Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Raphael Muhuga
aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Tanzania katika sherehe za
maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuzaliwa kwake.
Mgeni
rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta
akiwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo katika
Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa Tanzania kusheherekea
miaka 67 tangu uanzishwe.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akimlaki na Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaa leo.
Pichani
Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic
Kacou (katikati) akimtambulisha Mh. Samwel Sitta kwa baadhi ya
Wakurugenzi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Waziri
wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akipokea heshima ya wimbo wa Taifa
baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo
kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa baada ya
kutimiza miaka 67 ya UN tangu kuanzishwa.
Mh. Samuel Sitta akikagua gwaride maalum katika kilele cha wiki ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa.
Waziri
wa Afrika Mashariki akishuhudia upandishwaji wa bendera ya Umoja wa
Mataifa ikiwa ni ishara ya kusheherekea miaka 67 ya Umoja huo katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar leo.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou, Mgeni rasmi Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta na Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) Meha Jenerali Raphael Muhuga wakiwa Meza kuu.
Pichani
Juu na Chini ni viongozi wa Madhehebu ya Dini nchini wakiomba Dua kwa
ajili ya kubariki sherehe za kutimiza miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu
kuanzishwa.
Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Samwel Sitta akizungumza katika sherehe za kutimiza
miaka 67 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) katika viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam, Sitta aliipongeza Umoja wa Mataifa kwa
kuisaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ili kutokomeza
umaskini.Waziri Sitta alisisitiza kwamba bado Umoja wa Mataifa
unakabiliwa na changamoto nchini kama vile amani na usalama, tatizo la
njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uwepo wa silaha za maangamizi.Mh.
Sitta alifafanua katika kilele cha sherehe hizo umuhimu wa kupitia na
kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo ya millennia.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akitoa nasaha zake
wakati wa maadhimisho ya umoja huo katika viwanja vya Karimjee alisema
matatizo ya njaa, kupanda kwa bei za mafuta na mtikisiko wa uchumi
duniani ni kati ya changamoto kubwa ambazo Umoja wa Mataifa inakabiliana
navyo katika dunia ya leo. Dtk Kacou pia aliipongeza Tanzania katika
juhudi zake za kupunguza vifo vya wakinamama wakati wa kujifungua na
watoto ili waweze kufikia malengo ya millennia itakapofika 2015.Mratibu
Mkazi wa UN alisema Tanzania imepunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi
mapya ya ugonjwa wa Ukimwi.
Katibu wa UNA Tanzania Fancy Nkuhi akizungumza kwenye hafla hiyo alisema umoja wa mataifa imefanya kazi kubwa katika kuwaunganisha
vijana wa bara la Afrika. Nkuhi alisema kupitia YUNA walitoa elimu ya
afya ya uzazi na ugonjwa wa Ukimwi kwa vijana katika mikoa kumi hapa
nchini Tanzania katika harakati ya kuelimisha vijana madhara ya ugonjwa
huo na afya ya uzazi kwa vijana.
Wanafunzi
kutoka shule ya mchepuo wa kiingereza ya Heritage (Heritage English
Medium Schools) ambao walikuwa kivutio wakati wa maadhimisho ya miaka 67
ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakiwa katika gwaride
maalum kupamba sherehe hiyo.
Meza
kuu ikifurahia jambo wakati wa gwaride la watoto wa shule ya Heritage
baada ya kuonyesha mbwembwe katika kupamba sherehe hiyo.
No comments:
Post a Comment