KIBAO CHA KUINGIA SHULENI
KITABU CHA MAPOKEZI ENZI HIZO
WANAFUNZI WAKICHUTA MAJI
MMOJA YA WAFANYAKAZI WA SHULE HII
ENEO LA SHULE YA TABORA WASICHANA
Tabora
Shule
ya Sekondari ya Wasichana Tabora (pichani juu) iko karibu na shule ya
Tabora Boys, ni miongoni mwa shule kongwe, zilizosifika na bado
inaendelea kusifika kwa kiwango cha elimu watoacho.
Shule
hiyo iliyoanzishwa mwaka 1928 kama shule ya msingi kwa wakati huo wa
ukoloni, ilijulikana kwa jina la African Girls School. Shule hiyo yenye
ukubwa wa hekta zaidi ya 97, ilianzishwa na wakoloni wa Kiingereza kwa
madhumuni ya kutoa elimu kwa watoto wa kike wa machifu.
Mwaka
1957, shule ilipewa hadhi ya kuwa sekondari ya wasichana ambapo mwaka
1972 ilianza kusajili wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye
ulemavu wa ngozi (albino) na wasioona.
Kaulimbiu
ya shule ni strive to excel yaani kazana ufanikiwe, huu ni ukweli
unaobainishwa na uwepo wa wanataaluma waliobobea katika fani ya sheria,
udaktari, uhandisi, ualimu na hata katika siasa waliosoma katika shule
hiyo.
Miongoni
mwa viongozi waliosoma katika shule hiyo ni pamoja na Mke wa Rais
mstaafu na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna
Mkapa, aliyewahi kuwa Rais wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Ukerewe,
Getrude Mongella.
Wengine
ni aliye kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margareth
Sitta na aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira), Dk. Batilda Buriani.
Pia
aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani, aliyekuwa Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wanawake (UWT- Taifa) Anna Abdallah, Katibu Mtendaji wa
Baraza la Mitihani la Tanzania, Dk. Joyce Ndalichako.
Wamo
pia Jaji mstaafu Julie Manning, Jaji wa Mahakama Kuu, Eusebia Munuo na
aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi Duniani (UN Habitat), ambaye
sasa ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Nidhamu
ya shule hiyo ni jambo ambalo linawasaidia wanafunzi wasomao shuleni
hapo kuwafungulia milango ya mafanikio katika maisha yao.
No comments:
Post a Comment