Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda
akisalimiana na mratibu wa mahusiano baina ya Global Fund na Mabunge
Duniani Ndg. Svend Robinson, walipokutana kabla ya kuanza kwa mkutano
wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec,
Canada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda
akimtambulisha Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe.
Dr. Perpetua Nderakindo Kessy kwa Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe.
Alex Massinda kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge
Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec, Canada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda
akifuatilia taarifa mbalimbali na maazimio ya Mkutano wa Chama cha
Mabunge Duniani (IPU) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 127 wa IPU Mjin
Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe.
Alex Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
Mkurugenzi wa Maktaba na Utafiti wa
Bunge Ndg. Kileo Nyambele anaye muwakilisha katibu wa Bunge Dkt. Thomas
kashilila akishiliki kikao cha makatibu wa Mabunge yote wanachama wa
Mabunge ya Dunia (IPU) katika Mkutano wa 127 wa chama hicho mjini
Quebec, Canada. Kulia kwake ni Afisa dawati la IPU kutoka Tanzania Ndg.
James Warbarg.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda
akiongoza ujumbe wa Tanzania kupiga kura kuingiza agenda mojawapo kati
ya agenda 5 za dharura zilizowasilishwa kwa udharura katika mkutano wa
127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) ili zijadiliwe pia. Tanzania
iliungana na nchi za Afrika kupigia kura agenda ya kujadili hali ya
usalama katika nchi ya Mali pamoja na agenda iliyowasilishwa na
Uingereza kujadili kwa udharura swala la hatma ya Usalama na Misaada wa
Kibinadamu Nchini Syria na nchi Jirani. Kushoto kwake ni Balozi wa
Tanzania Chini Canada Mhe. Alex C. Massinda na Mhe. Hamad Rashid
Mohamed.
Spika wa Bunge akitoka katika ukumbi
wa Mikutano mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kwanza katika Mkutano
wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) mjini Quebec, Canada. Kushoto
kwake ni Mhe. David Kafulila anayehudhuria Mkutano huo pia.
Mhe. Anne Makinda akitoka katika
Mkutano na Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Karim Ghellab kwa lengo la
kufanya nae mazungumzo ya faragha kuimarisha uhusiano baina ya mabunge
ya Tanzania na Morroco.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda
akisisitiza jambo wakati alipokutana na Spika wa Bunge la Morocco Mhe
Karim Ghellab kujadili namna bora ya kuimarisha mahusiano baina ya
mabunge ya nchi zao. Tanzania ilipeleka ujumbe wa Wabunge kutoka kamati
ya Mambo ya Nje, ulinzi na Usalama kutembelea Bunge la Morocco Aprili
mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi
mbili.
Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab akimkabidhi Mhe. Spika zawadi mara baada ya kufanya nae Mazungumzo.
Ujumbe kutoka Bunge la Tanzania
katika Mkutano wa 127 wa IPU Mhe. Hamad Rashidna Mhe. Suzan Lyimo
wakifuatilia kwa makini mada kuhusu “Multilateralism and the role of
parliament in parliamentary diplomacy” wakati wa mkutano huo Mjini
Quebec, Canada.
No comments:
Post a Comment