Saturday, December 21, 2013

AJALI YA LORI YAUA WANNE YAJERUHI ZAIDI YA 30-TABORA



 

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Peter Ouma akiangalia Lori aina ya Isuzu lenye nambari za Usajili T829 AHH mara baada ya kuanguka na kusababisha vifoo vya watu wanne na majeruhi zaidi ya 30 katika ajali iliyotokea Tarafa ya Ilolangulu wakati lilipokuwa likienda mnadani huku likiwa limebeba wafanyabiashara wa mitumba pamoja na mizigo mbalimbali.
Tairi la Lori hilo ambalo lilikuwa bovu lilipasuka na kusababisha ajali hiyo mbaya.
Dereva wa Lori hilo Isuzu Bw.Ally Athuman ambaye alikutwa eneo la ajali hiyo mbaya
Baadhi ya wananchi waliofika eneo la ajali wakishuhudia Maiti zilizokuwa zimekusanywa kwenye gari la Polisi muda mfupi mara baada ya ajali kutokea.
Madaktari chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa ya Kitete mkoani Tabora wakijaribu kuandika majina ya watu waliopoteza maisha na wale waliojeruhiwa.
Kikosi maalumu cha huduma ya kuokoa afya ya majeruhi katika hospitali ya Kitete ambacho kilichukua hatua za haraka na makusudi kushughulikia majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo.
Idadi kubwa ya watu walivunjika miguu na mikono mbali na wale waliopoteza maisha ambao majeraha makubwa walipasuka vichwa na kuumia vifuani.


No comments:

Post a Comment