Na Lucas Raphael,Urambo
WATU watatu wamefariki dunia baada ya kula mboga aina ya uyoga unaodhaniwa
kuwa na sumu wilayani Urambo mkoani Tabora.
Alizungumza na waandishi wa
habari katika hospital ya wilaya ya urambo, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo,
Dk.Kheri Kagya,alisema kwamba watu hao
walikuwa wanane na walikula ugali kwa mboga aina ya uyoga ambao unadhaniwa kuwa
na sumu katika kijijini Igunguli, katika Kata ya Uyogo wilayani humo.
alisema kwamba mmoja wa wazazi katika
familia hiyo Makoye Tongele (35) aliamua kuwapeleka Hospitali ya wilaya ya
Urambo, watoto Kija Makoye (3) aliyefariki njiani na Wande Mahinge (5) na
Mahigi Tongele waliofariki wakipata matibabu katika Hospitali hiyo.
Dk. Kagya alibainisha
kuwa wengine waliokula chakula hicho walisalimika akiwemo Baba wa watoto hao
Makoye pamoja na watoto wengine Gimili Makoye(miezi kumi) na Talekwa Mahigi(3)
akiwemo pia aliyepika chakula hicho Nyanzobe Mswahili(25).
Dk.Kagya alisema wameshindwa
kuchukua sampuli ya chakula hicho kinachohisiwa kuwa na sumu kwa vile kililiwa
chote na hata aina ya uyoga wameshindwa kuutambua kwa vile nao ulichumwa wote.
Ameeleza kuwa Nyanzobe
aliwaeleza kuwa uyoga aliochuma porini ulikuwa unafanana na
uyoga waliowahi kula na hivyo kukwama kuutambua uyoga huo.
Kamamda wa Polisi Mkoani
Tabora,Kamishna Msaidizi wa Polisi Peter Ouma alisema wamepata taarifa za tukio
hilo na kusisitiza kwamba wananachi kuwa waangalifu kipindi hiki cha masika
kwani uyoga nyingi zinaota kutokana na rutuba zilizopo maeneo mbalimbali kwa
ajili ya mvua zinazonyesha mkoani hapa
Hata hivyo aliwataka wananchi
wanaopenda mboga aina hiyo kuchukua tahadhari ili wasikutane na mboga aina ya uyoga wenye sumu kama huo .
mwisho-
No comments:
Post a Comment