WAKAZI WA kata za kakola na kalunde wilaya ya Tabora
mjini mkoani hapa wamesema kuwa katiba itakayo patikana irejeshe jeshi la
kujenga taifa kwa vijana wanaohitimu Elimu ya kidato cha sita ambao wanatarajia
kuingia vyuo vikuu ili kuwajenge uzalendo kwa nchi yao.
Wakizungumuza
kwa nyakati mbalimbali wananchi hao mbele ya tume ya kukusanya maoni ya katiba
walisema kuwa utaratibu huo ukirejeshwa utadumisha utamaduni na uzalendo wa mtanzania
ambao unaelekea kupotea kwa wananchi.
Walisema
katiba hiyo ikizingatia mambo hayo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na elimu
ya juu mpaka wapitie kozi hiyo fupi itaongeza maadili ya mtanzania ambayo
yanazidi kutokomea kufuatia kuingiliwa na tamaduni za nchi za maghalibi.
Peter
Manzilili mwalimu mkuu wa shule ya msingi umanda akitoa maoni yake ya kupata
katiba mpya alisema kuwa Jeshi la kujenga Taifa likianzishwa litaongeza mapenzi
kwa kizazi hiki ikiwa na kukabiliana na matatizo ya ajira kwa vijana ambapo
imekuwa ni kelele kila kona.
Mafunzo
hayo yakiendeshwa vizuri kwa kufuata utaratibu vijana wengi watapata fursa ya
kujiajili kutokana namafunzo hayo ikiwa na kufanya kazi kwa bidii tofauti na
wakati huu.
Alisema
kuwa katiba hiyo ikizingatie hayo vijana watafanya kazi kwa bidii ikiwa na
kuipenda kazi nchi yao
tofauti na sasa vijana wengi hawana uzalendo.
‘’endapo
katiba hii ikaliweka suala hili naimani kabisa vijana watajiajili na wengine
kupata kazi na kuipenda zaidi nchi yao kama vijana wa zamani ambao sasa ni babu zetu bado
wanaipenda nchi hii kutokana na mfumo huo wa JKT’’alisema mwili huyo.
Rusi
Ismaili mkazi wa kata ya kakola aliongeza kuwa utaratibu huo ukirejeshwa hata
wa naume watasitisha kuwa piga wake zao kutokana na mafunzo hayo kufundishwa
kupendana na uzalendo kwa ujumla.
Aliongeza
kuwa kwa mufumo huo unyanyasaji wa kijinsi utapungua kwa wanawake pamoja na
haki zote za wananwake zitapatikana kupitia Jeshi hilo.
’’kama
kweli tunataka mabadilio basi katiba mpya irejeshe jeshi hili ili vijana wetu
wajifunze maadili uzalendo hapo tutapata mabadiliko ya kutosha na Tanzania hii itakuwa safi’’alisema Rusi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment