NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
Safari ya mwisho wa mwandishi wa habari wa siku nyingi Hamis
Bakari kikoroma maarufu kama Ben kiko (70) ilitimishwa jana katika kijiji cha
ndaukilo kitogoji cha usupilo wilayani sikonge mkoani Tabora katika mazishi
yaliohudhuriwa na watu mbalimbali mkoani
hapa.
Mazishi hayo yakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Tabora Sulemani
Kumchaya kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa tabora Fatuma mwassa naambapo aliwataka waahdishi wa habari
hapa nchini kuinga yale yote yaliomema
aliyofanya mwandishi huyo mkongwe hapa nchini
Alisema kwamba kwamba waandishi wa habari na vijana kwa ujuma
wake wanatakiwa kuwa wazalendo kwa nchi
yao kama alivufanya marehemu katika uhai wake kwa kutumikia nchi yake katika
vita ya kagera na sehemu mbalimbali ambazo alifanya kazi kwa kujituma .
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kila mtu anatakiwa kujitoa
kwa ajili ya nchi yake na sio kuweka maslahi ubinafsi mbele kwani huo sio uzalendo bali kutoa
kwa nchi kama alivufanya ben kiko wakati wa utendaji wake wakazi.
Alisema kwamba licha ya kufanya kazi tbc kwa vipindi tofauti tofauti
bali alikuwa ni mfanyakazi katika Redio ya Tabora VOT na kuwa mwalimu wa waandishi
wa habari katika mchuo cha musoma Utalii Tawi la Tabora .
Marehemu amepata elimu shule ya msingi misheni sikonge kabla
ya kwenda chabutwa kusoma elimu ya kati mwaka 1959-1962 shule ya wavulana
tabora kidato nne kabla ya kuhudhuri mafunzo ya ualimu ya miaka miwili katika
chuo cha ulimu mpwapwa mkoani Dodoma na kufanikiwa kupata cheti cha ualimu daraja A.
Aidha mwaka 1984-1985 alikwenda nchini India kupata mafunzo ya
uandishi wa habari ya ngazi ya Diploma .
Ben kiko hadi mauti yanamfika alikuwa mwenyekiti wa mtaa wa
uhazili uliopo katika kata ya kanyenye manispaa ya Tabora ameacha wajane watatu na watoto kumi.
SHEKHE SALUM MAHARUKI AKIONGOZA SALA YA KUUONBEA MWIILI WA MWANDISHI WA SIKU NYINGI NCHI HABARI BEN KIKO NJE YA NYUMBANI YAKE KATIKA KIJIJI CHA USUPILO WILAYA YA SIKONGE MKOANI HAPA
WANANCHI KUTOKA TABORA MJINI NA WALE WA WILAYA YA SIKONGE WAKIWA KATIKA MKUSANYIKO WA KUKAMILISHA SAFARI WA BEN KIKO
Add caption |