Thursday, October 11, 2012

MKUU WA MKOA WA SINGIDA AHIMIZA WANANCHI KUTUNZA BARABARA

 


Dkt. Parseko Kone akizungumza na wananchi wa kata ya Nkonko jimbo la Manyoni Mashariki wakati akihimiza utunzaji wa barabara pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ili waweze kutumia barabara kuyafikisha mazao hayo kwenye masoko ya uhakika.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone (wa kwanza kushoto) akielekeza jambo wakati akikagua barabara ya Chikuyu hadi kijiji cha Sanza wilayani Manyoni.Wa kwanza kulia ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida Mhandisi Yustaki Kangole akimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa. Wa pili kushoto ni mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki John Chiligati.
Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida Yustaki Kangole (wa kwanza kulia), akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone (wa pili kulia) wakati mkuu huyo wa mkoa akikagua barabara ya Chikuyu hadi kijiji cha Sanza inayojengwa kwa kiwango cha changarawe.
 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone ( wa pili kulia aliyenyoosha mkono) akielezea jambo wakati akikagua barabara ya Chikuyu hadi kijiji cha Sanza inayojengwa kwa kiwango cha changarawe. Wa kwanza kulia ni meneja wa TANROADS mkoa wa Singida mhandisi Yustaki Kangole.
 Sehemu ya barabara ya kutoka kijiji cha Chikuyu hadi kijiji cha Sanza jimbo la Manyoni Mashariki  inayojengwa kwa kiwango cha changarawe.
 (Picha zote na Nathaniel Limu).

No comments:

Post a Comment