Kutoka maktaba ya KAPIPIJhabari.COM:-Bw.Ghulam Dewij akiwa anapokea taji la maua kutoka kwa binti yake kama pongezi ya kuchaguliwa kuwa Meya wa manispaa ya Tabora.
Hivi
kama angekuwa Ghulam ni mbaya kiasi hicho mnacho mzushia angeweza
kuaminiwa na wengine kama ilivyo sasa hata kufikia hatua jina lake
limekwenda Dodoma na kurudi Tabora kisha wajumbe wenye akili timamu wa
Jumuiya ya Wazazi wakamchagua kwa wingi wa kura hizo alizopangiwa na
Mwenyezi Mungu kuzipata kuwa Mwenyekiti wao!....AMA KWA HAKIKA
ALIYEANDIKIWA YES NI YES TU HAKUNA KINGINE.............Ndugu zangu hebu
Tabora mjini tubadilike anayeonesha uwezo wake katika kutenda jambo zuri
kwa manufaa yetu sote tujaribu kumsapoti tutaona manufaa yake kwa muda
mfupi na sio kumtafutia dhahama na kumpaka matope bure,sio uungwana huo.
Kutoka maktaba ya KAPIPIJhabari.COM:-Bw.Ghulam
wakikumbatiana na diwani wa kata ya Gongoni ambaye pia ni mkurugenzi wa
Kampuni la Usafirishaji la NBS LTD mara baada ya kuteuliwa na CCM
kuwania nafasi ya Meya wa manispaa wakati huo.
LICHA ya kuwepo kwa vijimambo
vilivyodumu kwa siku kadhaa ambavyo naweza kusema visivyo na miguu wala
kichwa,Mbele wala nyuma,Chini wala juu ambavyo havikuwa na mashiko ya
aina yoyote na wala haviingii akilini kwa mtu mwenye akili
iliyosalama,Sana sana vilizidi kuwatia Presha waliovianzisha na baadaye
kupatikana wengine kuvikumbatia licha ya kuwa mara kadhaa akili
zilipowarudia walijikuta wakifikiria huenda wakawa na mapungufu makubwa
kichwani.
Niliendelea kujiuliza wakati wote
nilipokuwa nikiyasikia hayo waliyokuwa wakimzushia Bw.Ghulam,na
nilipojaribu kuyafuatialia kwa karibu zaidi nikagundua ni chuki zisizo
kuwa na maana yoyote ile kwani pamoja na kuwasikiliza hao waliokuwa
wakipita wakiyasema ndio walikuwa vinara wakubwa wa majungu hayo, na
karibu wakati wote hawakuwa na ushahidi kwa yale wanayoropoka
Sina nia mbaya lakini itabidi
mnifikirie wenyewe kunisamehe hata kama sijawaomba msamaha kwani sina
muda wa kufanya hivyo pale ninapogundua kuwa kuna ukweli kwa yale ambayo
mnayazusha halafu mkitakiwa kutoa ushahidi mnakosa majibu,kwakweli
nathubutu kusema ACHENI UNAFIKI,mwacheni kijana wa watu afanye kazi
aliyotumwa na wananchi msiendekeze maslahi yenu binafsi.
Ghulam Dewij nakubali kuwa ni
kiongozi ambaye bado nyota yake inazidi kung'ara ndani na nje ya
CCM,....Hebu jaribu kufanya mahesabu wewe mwenyewe, Ghulam mbali na
kushika nafasi mbalimbali katika Chama chake ambazo alionekana kuwa ni
mfano wa kuigwa kwa kile kinachodaiwa kukisaidia chama katika kuimarisha
masuala kadhaa ya kimsingi lakini pia amekuwa mstari wa mbele na kuwa
karibu zaidi na wanachama wenzake pasipo kubagua kiongozi au mpiga debe
wa chama,kwake yeye wote walikuwa ni muhimu.
Hili ndio linadhihirisha kuwa
Ghulam ni kiongozi aliyekuwa akikubalika na wadau wote wa ndani ya chama
nikiachilia mbali hao walioko nje ya chama ambao Ghulam ameonekana mara
kadhaa akishiriki shughuli za kijamii huko mitaani kama shida za maafa
na furaha za harusi na mengineyo.
Alipochaguliwa kama diwani wa
Kanyenye hii ilikuwa ni mara ya pili kwa wadhifa wa aina hiyo kwa kata
tofauti,nikimaanisha kote huko alikuwa anakubalika Kata ya Mbugani na
Kanyenye.
Sasa akachaguliwa kuwa Meya wa
manispaa ya Tabora na kuanza kuonesha uwezo wake katika kuyatekeleza
yale aliyotumwa na wananchi na hatimaye hata heshima na hadhi ya
manispaa yetu imeanza kurudi,....Hili likawa mwiba kwa wale waliotaka
kumuendesha vile wanavyotaka wao na tena ni kwa maslahi yao binafsi
jambo ambalo Ghulam Dewij aliliona si haki kwa kufanya hivyo kwa wajanja
wachache ambao sasa walimgeuka na kuanza kutengeneza hayo ambayo
yaliwaingia vichwani mwao na kumzushia kila aina ya ubaya....na mbaya
zaidi eti wakadiriki hata kuandaa mpango wa kumuondoa katika wadhifa wa
Meya wa Manispaa.
Ni mengi niliyonayo ukiachilia
mbali na lile la kutaka kumchonganisha na mkuu wa mkoa wa Tabora
ilimradi aonekane kuwa hafai.....Jamani Jamani!!!!hivi kama hafai ni
nani ambaye angefaa....Acheni UZUSHI.
BABU WA MIAKA 50 ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUTAKA KUIBA MBAO -SINGIDA
Mwanaume
anayekadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 50 aliyenusurika kuuawa kwa kile
kilichodaiwa alikuwa akitaka kuiba mbao kwenye nyumba moja mtaa wa
Misuna mjini Singida.Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina moja la Mwera
(pichani) ambaye anafanya kazi ya kusukuma toroli stand mpya ya
Misuna,inadaiwa usiku wa kuamukia leo wakati akijaribu kuingia ndani ya
nyumba ambayo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika kupitia
dirishani, miguu yake ilinasa kwenye nondo za dirisha na kushindwa
kuingia ndani.
Baada ya kushindwa kuingia
ndani,wakati akitaka kutoka kwa nguvu miguu yake iliyonasa kwenye
nondo,mikono yake ilitereza na kusababisha aning’ing’ie kichwa chini na
miguu ikiwa juu dirishani kuanzia alfajiri hadi aliponasuliwa saa mbili
kasoro robo asubuhi.
Baadhi
ya wakazi wa manispaa ya Singida wakimshangaa mwanaume huyo huku
akijaribu kuficha uso wake.Alinusurika kuuawa baada ya mpiga debe mmoja
Sele,kuwasihi watu hao ambao tayari walikuwa wamebeba silaha za
jadi.Picha ya pili,baada ya mpiga picha hii kumvua fulana yake kwa nguvu
na sura yake kuonekena.Picha na Nathaniel Limu.
No comments:
Post a Comment