Na Lucas Raphael ,Sikonge
BAADHI ya wananchi wa kata
ya kipili wilayani sikonge mkoani Tabora jana walisema kuwa mikataba itakayo
sainiwa na serikali isainiwe bungeni pamoja na kuandikwa kwa lugha ya
Kiswahili.
Wakizungumuza kwa nyakati
mbalimbali wakati wakitoa maoni ya katiba mpya wananchi wa kata hiyo walisema
kuwa baadhi ya viongozi wanaingia mikataba ambayo haina manufaa kwa Taifa
badala yake mikataba hiyo huwanufaisha baadhi ya viongozi.
Walisema kuwa katiba
itakayo undwa iweke sheria madhubuti ya kuhakikisha mikataba yote inafungiwa
mbele ya bunge pamoja na kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili kila mwananchi
aweze kuielewa.
Waliongeza kuwa mikataba
hiyo isiwe siri kama baadhi ya mikataba hapa nchini ambapo haifahamiki kwa
wananchi bali mikataba hiyo ifahamike ili kila Mtanzania aelewe mkataba huo
unavyo kwenda.
Wakiendelea kutoa maoni
hayo waliomba katiba itakayo undwa iweke uwazi wa mikataba hiyo pamoja na
kuzingatia maoni hayo yaliyotolewa na wananchi hao.
‘’Tunataka katiba hii
iweke mkazo juu ya hili kwani tunapata adha sana sheria ndogo ndogo ziwabane
wawekezaji hawa’’ alisema mkazi mmoja wa kijiji hicho.
Waliongeza kuwa richa ya
mikataba hiyo kuhakikiwa na bunge mkataba huo uwanufaishe wananchi waeneo
husika kwa kodi za mradi huo pamoja na huduma za kijamii ili wananchi waweze
kunufaika na mikataba itakayo endelea kuwekwa na serikali ikiwa ndani ya katiba
mpya.
‘’Tuna taka mikataba yote
tuifahamu,iandikwe kwa lugha nyepesi pia i sambazwe kwa wananchi ili kila
mwananchi afahamu mikataba hiyo tofauti na sasa baadhi ya mikataba imeandikwa
kiingereza pia haionekani ni siri kubwa kwa watu’’alisema Edward Nalali.
Mbali na maoni hayo
wakiendelea kuchangia walisema kuwa kuwepo na tume huru ya uchaguzi ambayo
itakayo jitegemea yenyewe pamoja na serikali iwajali wajane,Virema,wazee pamoja
huduma za Afya.
Tume huru ya kukusanya
maoni ya katiba mpya kundi la mkoa wa Tabora linaendelea wilayani sikonge baada
ya kuhitimisha zoezi hilo wilayani urambo huku likiongozwa na mwenyekiti wake
Fatuma said Ally.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment