KUTOKA
KUSHOTO NI HALIMA SHARIF,RUTH MEENA MWENYEKITI WA (WFT) MGENI RASMI
LETICA MUKURASI NA BI. SHAMSAD REHLI (OSIEA) WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO
KABLA YA KUFUNGULIWA RASMI
BAADHI YA WASHIRIKI WKONGAMANO HILO WAKIFUATILIA KWA MAKINI MADA ZILIZOKUWA ZIKITOLEWA KATIKA KONGAMANO HILO.
…………………………………………..
Tangu 2011, Tanzania imekuwa
ikiendesha mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba ya nchi
katika jitihada za kutengeneza katiba mpya ifikapo 2015. Asasi ya Women
Fund Tanzania (WFT) (au Mfuko wa Wanawake Tanzania), iliyojikita katika
kutetea haki za wanawake nchini, ikishirikiana na wadau wengine walio
katika harakati hizi, wameandaa mkutano wa siku tatu utakaojadili
maswala muhimu ya wanawake katika katiba mpya. Mkutano huo utafanyika
Oktoba 22 hadi 24, 2012, katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo, Dar es
Salaam.
Washiriki wa mkutano huo wanatoka
katika nyanja na mashirika mbali mbali nchini na wataibua na kujadili
mapungufu yaliomo katika katiba ya sasa, na kutengeneza mikakati ya
kuyashughulikia mapungufu haya. Wanaharakati wanawake na wakereketwa wa
maswala ya haki za wanawake wanatarajiwa kwa pamoja kuainisha maswala
muhimu ya wanawake yanayostahili utetezi ili yazingatiwe katika katiba
mpya.
Mkurugenzi wa WFT, Mary Rusimbi
amesema: “Mkutano huu unatoa nafasi muhimu kwa wanawake kujadili kwa
kina na kuimarisha uelewa wao juu ya maswala nyeti yanayogusa haki zao
katika mchakato unaoendelea hivi sasa. Pia ni fursa kwa wanawake
kujifunza mbinu zinazokubalika katika kujenga sauti moja na msimamo wa
pamoja katika mchakato huu.”
Asasi ya WFT na washirika wake
wanaendeleza harakati hizi kutokana na umuhimu wa ushikishwaji wa
wanawake katika maswala ya kikatiba na hasa katika nchi ambayo bado ina
baadhi ya sheria i zinazomkandamiza mwanamke.
Katiba ya sasa ya Tanzania ya
mwaka 1977 inadai kutomkandamiza mwanamke kwa jinsi yake au jinsia,
japokuwa kuna sheria kadhaa zinazotoa kipaumblele kwa taratibu za
kimila, na hivyo kutozingatia haki za wanawake. Sheria hizi zinahusu
maeneo mbalimbali kama vile ndoa, talaka, afya ya uzazi, elimu uongozi,
siasa, na maswala ya kujikimu kimaisha.
Wanawake 100 kutoka Tanzania bara
na Zanzibar, wamealikwa kuhudhuria mkutano huo unaotarajiwa kutoa
mpango kazi utakaoongoza harakati za kutetea haki za wanawake katika
katiba mpya.
Washiriki watatokea makundi
mbalimbali yakiwemo yale ya kijamii, ya kibiashara, vyama vya
wafanyakazi, taasisi za elimu ya juu, vyama vya kisiasa, mashirika ya
kidini, vyombo vya habari, teknologia ya habari, asasi za mazingira,
afya, utamaduni, na wafanyabiashara.
No comments:
Post a Comment