana Seif Ghulamali.
Baadhi ya wajumbe wakiwa wanasubiri kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo baada ya kupiga kura katika ukumbi wa chuo cha utumishi wa umma Uhazili mjini Tabora.
Mjumbe mmoja akiwa ametoka kuchukua chakula wakati akisubiria kwa hamu kubwa matokeo ya uchaguzi huo.
Mgombea wa nafasi ya uenyekiti UVCCM, Sunday Kabaye akitoa neno la shukrani katika uchaguzi huo baada ya kushindwa na kukubali matokeo.
Mwenyekiti
wa UVCCM Seif Ghulamali mara baada ya kutajwa kuwa mshindi katika
kinyang'anyiro hicho ambapo ukumbi mzima ulizizima kwa vifijo na
ndelemo.
Na Hastin Liumba,Tabora
Jumuiya ya umoja wa vijana chama cha mapinduzi,(UVCCM),mkoa wa Tabora imekamilisha
uchaguzi wake jana huku vitendo vya rushwa vikiwa nje nje hali iliyopelekea
diwani wa kata ya Kitete,(CCM),kuchapwa makofi na afisa wa TAKUKURU.
Katika uchaguzi
huo ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa
chuo cha utumishi wa umma,kampasi ya Tabora,ulianza majira ya saa sita mchana.
Aidha wagombea
wa nafasi ya mwenyekiti katika jumuiya
hiyo walikuwa ni Sunday Kabaye,Seif Ghulamali na Janeth Masika.
Akitangaza matokeo
hayo msimamizi wa uchaguzi huo,Idd Ame alimtangaza Seif Ghulamali kuwa mshindi
baada ya kujizolea kura 336,Sunday Kabaye kura 156 na janeth Masika kura 6 na
kura halali ziliopigwa ni 499.
Baada ya
uchaguzi huo kutangazwa matokeo yake,baadhi ya wajumbe kutoka wilaya ya
Kaliua,waliteta na gazeti hili kuwa walipewa maelekezo na “Profesa” bila kutaja
jina wamchague Ghulamali.
“Tulitakiwa
kumchagua Ghulamali huku mweznetu mmoja akisema maelekezo hayo ni kutoka kwa
profesa……tukawa hatuna jinsi na chai tulishapewa.” Alisema mjumbe huyo huyo
akigida bia yake ya Balimi.
Chanzo kingine
cha habari kilisema kuwa kuna kundi moja ambalo mgombea wao alishindwa kwenye
kiti cha jumuiya ya UWT,hivi karibuni lilijiapiza kuwa baada ua kushindwa UWT
wataonyeshana ubabe kwenye uchaguzi wa UVCCM.
Aidha kundi
hilo baada ya jana matokeo kutangazwa lililipuka kwa shangwe huku likicheza
muziki wa taarabu na kumkejeli mgombea aliyeshindwa Sunday Kabaye,kwa kuimba
Sunday!Sunday!Sunday!.
Chanzo kimoja
cha taarifa kilibainisha kuwa kundi hilo tayari limeanza kujipanga na kudai
kiti cha WAZAZI, mkoa watakibeba ili heshima iwepo.
Wakati hayo
yakiendelea nje ya ukumbi,baadhi ya wajumbe walisema endapo ujinga huo
utaendelea watahama chama bila kueleza watahamia chama gani.
Walisema jumuiya
ya UVCCM imeletewa kiongozi wa kuongozwa na rimoti kwa maslahi ya kundi la watu
wachache.
Aidha tukio
la kupigwa makofi na kufukuzwa kwa diwani wa kata Kitete na maafisa wa TAKUKURU
kuliashiria kuwa uchaguzi huo uliashiria ulikuwa na vitendo vya rushwa.
Chanzo kimoja
cha taarifa kilisema ndani ya ukumbi rushwa ilikuwa ya wazi wazi kwa wajumbe
kushinikiza mgombea mmoja achaguliwe.
No comments:
Post a Comment