Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati,
Ghuba ya Uarabu na Uajemi linawahamasisha Watanzania wajitokeze kwa
wingi kwenda kumshangilia Francis Cheka katika mpambano wake na Benjamin
Simon wa Ujerumani.
Mpambamo huo ambao utafanyika
tarehe 18 November 2012 katika ukumbi wa Universal jijini Berlin nchini
Ujerumani utawakutanisha miamba miwili iliyosheheni kila aina ya ujuzi
wa kupigana.
Watanzania wawe na tabia ya kuwaenzi wenzao wanapowakilisha taifa hili kama wenzetu wanchi nyingine kama Kenya na Uganda wanavyofanya. Mbali na watanzania watakaokwenda
wakifuatana na Francis Cheka tokea nyumbani, pia watanzania wanaoishi
nchini Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya kama Uingereza, nchi za
Skandinavia, Ufaransa, Uholanzi, Hungary na nyingine wanaombwa
kujitokeza kwa wingi ili waweze kumshangilia Mtanzania mwezao aweze
kupeperusha bendera ya nchi yetu vizuri.
Tayari mtangazaji maarufu wa ITV
na Radio One “Maulid Baraka wa Kitenge” pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Jambo Concept inayomiliki magazeti ya Jambo Leo, City Sports Lounge,
Jambo Magazine Brand Tanzania bwana Juma Abbas Pinto aliye pia mjumbe wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wameshaonyesha nia ya kwenda Ujerumani
kulitangaza pambano hilo kwenye vyombo vyao vya habari pamoja na
kumshangilia Francis Cheka.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
inahamasishwa pia itumie nafasi hii kuitangaza nchi yetu huko Ulaya kama
zinavyofanya bodi nyingine kama za Kenya, Botswana, Uganda, Oman na
nyinginezo zinazotumia wanamichezo wake kutangaza vivutio vya kitalii
nchini mwao.
“Tunaishauri Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) izitumie nafasi ambazo watanzania wanawakilisha nchi ili
kutangaza vivutio vyake vya katalii”.
No comments:
Post a Comment