Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi
ujenzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Oman katika mtaa wa
balozi jijini Muscat Oman jana.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, (watatu kushoto) ni Balozi wa
Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh na (kulia) ni Afisa Mwandamizi
Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Bwana Abdallah Kilima.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua ujenzi wa jengo la ubalozi wa
Tanzania nchini Oman jana.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe,watatu kushoto ni Balozi wa
Tanzania nchini Oman, Bw. Ali Ahmed Saleh, (wanne kulia aliyeshika
karai) ni Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Bw.
Abdallah Kilima na (kulia anayeshuhudia) ni Afisa katika Ubalozi huo,
Bw. Saidi Mussa.Picha na Freddy Maro-IKULU
Serikali
ya kifalme ya Oman inatarajia kutuma ujumbe wake ambao utajumuisha
na wafanyabiashara kuja Tanzania kutathmini na kuangalia maeneo gani
nchi hiyo na wafanyabiashara wake wanaweza kuwekeza ,kufuatia ziara ya
kiserikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ya siku 4 nchini Oman.
“Tutaunda
kamati na kutuma ujumbe kwenda Tanzania kuangalia na kujua aina gani
ya biashara na vitega uchumi Oman inaweza kuwekeza”.AmesemaNaibu
Waziri Mkuu wa serikali ya kifalme ya Oman, Mheshimiwa Sayyid Fahad
Mahmood Al Said wakati wa mazungumzo yao ya kiserikali.
Naibu Waziri Mkuu huyo amesema Oman ina matumaini makubwa kuhusu mazungumzo yao ya tarehe 17
Octoba, 2012 yaliyofanyika katika makao makuu ya Baraza la Mawaziri.
Octoba, 2012 yaliyofanyika katika makao makuu ya Baraza la Mawaziri.
Amesema
Baraza la Mawaziri la nchi yake litakaa na kujadiliana pamoja na Chama
cha wafanyibiashara na Viwanda kuandaa serikali ya kuja Tanzania na
kuhakimisha mahusiano yetu yanadumu.
Rais
amemueleza Makamu wa Waziri Mkuu kuwa Tanzania hivi karibuni imegundua
gesi kwa wingi na hivyo kuna changamoto kubwa ya kujenga uwezo kwa watu
wake waweze kujadiliana na kuwekeana mikataba itakayoleta tija kwa Taifa
na watu wake.
Rais
Kikwete pia amekutana na watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchini
Oman ambapo amewaeleza kwa kifupi maendeleo yanayoletwa na serikali
katika Nyanja za Kilimo, Elimu, Afya, miundombinu na mambo mbalimbali ya
kisiasa yanayoendelea nchini Tanzania.
Watanzania
hao, nao wamepata nafasi ya kuelezea matatizo na matarajio yao kwa Rais
, ambapo Rais amewapata nafasi ya kufafanua na kujibu baadhi ya hoja
zao na kuwapa changamoto watanzania wote wanaoishi nchi za nje ya
kushiriki katika shughuli za maendeleo na kukuza Uchumi wa Tanzania
kwa kutafuta na kushawishi wawekezaji na marafiki mbalimbali kusaidia
katika nyanja mbalimbali ambazo zinahitaji misaada ya maendeleo.
Rais anamaliza ziara yake tarehe 19 Octoba, 2012 na kurejea nyumbani jioni.
No comments:
Post a Comment