Friday, October 12, 2012

KUPIGA KURA IWE MIAKA 15 NA SIO 18 YA SASA WANANCHI



Na Lucas Raphael,Kaliua 

KUPIGA KURA MIAKA 15


Baadhi ya wananchi wa kijiji  na kata ya  Ushokola wilaya ya Kaliua mkoani Tabora wamesema kwamba  umri wa kupiga kura ya uchaguzi mkuu uwe kuanzia miaka 15 na sio miaka 18 ya sasa.

Akitoa maoni yao katika kikao cha tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya kilichofanyika katika ofisi ya mtendaji wa kata ya ushokola Felishiani Teodori kuwa umri huo uwe kuanzi miaka 15  kutokana na uelewa wake wa  umri huo ni mkubwa.

Felishiani alisema kuwa kijana mwenye umri wa 15 anauwezo wa kutambua mambo mema na mabaya hivyo hakunasababu za msingi zinazo weza kumzuia kijana huyo.

Wakichangia kwanyakati tofauti wananchi hao walisema kuwa viongozi wa kuteuliwa na wananchi hususani wabunge waongoze kwa miaka kumi.(10).

Walisema kuwa wabunge wengi baada ya kuchaguliwa na wananchi huhamia katika miji mikubwa na kuwaacha wananchi pekee haliambayo wananchi hao hushindwa kutoa kero hizo kwa kiongozi huyo.

Akitoa maoni yake Yusuph Juma mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa mbunge endapo akatoa ahadi kwa wananchi na kutokufanikisha ahadi hizo kwa muda wake afikishwe mahakamani kujibu tuhuma hizo za kuwadanganya wananchi.

Yusuph aliongeza kuwa kwa upande wa madiwani wapatiwe miaka hiyo 10 ya kugombea pia nafasi za wabunge wa kuteuliwa zifutwe na badala yake wabunge wote wachanguliwe na wananchi.

Maoni mbalimbali yaliyo telewa na wananchi hao ni pamoja na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania apunguziwe madaraka yake pamoja na baraza la mawaziri lichaguliwe na wabunge wa jamuhuri ya Tanzania.

Tume hiyo inaendelea na mchakato wa kukusanya maoni hayo katika wilaya ya kaliua mkoani Tabora.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment