Askari
Kanzu akimsindikiza kwa teke mmoja kati ya watuhumiwa waliokamatwa
wakati wa operesheni maalum iliyowekwa katika jiji la Dar es Salaam,leo
mchana ili kuwadhibiti baadhi ya waliodaiwa kuwa ni waumini wa dini ya
kiislam, waliokuwa wamepanga kufanya maandano mchana wa leo baada ya
Swala ya Ijumaa kuelekea Ikulu kwa lengo la kushinikiza kiongozi wao,
Katibu wa Jumuiya za Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda, aliyekamatwa
majuzi,aachiwe. Hata hivyo jitihada za watu hao ziligonga ukuta baada ya
wao kujipanga kutokea kila kona na kukutana maeneo ya Ikulu, lakini la
Askari pia walijiandaa na kujipanga vyema kila kona ya jiji na
kuwadhibiti watu hao.
Vurugu
kubwa ilikuwa katika maeneo ya Kariakoo ambako pia walijitokeza baadhi
ya vijana waliojichanganya na makundi hayo na kuanza kuvamia maduka na
kupora mali za watu na kuwatishia wenye maduka, jambo ambalo liliwafanya
Polisi kuwatawanya kwa kupiga risasi hewani na waliokaidi amri hiyo
walianza kushughulikiwa kama picha hizi zinavyoonyesha Pata Mkanda
Kamili.
Twende garini.....
Akaaaa sio mimi jamaniiiiiii, Babu (kulia} akijitetea...
Askari wakimdhibiti babu...
Babu akishuhshwa garini kuingizwa kituoni.....
Mgambo wa kike akipambana na kijana kumburuta kumpeleka garini, baadaye mgambo huyu CHALIII
Mgambo chaliii,lakini wapi anaye tuuuu....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Jamaa akijaribu kueskep ambapo
alikula bonge la mtama na kutambaa kama hivi na kudakwa na mgambo wa
kike....PICHA ZOTE NA VIJIMAMBO BLOG
No comments:
Post a Comment