Na Mwanshi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
……………………….
Jeshi la Polisi zanzibar
limetangaza kuzifunga baadhi ya barabara za mji wa Zanzibar ili
kuwawezesha wananchi wakiwemo watoto wadogo kusherehekea siku kuu ya
Eddi el Haji kwa usalama na amani.
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la
Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amezitaja baadhi ya barabara
zitakazofungwa kwa muda wa siku nne kuanzia Ijumaa wiki hii hadi
Jumatatu wiki ijayo kuwa ni ile inayotoka Mnazi Mmoja hadi Viwanja vya
michezo vya Maisala, barabara ya kutoka Ofisi ya Baraza la Wawakilishi
la Zamani kuelekea Viwanja vya Maisala na Barabara ya ya kutoka Ukumbi
wa CCM kuelekea Mnazi Mmoja.
Inspekta Mhina, amesema kuwa
barabara hizo zitafungwa kuanzia majira ya saa 9.00 arasili hadi saa
4.30 usiku kwa kila siku muda ambao watu wengi watakuwa wamesharejea
majumbani kwao baada ya kusherehekea siku hiyo.
Awali akitoa taarifa kwa vyombo
vya habari mjini Zanzibar, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi
Ungauja ACP Aziz Juma Mohammed, alisema kuwa sherehe hizo zitaadhimishwa
kwa muda wa siku nne mfululizo zitaanza Ijumaa ya Oktoba 26 hadi
Jumatatu ya Oktoba 29 2012.
No comments:
Post a Comment