Thursday, October 11, 2012

MWENYEKITI UVCCM MKOA WA TABORA ATOA SHUKRANI KWA KUCHAGULIWA

 



Ndugu zangu wana Tabora wenzangu.

Napenda kutoa Shukraani zangu za dhati kwanza kwa Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njema nguvu pia lakini pia nawashukur wijana woote wa wilaya zoote 7 za Tabora kwa kunichagua kuwa MWENYEKITI WA UVCCM MKOA TABORA.

 
Ninaimaani nitashirikiana nanyi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili katika mkoa wetu wa Tabora katika sekta mbalimbali kisiasa,kijamii,kiutamaduni na Kiuchumi.
Ni imaani yangu kuwa Vijana tukiamua Tunaweza.

ASKARI MAGEREZA MUGUMU AJIUA AKIWA LINDO.

Na Anthony Mayunga-Serengeti
Oktoba 9,2012.

ASKARI magereza wa gereza la mahahusu lililoko mjini Mugumu wilayani
Serengeti Alphonce Mayuma(21)amejiua kwa kujipiga risasi mdomoni na
kutokea kisogoni  wakati akiwa kwenye lindo.

Tukio hilo ambalo limethibitishwa na polisi na uongozi wa hospitali
teule ya Nyerere ddh linadaiwa kutokea oktoba 9 majira ya saa 4:15
asubuhi gerezani hapo wakati akiwa kazini.

Chanzo cha uamzi huo hakijawekwa wazi lakini habari kutoka kwa baadhi
ya maaskari zinasema kuwa askari huyo alichukua fedha za mwenzake kwa
njia ya wizi baada ya kujua namba yake ya siri.

“Alichukua tsh 220,000= na mwenzake baada ya kubaini walifikishana
kwenye uongozi wa gereza na kukiri na kisha kulipa ,tukio ambalo
limetokea hivi karibuni,lakini baada ya kulipa alionekana mwenye
msongo wa mawazo”kilisema chanzo kimoja.

Inadaiwa kuwa mara baada ya kulipa hizo fedha aliombwa kuandika
maelezo kitendo ambacho inadaiwa kuwa kilimstua na akawa akihoji
sababu za kuandika maelezo ili hali wamemalizana walilenga kumfukuza
kazi.

"Aliuliza mara kwa mara kuwa wanataka kumfukuza kazi ,iweje kama
amechukua fedha benki na kumrudishia inakuwaje wanamfuata fuata
tena"alisema askari mmoja jina limehifadhiwa.

Kutoka na hali aliyoonyesha oktoba 8,mwaka huu alinyimwa bunduki
wakati alipokuwa anaingia zamu ya usiku,hata hivyo oktoba 9 asubuhi
amekabishiwa bunduki wakati anaingia  zamu kwenye kidungu cha gereza
ndipo akajipiga risasi moja na kufa.

No comments:

Post a Comment