Na Lucas Raphael,Tabora
WAHITIMU wanaomaliza vyuo vikuu nchini wameaswa kutotengemea kazi za kuajiriwa na badala yake wawe na mawazo ya kujiajiri wenyewe.
WAHITIMU wanaomaliza vyuo vikuu nchini wameaswa kutotengemea kazi za kuajiriwa na badala yake wawe na mawazo ya kujiajiri wenyewe.
Mkuu
wa mkoa wa Tabora Fatuma Mwassa katika hotuba yake iliyosomwa na mkuun wa
wilaya ya Tabora mjini Sulemani Kumchaya alisema kwamba lazima wahitimu wa vyuo
vikuu kuondokana na mawazo ya kuajiriwa katika maisha yao .
Ameeleza
ili kuondokana na mawzo hayo ya kuajiriwa ,wanafunzi wa vyuo vikuu ,ni lazima
wae na mawazo ya kutumia elimu watakayopata kujiajiri tangu wanapoingia mwaka
wa kwanza chuoni.
Akizungumza
na wanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha Askofu mkuu mihayo (AMUCTA)katika kuukaribisha
mwaka mpya wa masomu 2012 /2013.
Kumchaya
amewahakikishia wanafunzi hao kuwa ofisi yake ipo tayari kuwasaidia ili
wajiajiri pindi wamalizapo masomu yao
katika chuo hicho kikuu .
Naye
mwenyekiti wa bodi ya wakurungezi wa chuo hicho ,Askofu mkuu wa mhashamu Paul
Ruzoka alisema kwambawananchuo kwa kuwepo kwao chuoni sio kujifunza kupata
cheti bali kujingea ufanisi katika maisha yao na pia kuwasidia wengine na jamii
kwa ujumla wake.
Askofu
Ruzoka ambaye pia analiongoza jimbo kuu wa la Tabora amewataka watumie fursa waliyoipata
vizuri ,wakielewa kuwa serikali imewawezesha na jamii inawasubiri ili
waitumikie .
Mwisho
No comments:
Post a Comment