Balozi
Seif Ally Iddy akizungumza na waandishi wa habari kwenye mahafari ya 10
kwenye shule ya sekondari ya Modern alipokuwa mgeni rasmi mwishoni mwa
wiki.kushoto ni mkuu wa shule hiyo Philip Wasike. PICHA NA MAHMOUD AHMED
………………………………………….
Na.Ashura Mohamed-Arusha
Makamu wa Pili wa Rais wa
Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Iddi amewataka wazazi
nchini kuwekeza katika sekta ya elimu ili watoto waweze kupata elimu
bora zaidi kwa kuwa karne ya sasa ni tofauti na karne ya zamani.
Aliyasema hayo katika mahafali ya
kumi ya kidato cha nne,sita,darasa la saba,kidato cha tatu c katika
shule ya Arusha Mordem iliyopo eneo la Kisongo nje kidogo mwa Jiji la
Arusha.
Balozi Seif alisema kuwa hii ni
karne ya 21 ya sayansi na teknolojia ambapo elimu ni kitu cha thamani na
kikubwa sana hivyo pindi mzazi anapokuwa amewekeza katika elimu kwa
mtoto wake basi ni wazi kuwa mzazi anakuwa ameisaidia serikali kuandaa
taifa ambalo si tegemezi.
Pia Balozi Seif alikemea tabia ya
viongozi kuingiza swala la siasa katika mambo muhimu kama elimu kwa
kuwa inaondoa ufanisi katika sekta hiyo hivyo amewataka viongozi
kutenganisha siasa na elimu kwa siasa kubaki siasa na elimu iwe ni
elimu.
Alisema kama siasa itaingizwa
katika sekta ya elimu basi matokeo yake ni kuvurunda katika sekta hiyo
hivyo ni lazima jitihada za makusudi zifanyike ili kuzuia siasa katika
sekta hiyo na iendelee kufanya vizuri ili Tanzania ipate viongozi bora
wa baadae wenye elimu ya kutosha itakayoisaidia nchi kupata maendelao.
“Mimi nataka niwaambie kuwa
hakuna haja ya kuingiza maswala ya siasa katika sekta ya elimu ila siasa
ibaki kama siasa alafu elimu pia ibaki kama elimu tukienda kwa mfumo
huo tutapata mambo mengi mazuri ila tukiingiza siasa sekta hii
itavurugika na tusitegee chochote kipya”alisema balozi Seif
Kwa upande wake mkuu wa shule
hiyo Philip Wasike alisema kuwa kuna uvumi ulionea kuwa shule ya arusha
morden imefilisika na kuuzwa kwa taasisi moja ambapo amefafanua kuwa
uvumi sio ukweli bali kilichofanyika ni kuwa kutokana na eneo la shule
hiyo lilivyokaa imeonekana kuwa ni dogo hivyo uongozi wa shule hiyo
umeamua kujenga compus nyingine katika eneo la njiro ambapo itagharimu
jumla ya shilingi bil.6.
Bw.Wasike alisema kuwa shule ya
Arusha Morden kwa sasa inafanya vizuri katika matokeo mbalimbali haswa
katika mtaala wa Cambrige ambapo wanafunzi wamekuwa wakifaulu kwa
kiwango kikubwa zaidi hivyo lengo la compus hiyo kuhamishiwa Njiro ni
kuwa shule ya kipekee zaidi kwa kuwa shule hiyo kwasasa ina mitaala
miwili ya baraza la mitihani Tanzania(NECTA) na Baraza la mitihani la
uingereza(CAMBRIGE).
Aliongeza kuwa bila kuwa na
eneo la kutosha wanafunzi hawataweza kujisomea kwa nafasi ya kutosha
kila mmoja kutokana na mtaala wake bila kuathiri wengine hivyo compus
hiyo ya njiro inategemewa kumalizika na pindi ifikapo April 2013 compus
ya kisongo itahamia njiro.
Pia alitumia fursa hiyo kutoa
changamoto kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kujaribu
kuangalia namna ya kuboresha mfumo wa elimu wa Tanzania ili uendane na
karne ya sayansi na teknolojia kwa kuwa mfumo huo iliopo mpaka sasa
umetumika kwa muda mrefu sana.
Amesema kuwa mfumo uliopo wa
elimu unaonekana kama ni wakukariri hivyo ni lazima pafanye mabadiliko
ili ueendane na wakati uliopo kwa kubadili aina ya ufundishaji kwa sasa
ambao utamfanya mtoto afikiri zaidi ili uweze kumsaidia pia hata
kutumia akili njyingi zaidi kufikiria maisha na kujitegemea bila
kutegemewa kuajiriwa.
Jumla ya wanafunzi 130 wamehitimu
elimu ya msingi na sekondari ambapo shule hiyo ina wanafunzi kutoka
nchi kumi na mbili tofauti ndani na nje la bara la afrika
No comments:
Post a Comment