Friday, October 12, 2012

WAKULIMA WATAKA MWAKILISHI WAO MBUNGENI.


 Na Lucas Raphael,Kaliu



Wananchi wa wilaya ya kaliua mkoani Tabora jana hasa wakulima walisema kuwa katika mbunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania wapatiwe mwakilishi wao atakaye wawakilisha katika Bunge hilo kwenye maswala yote yanayohusu kilimo na mifugo.

Wakichangia maoni yao kwanyakati tofauti katika tume huru ya kuchangia maoni ya kupata katiba mpya kikao hicho kilicho keti katika viwanja vya mnadani jana walisema kuwa wapatiwe mbunge.

Hamis mfaume mkazi wa kaliua mjini akichangia maoni katika tume hiyo alisema kuwa wakulima hawana mwakilishi bungeni hali ambayo wanajikuta wanapoteza haki zao.

Alisema kuwa baadhi ya makapuni yanayonunua mazao yao huchukua asilimia kubwa kuliko mkulima kwa kisingizio cha pembe jeo haliambayo mkulima hukosa faida ya kilimo hicho.

Kwanyakati mbalimbali katika viwanja hivyo wananchi hao walilaani makapuni hayo yanavyo wanyonya katika kilimo chao.

Godfrey Mshahila mkazi wa eneo hilo alisema endapo wakulima hao wakapatiwa nafasi ya kuwa na mwakilishi haki zao za msingi zitapatikana tofauti na wakati huu hakunja mwakilishi.

Alisema kuwa hata mbunge huyo mkulima afanane na mazingira ya mkulima na uchaguzi huo ufanyike kwa wakulima hao tu.

‘’hata mbunge huyo mkulima lazima awe anafanana na mkulima pamoja na uchaguzi wake ufanyike na wakulima husika ili mtupate ufumbuzi juu ya suala hili.

Kauli hiyo imetokana na asilimia kubwa ya wananchi wa wilaya hiyo kujihusisha na kilimo cha tumbaku ambapo baadhi ya wakulima hukosa haki zao za msingi ambazo wengiwangeweza kuzipata haki hizo kwa nyakati mbalimbali.

Wakihitisha zoezi hilo la kuchangia maoni yao walimtaka mwenyekiti wa tume hiyo katika mkoa wa Tabora Salima Ally kuhakikisha maoni hayo yanafika katika idara husika ili yafanyiwe kazi .

Awali ya hapo mwenyekiti huyo akifungua kikao hicho alisema kuwa kila maoni yata heshimika na kufikishwa katika pahala pahusika.

Mwisho.


No comments:

Post a Comment