MJUMBE halmashauri kuu ya CCM ,(NEC),mkoani Tabora, John Mchele,
amesema hakuamini endapo amefanikiwa kupata nafasi hiyo muhimu ndani
ya chama,lakini atahakikisha anawatumikia wanaCCM, kwa moyo wake wote.
Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni wakati alipokuwa akifanya mahojiano
na gazeti hili ofisini kwake.
“Haikuwa rahisi kuamini kwamba mimi nimekuwa mjumbe wa NEC ya CCM au
ni utani".haya yalikuwa baadhi ya maneno ya Mchele.
Mchele alisema kwa matokeo hayo atahakikisha akidhamilia anafanya
jambo fulani na tena lililo na maslahi kwa jamii huwa harudi nyuma
hadi kupatikana kwa mafanikio au la sivyo jua litachomoza na kuzama
hadi kieleweke.
Anaongeza kuwa mara kadhaa amekuwa na mshangao kwa baadhi ya watu na
wanaCCM, ambao wamewahi kumshawishi hata kugombea Ubunge katika
chaguzi zilizowahi kufanyika hasa wa mwaka 2000,2005 na 2010 lakini
bado sipo tayari.
Mchele anasema kuwa hakuwa tayari kufanya hivyo na wala kuonesha
dalili zozote za kujitosa katika kinyang'anyiro chochote ndani ya CCM
kwa wakati huo.
Anafafanua kuwa binafsi si mtu wa makundi,si mtu wa kushawishiwa
kuingia kwenye migogoro,na wala si mtu wa kulipizana kisasi na mtu
aliyemkosea.
Aidha anasema kuwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za ngazi za
mkoa hasa kwenye vitengo vya taasisi za wafanyabiashara na
wasafirishaji,na sasa yeye ni mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Tabora na
anaamini atawaunganisha wanachama katika Taasisi hizo na Serikali.
Aliongeza kuwa amekuwa akishiriki kwa hali na mali shughuli za kijamii
ambapo nafasi ya ujumbe wa NEC ataitumia kuunganisha watu hata kama
hakuwahi hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi.
Anaongeza kuwa jitihada zake atazielekeza zaidi katika kuonesha
anaweza kuwaongoza wana CCM wenzake na hasa mchango wake wakati huu
wa mfumo wa vyama vingi kwakuwa ili CCM iweze kushinda inahitaji ipate
watu wabunifu,waaminifu na waungwana.
No comments:
Post a Comment