Thursday, October 18, 2012

WATAKA KATIBA IFUNDISHWE MASHULENI





Na Lucas Raphael,Kaliua
 
WANAFUNZI wa shule ya sekondari kashishi wilayani kaliua mkoani Tabora wamesema kuwa katiba itakayo patikana ifundishwe mashuleni kama somo linalo jitegemea kuanzia shule za Awali hadi  vyuo vikuu 

Walisema hayo wakati wakichangia maoni ya katiba mpya ambapo tume ya kukusanya maoni hayo bado inaendelea na mchakato huo mkoani Tabora. 

Staphen kakumbi mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari kashishi iliyopo wilayani hapa,alisema kuwa katiba itakayo patikana ifundishwe kwa wanafunzi hao kuanzia Elimu ya Awari hadi chuo kikuu.

Alisema kuwa wanafunzi wengi hawafahamu nini maana ya katiba hivyo kila mwanafunzi hana baudi ya kupata msaada wa Elimu hiyo.

Akizungumuza na mwananchi mwanafunzi huyo baada ya kutoa maoni yake alisema kuwa lengo la kuchangia maoni hayo ni kuhakikisha kila mwanafunzi anafahamu vipengele vya katiba na mambo muhimu yaliyomo katika katiba hiyo.

Mwalimu wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Nicolaus mushi alisema kuwa katiba aindikwe kwaa lugha mbili ya Kiswahili pamoja na Kiingereza ili kuwapa fursa wananchi wengi kuweza kuielewa katiba hiyo.  

Nicolaus alisema kuwa katiba hiyo ni m uamara wa maisha hivyo lazima kila mtanzania apate katiba hiyo ili kupanua wigo mkubwa kwa wananchi katika kuelewa katiba.
 
Baadhi ya maoni yaliyotolewa na wananchi hao kuwa nipamoja na kuwa na serikali tatu,rais apunguziwe madaraka yake pamoja na viti maalu kwa wabunge na madiwani vifutwe.
 
Mwisho.

No comments:

Post a Comment