Na Lucas
Raphael,Tabora
Wananchi wa kata
ya kipili wilayani sikonge mkoani Tabora wamesema katiba mpya izingatie
mawasiliano ya miundombinu,simu pamoja na kupata mawasiliano ya vyombo vya
habari kulingana na maeneo husika.
Wakitoa maoni ya
katiba mpya pindi tume hiyo ilipo tembelea kata hiyo walisema kuwa mawasiliano
ya simu yapewe kipaumbele kwa jamii ili kupata fursa ya kupata mawasiliano ya
kupashana habari.
Wananchi hao
wakizungumza kwanyakati tofauti walisema kuwa katiba izingatie mawasiliano ya
jamii ili kila mwananchi wa Tanzania
aweze kupata fursa ya kupashana habari na kupata habari kutoka eneo moja hadi
eneo jingine.
Wananchi hao wa
kata hiyo hawana mawasiliano ya simu,miundombinu mibovu wakati wa kipindi cha
mvua pamoja na mawasiliano ya vyombo vya Habari haliambayo ilichangia wananchi
hao kuomba katiba izingatie huduma hiyo hususani vijijini.
Emmanueli Ndege
alisema kuwa katiba izingatie huduma hiyo muhimu kwa jamii ili wananchi
wanufaike na fursa hii ya utandawazi tofauti na hali ilivyo sasa baadhi ya
wananchi hawana mawasiliano.
“mawasiliano ni
kitu muhimu sana kwa wananchi kwani eneo hili
tunaweza tukapata majanga,ama matukio inakuwa ngumu kutoa taarifa lakini kama mitandao inakuwepo taarifa zina tolewa kwani kwa
sasa simu zetu zinaozea mifukoni.’’alisema mkazi huyo.
Osca John
akichangia maoni yake aliongeza kuwa endapo makuampuni yamawasiliano yanaingia
mikataba na serikali yawekewe sheria ya kuhakikisha eneo husika wanapata
mawasiliano kulingana na mikataba hiyo ilivyofungwa na sikwakuchagua eneo mmoja
Tume hiyo ya
katiba kundi la tisa la mkoa wa Tabora lilisafiri umbali wa kilometa 380
kuwafuata watanzania wa kata hiyo kutoa maoni yao juu ya katiba mpya ambapo tume hiyo
ililazimika kufanya mkutano mmoja kulingana na changamoto za umbali pamoja na
miundombinu.
Hata hivyo
wananchi wa kata ya kipili na kitunda walisema kuwa viongozi wa kiserikali huwa
hawafiki maeneo hayo kwanyakati mbalimbali mpaka matukio ya kitaifa yafike hali
ambayo hujihisi kama wametengwa na serikali yao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment