Na Lucas Rphael,Nzega
MAHAKAMA ya Hakim mkazi wilayani Nzega
Mkoani Tabora imewahukumu watu wa wa 4 kwenda jela miaka 120 kutokana na
kukutwa ha hatia ya kufanya unyan`ganyi kwa kutumia silaha.
Waliotiwa hatiwa hatiani na mahakama
hiyo ya hakimu mkazi ni ,Joseph Manala(38),Emmanuel
machibya(20)Juma Lutalamula(30)Juma msabato(42).
Akisoma hukumu hiyo hakim mkazi wilaya
ya nzega, Silvester Kainda watuhumiwa wa nne (4) wametiwa hatiani kwa kosa
la kuvamia kwa kutumia siraha na kupewa hukumu ya miaka 120 huku kila mmoja
akitumikia miaka 30 gerezani.
Alisema kwamba vitendo vya unyan`ganyi
kwa kutumia silaha vimekuwa vikiongezeka kila siku jamboo ambalo linatishia
amani ya watanzania hivyo dhahabu kali ndio lilio sahii kwa watu waina hii.
Alisema kwamba hiyo iwe fundisho kwa
watu wengine wenye tabia kama hiyo ya kupara mali zawatu ambao wametafuta kwa
jasho lao na wengine kuchukua mali hizo kama zao..
Hakimu kainda aliiambia mahakama hiyo
kwamba ushidia uliotolewa mahakani hapo umeonyesha bila shaka na kufanya
mahakamni iweze kuwatia hatiani washitakiwa hao kwani nikweli walitenda kosa
hilo .
Hata hivyo mahakama hiyo imewaachia
huru watuhumiwa wawili baada ya kuonekana kutokuwa na hatia katika shitaka hilo
kuwa ni Peter Steven (30) pamoja na Ramadhani Juma (19).
Awali mwendesha mashitaka wa Jeshi la
polis wilaya Melito Ukongoji aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo April 5
mwaka huu katika cha kijiji cha Itanana kata ya Bukene walikuiba Duka la
Joakim John mkazi wa kijiji hicho kisha na kumjeruhi vibaya mwili wake.
Mwendesha akisoma shitaka hilo
alisema kuwa watuhumiwa hao waliiba fedha zaidi ya laki saba na kufanya
uhalibifu mkubwa wa mali ikiwa na kumjeruhi Joakim John huku wakitumia siraha
aina Gobole na mapanga.
Kabla ya kutolewa kwa hukum hiyo
mwendesha mashitaka Melito aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa
watuhumiwa hao kutokana na kukithiri kwa matukio hayo ili iwe fundisho kwa watu
kama hao.
Wakati wa kujitetea watuhumiwa hao
waliiomba mahakama hiyo itoe hukum ndogo kutokana na baadhi yao kuwa ni
waathirika wa Virusi vya ukimwi huku wengine wakikabiliwa na majukum ya
kifamilia.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment